Friday, June 1, 2012

WOLPER: SIJABADILI DINI KWA SABABU YA DALLAS


Jacqueline Wolper.
STAA anayekimbiza ndani ya Bongo Movies, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa dini ya Kiislam aliihusudu siku nyingi kabla hajakutana na mpenzi wake Dallas.
Wolper alifunguka hayo juzikati kupitia Runinga ya Channel Five alipoulizwa kama alibadili dini kwa sababu ya kukutana na mpenzi wake huyo, alikataa na kusema kabla hata hawajakutana yeye alikuwa akipenda imani hiyo.
“Nakumbuka nilikuwa nikiupenda Uislam na kuweka picha zenye viashiria vya dini hiyo ndani kwangu hivyo Dallas alinikuta tayari ninapenda ndipo nikabadili,” alisema Wolper.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...