Wednesday, August 24, 2011

Mtanzania ajiingizia mamilioni kwa kukaa UTUPU...




MODO maarufu wa Kitanzania, Ida Ljungqvist (pichani) mwenye maskani yake Los Angeles, California nchini Marekani, amekuwa gumzo kwa miaka kadhaa tangu alipokubali kwa hiari yake mwenyewe kufotolewa picha za ‘eksi’ na kujiingizia mamilioni...




Kwa mujibu wa habari zilizochafua vyakutosha katika mitandao mbalimbali duniani zikimuonesha kuwa ni mtu wa ovyo, mrembo huyo mwenye miaka 29 alizaliwa na mama Mtanzania na baba Mswidishi Septemba 27, 1981.




Ilielezwa kwamba, Ida alianza ‘kamchezo hako ka aibu ka kusimama’ mbele ya kamera za majarida mbalimbali nchini humo yanayolipa vizuri akiwa mtupu tangu mwaka 2008 ambapo aliibuka kinara wa picha ‘mbofumbofu’ wa Machi katika jarida maarufu la Playboy la Marekani.




Habari zikazidi kutiririka kwamba, bila kujali kuwa anachafua jina la Tanzania kimaadili, Ida ambaye hujitambulisha majukwaani kuwa anatoka Tanzania, mwaka 2009 aliibuka tena kinara na safari hiyo hakuwa wa mwezi bali wa mwaka.




Ilielezwa kuwa, Ida ni modo wa kwanza wa Kiafrika kuibuka kinara wa picha hizo kwani inaaminika kuwa siyo rahisi kwa msichana kutoka barani Afrika kuwa na ujasiri wa kukaa utupu.




Habari hizo ziliweka kweupe kwamba, Ida alivumbumbuliwa na kinara wa picha hizo nchini humo mwaka 2007, Sara Jean Underwood huko Beverly Hills, California.




IDA AMEFIKAJE HAPO ALIPO?
Taarifa za Ida zinaonesha kwamba, kutokana na safari za baba yake aliyekuwa akifanya kazi katika Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF), mrembo huyo mwenye uwezo wa kuzungumza Kiswahili, Kiingereza na Kiswidishi alipata ‘chansi’ ya kuzunguka na ‘mdingi’ wake duniani na kuona mambo mengi hivyo akajitumbukiza kwenye umodo.





Ilidadavuliwa kwamba, baada ya kuhitimu digrii ya Urembo na Masoko, sasa anajipanga kusomea Uchumi.

KWA TAARIFA YAKO
Baadhi ya mastaa wa ‘mambele’ wenye mvuto wamekuwa wakilipwa mkwanja mrefu na kupigwa picha za utupu ambazo hutumika kurasa za mbele za majarida mbalimbali ambayo huuzwa kwa bei mbaya duniani kote hasa katika ‘masupamaketi’ yenye tahadhari ya kusomwa na watu wenye miaka 18 na kuendelea. 


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...