Saturday, March 31, 2012

DIAMOND ARE FOREVER FULL VIMBWANGA


Wanenguaji wa THT, wakiwa wamembeba juu Diamond wakati wa shoo hiyo.


Diamond akionesha uwezo wake katika kucheza.


UKIZUNGUMZIA shoo kali kumi zilizoteka mioyo ya mashabiki hapa nchini na ukaacha  kuizungumzia shoo iliyopigwa usiku wa kuamkia leo  jijini Dar es Salaam, basi utakuwa hufuatilii kwa makini burudani zinazofanyika Bongo.
Shoo ya  “Diamonds Are Forever”,  iliyochukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam usiku wa Machi 30,  mwaka huu ni funga kazi ambayo kwa hakika ni namba moja kati ya nyingi zilizowahi kufanyika  hapa jijini Dar.
Shoo hiyo iliyopigwa na  Nasseb Abdul ‘ Diamond’ au ukipenda unaweza kumwita ‘Platinum’ ilianza majira ya saa nne usiku na kuhudhuriwa na baadhi ya mastaa wa Bongo, akiwemo mpenzi wa zamani wa Diamiond,  Miss Tz mwaka 2006 na mcheza filamu,Wema Isaac Sepetu.
Diamond alidhihirisha kuwa  ana jina  na uwezo wa kujaza mashabiki zaidi ya elfu moja peke yake bila msaada wa  msanii  mwingine.
Pamoja na shoo hiyo kutawaliwa  na  vituko vya hapa na pale kutoka kwa Diamond na Wema bado mashabiki walipata fursa ya kufurahia na wengine kukubaliana na uwezo wa Diamond katika kulitawala jukwaa.
Wasanii kutoka THT Elias Barnabas (kulia) na Amini wakimpa sapoti Diamond.


Diamond akicheza juu ya meza aliyokuwa ameketii Wema na marafiki zake.


Q Chief, akiimba huku amekaa chini katika shoo hiyo muda mfupi baada ya kukaribishwa na Diamond.


… akikumbatiana na mama yake mzazi.


Wema Sepetu akishangalia wakati  Diamondi akicheza.


Jokate naye akicheza kwa furaha.


Diamond akiserebuka na mmoja wa mashabiki zake.


Wema akimtunza Diamond, ambaye alikataa kupokea mkwanja wake


Wema akionesha huzuni baada ya Diamond kukataa kupokea fedha zake na kurejea kwenye meza yao.


Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiingia ukumbini hapo.


Wema Sepetu wakati akiingia Ukumbini.


Diamond, Mama yake Mzazi na Queen Doreen wakiwa katika pozi mara baada ya kuwasili ukumbini.


Diamond na Mama yake wakiwasili.


Ndugu na marafiki wa Diamond, wakihojiwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuwasili  ukumbini.


Mwanamitindo Martin Kadinda akihojiwa mara baada ya kuwasili ukumbini hapo.


Diamodi akiimba huku amempigia magoti Aunt Ezekiel.


Baadhi ya mashabiki waliofurika ukumbini hapo wakiserebuka.

Mastaa wafanya pati ya ufuska






Baadhi ya mastaa waliotimba kwenye pati ya kuzaliwa ‘bethidei’ ya Kimwana Manywele 2006, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunt Lulu’ wanadaiwa kugeuza ukumbi kuwa uwanja wa ufuska kufuatia matukio machafu waliyoyafanya...

Tukio hilo lililoshuhudiwa na paparazi wetu lilichukua nafasi usiku wa kuamkia Alhamisi ya Machi 29, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Sumit Kinondoni Mkwajuni jijini Dar ambapo mtangazaji huyo wa zamani wa C2C alikuwa akitimiza miaka kadhaa (aligoma kuitaja).

Awali, shughuli hiyo ilianza vizuri kwa ‘mtoto aliyezaliwa’ (Aunt Lulu) kuingia ukumbini akiwa amevalia kiheshima ambapo shampeni ilifunguliwa na wageni kula na kunywa huku wakimpongeza staa huyo.

‘SAPRAIZI’
Wakati pati hiyo inakaribia ukingoni, ghafla Miss Mara na Miss Tanzania 2001, Rashida Wanjara aliyeingia ukumbini hapo dakika kadhaa zilizopita alimmwagia Aunt Lulu ‘minoti’ ya elfu kumi kumi iliyokadiriwa kuwa zaidi Sh. laki 3.


