
Ay amemaliza kufanya video yake mpya huko Afrika Kusini, video ya single aliyomashirikisha producer Marco Chali ambapo itatoka kwenye wiki ya pili ya June.

Marco Chali akifanyiwa Make up kwa ajili ya hiyo video ambayo ni wanaume wawili tu wameonekana ndani yake, Ay na Marco Chali na imefanyika Johannesburg Afrika kusini.

Ay amesema kampuni ya GODFATHER ndio inayoitengeneza hiyo video, mpaka sasa imefanya video nyingi na wakali wengine Afrika kama Chop my money ya P SQUARE, J Martins, Mr Flavour na wengine wengi.

Timu yote ya watu 30 iliyohusika kuitengeneza hiyo video ni ya wazungu tupu, kila mmoja alikua na kazi yake.

Kwenye utengenezaji wa hiyo video walikuja models zaidi ya 30 lakini wengi walichujwa palepale kwenye location.





































No comments:
Post a Comment