Saturday, June 9, 2012

MAMA HUYU ATESEKA KWA MIAKA 15



Bi. Beatrice Kantimbo.
“NIMEKUWA nikiteseka kwa kuuguza mguu wangu kwa miaka 15 sasa, hakika napata maumivu makali sana, naomba Mungu anisaidie na awajaze moyo wa huruma Watanzania wenzangu ili niweze kwenda kutibiwa.”
Maneno hayo ya kusikitisha yalisemwa na Beatrice Kantimbo, mkazi wa Kwembe, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam wilayani Kinondoni ambaye amekuwa akiteseka kwa kuuguza mguu wake uliovimba kwa miaka 15 sasa.
Akizungumza wiki iliyopita, Beatrice alisema baada ya kuugua maradhi hayo amekuwa akienda katika hospitali mbalimbali kutibiwa lakini hajapona.
“Ninaumwa sana na baada ya kutembelea hospitali mbalimbali nimeambiwa ni lazima nikatibiwe katika Hospitali ya Apollo, India. Tuliwasiliana na Daktari Shashibhushan Kumar wa huko ambaye baada ya kuona picha tulizomtumia amesema gharama za matibabu yangu ni dola za Kimarekani kati ya 9500 na 12,000 (zaidi ya shilingi mil. 19).
“Bahati mbaya sina fedha hizo na wala familia yangu haina uwezo huo. Nawaomba wasamaria wajitokeze kuokoa maisha yangu…” (alianza kulia, akafuta machozi kisha akaendelea)
“Nimejitahidi nimepata hati ya kusafiria yenye namba AB509215, nikashauriwa nifungue akaunti benki ili watu wanisaidie nimefanya hivyo, namba ya akaunti ni 011201364730 NBC, Naomba mnisaidie…” alisema mama huyo huku akibubujikwa na machozi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...