Saturday, June 9, 2012

FOMU YA KUJIUNGA FREEMASON



Fomu ya kujiunga na Freemason.
Kiongozi wa Freemasons Bongo, Sir Ande Chande.
Pete ya Freemasons.
Alama za Freemasons.
Jacqueline Wolper.
Marehemu Steven Kanumba.
HATIMAYE fomu zenye maelekezo ya binadamu aliye tayari kujiunga na imani inayodaiwa ni ya kishetani ya Freemason inapatikana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku ikizua kizaazaaa Bongo hasa kwa vijana wanaoamini ni njia ya kupata utajiri wa ghafla.
Ufukunyuku wa Ijumaa Wikienda umeiibua fomu hiyo yenye maelekezo kwa lugha ya Kiingereza ikimtaka mjazaji kuikabidhi ndani ya mtandao husika baada ya kuijaza.
MWONEKANO WA FOMU
Fomu hiyo nyeupe, juu ina rangi ya njano yenye maandishi ya utukufu kwa Mungu na ukamilifu wa kibinadamu (To the Glory of God and Perfection of Humanity).
Kushoto mwa fomu hiyo kuna picha ya mwanamke aliyesimama akiwa amenyoosha mkono ulioshika kitu chenye ncha kali kwa mwanaume aliyepiga magoti.
Inaonekana mwanaume huyo anaapishwa ili kuingia kwenye imani hiyo na pembeni kuna watu wamesimama wakishuhudia tukio hilo.
KUNA SIFA?
Sifa na masharti ambayo mwombaji anatakiwa kuwa nayo vinashangaza watu kwani baada ya mwombaji kuijaza, kuna mtu atampigia simu kwa ajili ya kujibu maswali ya mjazaji.
Kuhusu hilo kuna maelezo yanayosomeka:
If you are interested joining or just getting some more information, please fill out the form below and some one from order will contact you for your preference to answer any question you may have.
(Kama unapenda kujiunga au kupata maelezo zaidi, tafadhali jaza fomu hii chini na kuna mtu atawasiliana na wewe kwa ajili ya kujibu maswali yako yoyote uliyonayo).
KINACHOTAKIWA KUJAZWA
Hakuna makeke mengi kwenye fomu hiyo kama zilivyo za kugombea ubunge hivyo kufanya watu kumiminika mitandaoni kwa ajili ya kuijaza.
Fomu yenyewe inatakiwa kujazwa jina la kwanza na la pili. Mji anaoishi muombaji, mkoa na nchi.
Baada ya hapo, kuna sehemu inatakiwa kujazwa baruapepe (e-mail) na simu.
Aidha, kuna sehemu ya kuandika maoni kisha mwombaji anabonyeza mahali palipoandikwa submit (wasilisha).
FOMU YAZUA KIZAAZAA BONGO
Tangu kuibuka kwa wimbi la watu kudaiwa kujiunga na imani hiyo nchini, wasomaji wengi wa magazeti wamekuwa wakitaka kuwa wanachama.
Baadhi ya wasomaji hao wamekuwa wakipiga simu kwa namba za wahariri zinazopatikana magazetini wakiuliza wapi wanaweza kujiunga na Freemason.
Mfano mzuri juzi Jumamosi, msomaji mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina, alipiga simu kwa wahiriri watatu wa Global, uhitaji wake ukiwa kuelekezwa sehemu ambayo ataweza kujiunga na imani hiyo yenye utata.
WACHUNGAJI MUWE MACHO
Kutokana na hali hiyo, iko sababu kwa watumishi wa Mungu (wachungaji) kufuatilia kwa makini imani hii na kuwafundisha waumini wao kama inakubalika kwa Mungu au la!
Wapo wanaodai Freemason si imani ya kishetani bali ni mahali ambapo mtu akijiunga anakuwa na maisha mazuri.
Hata hivyo, kuna madai kwamba ni imani ya kishetani ambapo ibada zake huambatana na kafara ya damu za wanyama, hususan mbuzi.
NINI KINAFUATWA FREEMASON?
Dalili zote zinaonesha kuwa wengi wanatamani kujiunga na imani hii si kwa sababu ya kuitafuta njia ya kweli na sahihi ya kufika kwa Mungu, bali tetesi ni kwamba ukiwa mwanachama wa Freemason utajiri njenje kama inavyodaiwa kuwatokea mastaa wa Kibongo, marehemu Steven Kanumba, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Jacqueline Wolper.
Utafiti umebaini kuwa, Wabongo wengi wanatamani kuwa na maisha mazuri, nyumba na magari ya kifahari, hivyo wanaamini ni Freemason tu ndiyo itakayowakomboa.

4 comments:

  1. Ni kweli ata mm nilitamani kuwa lakini nimeshindwa

    ReplyDelete
  2. Nahitaji kujiunga lakini nimetapeliwa Sana na watu Wana jiita wakala wa freemason

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...