Tuesday, June 26, 2012

MISS TZ APIGWA NDOA


MSHIRIKI wa Miss Tanzania 2011/12, Husna Maulid amepigwa ndoa kimyakimya na jamaa mmoja aliyemtambulisha kwa jina la Abubakar Rajab, mkazi wa Ilala, Dar es Salaam nyuma kukiwa na madai kuwa kaolewa na mume wa mtu hivyo ni mke wa pili...


Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii, tukio hilo lilichukua nafasi Ijumaa iliyopita Juni 22, mwaka huu nyumbani kwa kina Husna, Mikocheni Ushindi, Dar baada ya wazazi wake kuridhia binti yao aolewe na mwanaume huyo.



Chanzo hicho kilidai kuwa pamoja na Husna kufahamu kuwa jamaa huyo yupo ndani ya ndoa, hakujali hilo kwa kuwa alidhamiria kuingia kwenye maisha ya ndoa hivyo haogopi ukewenza.



Ilifahamika kuwa wakati Husna akiulizwa na mashehe kama ameamua kuolewa kwa ridhaa yake bila ushawishi wa wazazi au ndugu alikuwa na haya ya kusema:



“Nakiri mbele yenu kuwa nimempenda Abubakar na nimeridhia kuolewa naye bila kishawishi kutoka kwa mtu yeyote.” 
Huko nyuma Husna alipata umaarufu kutokana na tabia yake ya kupenda kupiga picha za utupu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...