Saturday, June 9, 2012

MAKALIO MAPYA YA KICHINA
KUFUATIA taarifa kuwa, dawa za Kichina za kuongeza makalio zina madhara kwa watumiaji, njia mbadala ya kukuza maeneo hayo nyeti imegunduliwa na imeanza kutumika kwa kasi Bongo, Amani linakuhabarisha.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu umebaini kuwa njia hiyo inayotumiwa kwa sasa na wanawake wengi hasa wa mjini si ya kumeza wala kupaka dawa bali ni ya kuvaa taiti zilizojaladiwa vifaa maalum vilivyotuna mithili ya makalio.

Jinsi inavyokuwa
Akizungumza na Amani, mmoja wa wafanyabiashara wa ‘makalio’ hayo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Sanura, alisema ubunifu huo umekuja kufuatia utafiti kuonesha kuwa baadhi ya wanawake wanatamani kuwa na makalio makubwa ila wanaogopa kutumia dawa za Kichina.
“Wanawake wengi wanatamani kuwa na makalio makubwa ili wawadatishe wanaume lakini hawakujaaliwa kuwa nayo, wapo ambao wamefikia hatua ya kutumia zile dawa za Kichina na ilipobainika zina madhara wameacha.
“Watu wakakaa na kuumiza vichwa, ndipo walipogundua njia hii ambayo ni salama kwani anachotakiwa kufanya mwanamke ni kununua taiti hizo ambazo ndani yake kuna kina kitu chenye shepu ya kalio na hips, akivaa na suruali au sketi, huonekana amejaaliwa kumbe hamna kitu,” alisema mama huyo mwenye duka lake la nguo maeneo ya Kariakoo, Dar.


Wateja ni nani?
Imeelezwa kuwa wanaonunua vifaa hivyo ni wanawake wakiwemo pia baadhi ya wanaume ambao huwanunulia wapenzi au wake zao ili kuwafanya wawe na muonekano tofauti.
“Huwezi kuamini si wanawake tu wanaokuja kununua vifaa hivi, wapo pia baadhi ya wanaume ambao huwanunulia wapenzi wao na kati ya hao wamo pia mastaa. Ndiyo maana kuna ambao unawaona leo ana kijungu, kesho hana,” alisema mama huyo.


Lengo la kufanya hivyo ni lipi?
Uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya wanawake hutumia makalio hayo ili kuwadatisha wanaume wanapokatisha mitaani na wengine ili kuwarusha roho wanawake wenzao.
“Kuna wanawake wana tabia za ajabu sana, kwa wengine kuwa na kalio ni sifa kwao na ndiyo maana baadhi yao huvaa wanapokwenda kwenye sherehe au ‘outings’ za kawaida ili tu kuwarusha roho wenzao.


“Lakini wapo pia wanawake wanaoyatumia ‘makalio’ hayo kutafuta soko kwani hawa wanaojiuza wameshajua baadhi ya wanaume ni wabovu sana kwa wanawake wenye makalio,” anasema mama Sanura.


Wadau wanasemaje?
Kila mmoja anaweza kuwa na maoni yake kuhusiana na matumizi ya makalio haya mapya ya Kichina lakini wengi walioongea na Amani wamekuwa wakiponda wale wanaovaa taiti hizo wakidai ni ulimbukeni.

“Huu ni ulimbukeni jamani, kama wewe hukujaaliwa kuwa na kalio orijino, hilo feki litakusaidia nini? Kama unavaa ili kuwadatisha wanaume, je ukiwa naye chumbani atanufaika na nini?
“Ifike wakati tukubaliane na maumbile tuliyojaaliwa na Mungu, kuvaa taiti hizo ni kujichoresha tu kwani leo unaonekana una wowowo kisha kesho utaonekana wa kawaida,” alisema Elizabeth wa Kinondoni, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...