Thursday, November 10, 2011

WEMA ANASWA NA PICHA ZA UTUPU




PICHA chafu zinazomwonesha Miss Tanzania mwaka 2006, mwenye vituko kila kukicha Wema Isaac Sepetu, ambaye yuko katika uchumba na msanii wa Bongo Fleva Naseeb Abdul ‘Diamond’,  zimenaswa ‘live’ katika moja ya mitandao ya kijamii...

Picha hizo zinamuonesha mrembo huyo akiwa amelala kitandani katika staili mbalimbali huku kuanzia shingoni kwenda chini akiwa hana nguo.

Katika picha moja mlimbwende huyo wa Bongo anayesumbua katika filamu kwa sasa, ameweka kiganja cha mkono wenye kidole chenye pete ya uchumba aliyovishwa wiki kadhaa zilizopita.

ZIMESAMBAA HADI MAREKANI?
Picha hizo zilisambaa kwa haraka Jumapili Novemba 6, mwaka huu kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook, BMM huku wengine wakitumiana kwenye waraka pepe.

Mdau mmoja wa mambo ya kijamii, Jumapili jioni aliliambia Risasi Mchanganyiko kuwa, ana picha hizo na kudai alitumiwa na rafiki yake anayeishi nchini Marekani.

“Kaka nina picha chafu za Wema, kuna jamaa yangu anaishi Marekani amenitumia leo (Jumapili),” alisema mdau huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake.

Ze UTAMU plus ilimjulisha kuwa tayari picha hizo zipo kwenye droo la dawati lake zikifanyiwa uchunguzi wa kina ili kujiridhisha kama kweli ni Wema au zilitengenezwa.

Jumapili hiyo hiyo saa mbili usiku, tulitumiwa picha nyingine kutoka kwa msomaji wake mmoja wa kike ambaye naye alidai ametumiwa na shoga yake anayeishi jijini Dar es Salaam.

WEMA ANANGA ‘WABAYA’ WAKE
Kinachoonekana ni kwamba, baada ya picha hizo kusambaa, Wema alipata habari, akachukua picha moja (angalia picha kubwa ukurasa wa kwanza) na kuiweka kwenye mtandao wa Black Berry Messengers ‘BBM’ katika simu yake kisha akaandika:

“Kuweka waweke wengine, akiweka Wema tatizo, uzuri hii picha hata baby wangu  (Diamond) anaijua.” Hapa alimaanisha kuwa ‘wabaya’ wake wanamfuatafuata kwa kuzianika picha zake mtandaoni.

WEMA APUUZA ONYO
Novemba 2, 2011 saa 5 asubuhi, mdada mmoja (jina tunalo) aliiambia UTAMU kwamba alikutana na Wema maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar es Salaam na kubahatika kuishika simu ya staa huyo na kushtuka baada ya kuona picha chafu za staa huyo.

Alisema, aliona picha chafu za Wema akiwa kitandani peke yake, nyingine yupo na Diamond, akamuonya kuwa siku simu hiyo ikipotea, atakuwa amejianika katika jamii, lakini  Wema hakuonesha kujali, akisema hawezi kupoteza simu yake kwa sababu yuko makini.

Juzi (Jumatatu) UTAMU ilimsaka Wema kwa njia ya simu ili kujua nini kilitokea hadi picha hizo zikasambaa kwa kasi, lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.  

KUTOKA KWA UTAMU BLOG
Baadhi ya mastaa wamekuwa na tabia ya kupiga picha za utupu na kuziweka kwenye simu zao za mikononi, jambo ambalo ni hatari hasa inapotokea simu hiyo ikapotea au kupelekwa kwa fundi.

Ni vyema kuliangalia hilo kwa umakini wa hali juu ili kuifanya jamii iwaamini kwa mienendo yao mizuri. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...