Saturday, June 9, 2012

UFISADI MWINGINE WA ATCL ULIOWEKWA HADHARANI NA MWAKYEMBE!






Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe ameibua ufisadi mkubwa uliofanywa na waliokuwa watendaji wakuu wa shirika la ndege Tanzania ATCL chini ya aliyekua kaimu Mkurugenzi Mtendaji Paul Chizi kufuatia kuingia mkataba usio na tija wa ukodishaji wa ndege kubwa aina ya Airbus 320 MSN 630 kutoka nchini Liberia, ndege ambayo ni mbovu.
Amesema “ni mkataba wa kipuuzi kabisa sijawahi kuuona katika historia, ni wa kipuuzi kuliko hata wa Richmond, tumeingizwa mjini peupe kabisa, tumeanza kuilipia Airbus wakati iko kwenye anga yani Tanzania inalipa pesa ya kukodisha hiyo ndege miezi sita iko kule, sisi tunalipa kwa pesa ya wakulima na wafanyakazi wanaolipa kodi… leo tunadaiwa bilioni 69 na jamaa wamefungua kesi, serikali imechoka kuibeba ATCL na mtalikumbuka baadae”
Ndege ya ATCL iliyokodiwa hivi karibuni chini ya uongozi wa Paul Chizi aliyesimamishwa kazi.
Mwakyembe amezungumza na wafanyakazi wa shirika hilo katika ziara aliyoifanya ambapo amesema mabadiliko ya kiuongozi aliyoyafanya na kumteua rubani wa siku nyingi katika shirika hilo Captain Lusajo Lazaro kukaimu nafasi iliyokua inashikiliwa na Chizi yamezingatia uwajibikaji, na kuhusu taarifa za kumlaumu Mwakyembe kwa kuchagua mtu wa kabila lake amesema “wanaosema hivyo ni kutokana na elimu ndogo, ufinyu wa kufikiri kama top management alikuepo huyo  hivi jamani nitafute mtu mwingine kwa sababu ya ukabila? mnafikiria ukabila leo hii watanzania? nimewasimisha wakurugenzi wanne wote ni Wanyakyusa”
.
Kuhusu waliokasirika juu ya maamuzi ya kuwasimamisha kazi wakurugenzi wa ATCL, kwa hasira Mwakyembe amesema “waliokasirika ondokeni ATCL simameni muondoke, nani anawahitaji? aliekasirika aondoke sasa hivi na nitawafukuza kwelikweli, ndege za kukodisha zinatija gani?”
Mwakyembe pia ameshangazwa na ufisadi wa kukithiri kutokana na kitendo cha uongozi uliosimamishwa ATCL kutumia shilingi milioni 79.8 za kitanzania kwenda China kushonesha sare jozi 17 za wafanyakazi huku pia maafisa wawili wakiwa nchini humo kwa siku 48 kusimamia hiyo kazi ya sare.
Sikiliza Mwakyembe mwenyewe akizungumza kwenye ishu mbalimbali hapo chini..



No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...