Friday, June 1, 2012

WEMA TENA!!!



Wema akidendeka na Mwinyi Ahmed ‘Mwinyi wa Machozi’.

..Hapa akidendeka na Diamond.

Wema akivishwa pete na Mwinyi.

...Hapa akivishwa pete na Diamond.

Wema akionyesha pete aliyovishwa na Mwinyi.
...Hapa akionyesha pete aliyovishwa na Diamond.

Wema akimtunza Mwinyi.

...Hapa akimtunza Diamond.

WEMA Isaac Sepetu ametoa kali ya mwaka kwa mara nyingine tena baada ya kuandaa usiku wa aina yake na kudendeka laivu na mwanamuziki wa Machozi Band, Mwinyi Ahmed ‘Mwinyi wa Machozi’..
NI NDANI YA MAISHA
Tukio hilo lilijiri usiku wa Mei 29, mwaka huu ndani ya New Maisha Club, Masaki jijini Dar es Salaam wakati Wema akimalizia kipande cha filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la The Super Star itakayoingia sokoni muda siyo mrefu.
KABLA YA TUKIO
Siku hiyo mchana zilienea habari katika kila kona jijini na mitandaoni kuwa Wema alitarajia kuvishwa pete ya uchumba na Mwinyi hivyo aliamua kuifanya ishu maalum hivyo akaiandalia usiku wake kwa kulipia ukumbi na kuchukua Bendi ya Machozi kwa gharama zake ambapo hakukuwa na kiingilio lakini ukweli ni kwamba ilikuwa ni harakati za kukamilisha filamu hiyo.
NDANI YA KLABU
Ndani ya klabu hiyo, Wema alikuwa mwenye furaha ya ajabu na muda mwingi alikuwa ‘beneti’ na baadhi ya marafiki zake katika mtandao wa kijamii wa BBM, ambao walifika kwa ajili ya kumpa sapoti katika zoezi hilo.
MACHOZI WASHUSHA SHOO KLASKI
Wakati Machozi Band wakishusha shoo iliyokuwa ‘klaski’, ghafla Mwinyi alisimamisha muziki na kutangaza kuwa katika maisha ya binadamu, siku zote tunateswa na mapenzi na mateso hayo huisha pale unapopata mtu akakupenda nawe ukampenda.
Kabla sentensi hiyo haijapoa, jamaa huyo akaunganisha kuwa ameshampata ampendaye na hivyo hatarajii tena kuteswa na mapenzi kufuatia tukio aliloahidi kulifanya muda mfupi mbele ya umati uliofurika ukumbini hapo usiku huo.
“Mabibi na mabwana, naomba kuonesha nia yangu kwa mpenzi wangu ambaye naamini nampenda kwa dhati na hatakuja kunisumbua maishani.
“Si mwingine, namleta kwenu Wema Sepetu ambaye leo nitamvisha pete ya uchumba tayari kwa safari ya ndoa yangu hivi karibuni,” alisema Mwinyi na kufuatiwa na shangwe la kufa mtu kutoka kwa waalikwa ambao wengi walikuwa ‘watoto wa mujini’.
Baada ya hapo, ndiyo malkia huyo wa Bongo 2006/07 alipopanda stejini na kukumbatiana na Mwinyi kabla ya kuvishwa pete.
Wakiwa wamekumbatiana, wawili hao walitumia chansi hiyo ‘kudendeka’ hadharani ndipo tukio la Wema kuvishwa pete ya uchumba likafuata.
Baada ya zoezi hilo lililovuta hisia kwa mashabiki wa Wema waliofurika ukumbini humo wakijua tukio hilo ni la kihistoria na kwamba kinachofanywa ni kitu cha kweli, ghafla mnyange huyo akaweka wazi kuwa ni sehemu ya matukio yatakayoonekana kwenye filamu hiyo.
“Najua
nimemaliza zoezi hili wengi wakijua kilichofanyika jukwaani ni kitu halisi, kwa kuwa nilikuwa nimeamua kuwakutanisha marafiki zangu kwa pamoja ili wafurahie nami
“Kutoka moyoni hapo nilikuwa nakamilisha moja ya kipande cha filamu yangu ambayo natarajia kuiachia hivi karibuni hivyo nimefurahi kwamba mambo yameenda kama nilivyokuwa nimetarajia na pia nimeweza kuwaburudisha kwa namna moja au nyingine,” alisema Wema na kuongeza: “Asanteni kwa kuja.”
NI TUKIO LA GHARAMA
Kwa namna tukio hilo lilivyoandaliwa, litakuwa ni la gharama kubwa jambo ambalo Wema mwenyewe alikiri kutokwa na mkwanja mrefu bila kutaja ni kiasi gani.
Mbali na gharama za ukumbi huo na Machozi Band, pia mwanamuziki aliyewahi kuwa mpenzi wa Wema anayeitumikia Mashujaa Band, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ alitumbuiza usiku huo.
Tofauti na maelewano waliyokuwa nayo juu ya uwepo wake mahali hapo, mara baada ya Chaz Baba kupanda jukwaani muda mwingi Wema alikwenda jukwaani na kummwagia mvua ya noti za ‘misimbazi’.
WASHADADIAJI WA MAMBO YA WATU
Mara baada ya tukio hilo ambalo pamoja na kuwa ni sehemu ya filamu, lilifanana na lile halisi la mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’ la kumvisha Wema pete ya uchumba mwaka jana kwenye ukumbi huohuo, washadadiaji wa mambo ya watu walisikika wakinong’ona kuwa lilikuwa ni kijembe kwa Diamond.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...