Tuesday, June 12, 2012

BASI LINGINE LATEKETEA KWA MOTO MORO


Basi la kampuni ya Moro Best likiwa limeteketea vibaya kwa moto.
WIMBI la mabasi ya abiria kuteketea kwa moto linaendelea kushika kasi mkoani hapa ambapo jana basi lingine la kampuni ya Moro Best lenye namba za usajili T846 BCU lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Kilosa kulipuka kwa moto eneo la Kasanga barabara kuu ya Morogoro- Iringa nje kidogo ya Mji wa Morogoro.
Habari za awali zilizopatikana eneo la tukio zilidai kuwa hakuna mtu yoyote aliyepoteza maisha kwenye janga hilo la moto ingawa mizigo mingi ya abiria iliteketea.
Tukio hili linatokea ikiwa ni takribani miezi miwili iliyopita baada ya basi lingine la kampuni ya Muro lililokuwa likitokea jijini Mwanza kuelekea jijini Dar es Salaam kuteketea kwa moto eneo la Maseyu barabara kuu ya Morogoro - Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...