MASHOGA WABADILI UPEPO
Wakati watu wakiendelea kutandika ulabu, ghafla vijana watano wanaodaiwa kuwa ni mashoga walianza kushindana kukata nyonga ukumbini humo, hali iliyofanya kila mtu kubaki kuwatazama wao.

MASTAA NAO WAHARIBU!
Mastaa waliofika ukumbini humo wakiongozwa na Isabella Mpanda, Rashida Wanjara, Aunt Lulu na wengine wengi walitia chumvi sherehe hiyo baada ya kucheza kihasara na kuacha maungo nyeti hadharani.

JINSI MOJA WADENDEKA
Pia baadhi ya warembo wanaojiita wadada wa mjini walipigwa chabo wakidendeka laivu wenyewe kwa wenyewe hivyo kusababisha pati hiyo kukumbushia enzi za Sodoma na Gomora kufuatia matukio hayo machafu.
Aunt Lulu ambaye siku hiyo alionekana mpole alidai kuwa, anajisikia vibaya kila siku kuandikwa akiwa na mavazi ya hasarahasara hivyo kuamua kubadilika kwa kutoka kitofauti siku hiyo.

Diamond akikamua live ndani ya mlimani city



Msanii mahiri wa kizazi kipya Diamond akiimba hivi sasa mbele ya umatndai wa watu ndani ya ukumbi wa Mlimani City jijini Dar,kwenye onesho lake maalum iliyoitwa Diamond are Forever Concert

Diamond akiendelea kukamua mbele ya umati wa watu waliofika kulishuhudia onesho lake maalum linaloendelea hivi sasa ndani ya ukumbi wa Mlimani City,jijini dar.Picha zaidi bofya hapa.

Friday, March 30, 2012

Mpasuo wa Maya wachochea ngono ukumbini...





Gauni alilokuwa amevaa msanii wa filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ kwenye sherehe za kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Klabu ya Bongo Movie, liliwapa wakati mgumu baadhi ya wanaume kufuatia mpasuo ulioacha wazi asilimia kubwa ya paja lake.

Tukio hilo lilinaswa na paparazi wetu hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo mara baada ya msanii huyo kutinga ukumbini hapo, minong’ono ilianza kufuatia nguo aliyokuwa amevaa.

Huku akiwa hana aibu, msanii huyo aliketi na kuliacha paja lake wazi, kitendo kilichowafanya baadhi ya wanaume kuanza kumtolea maneno makali wengine wakidai anawashawishi ngono.

“Ndiyo nini sasa kutuvalia vile kama siyo kutuweka majaribuni tu?” alisikika akiwaka kijana mmoja aliyekuwa amekaa nyuma ya msanii huyo.

Hata hivyo, licha ya Maya kubaini kuwa, vazi lake lilikuwa likishawishi ngono aliendelea kupozi kimitego, kitendo kilicholaaniwa na baadhi ya watu waliomuona.

MAMA NA BINTIE WATWANGANA KUGOMBEA BWANA






Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni! Mwanamke mmoja jijini Dar es Salaam aliyetajwa kwa jina moja la Kesi ameibua timbwili zito baada ya kutwangana na bintiye Eliza wakidaiwa kugombea mwanaume...


NI TANDALE
Tukio hilo ambalo ni aibu isiyopimika lilifunga mtaa nyumbani kwa mama huyo maeneo ya Tandale Mbuyuni, Dar hivi karibuni baada ya Eliza kumtuhumu mama yake mkubwa kuwa anatembea na bwanaa’ke.

Wakiwa kwenye pilikapilika za kazi zao, waandishi wetu walipigiwa simu na chanzo ambacho kilidondosha habari juu ya sekeseke ambalo lilikuwa linanukia kutokea maeneo hayo la mama na mtoto kutwangana kisa mwanaume.
HOT POT ilipotimba kwenye eneo la tukio, lilikuta umati ukiwa umejazana huku magari, Bajaj, pikipiki na baiskeli zikiwa hazina pa’ kupita.


PAMBANO LAIVU, WATU WASEREBUKA
Wakati wawili hao wakitwangana laivu, baadhi ya majirani, hasa akina mama walikuwa wakishangilia kwa kupiga ndoo kama ngoma huku wakiserebuka kwa furaha.
Ilibidi kuhoji majirani kulikoni watu kutwangana na wengine kufurahia ambapo walidai kuwa wamechoshwa na visa vya mama na mwanaye kuchukuliana mabwana.


MAMA ACHOROPOKA
Hata hivyo, mama huyo alifanikiwa kuchoropoka mikononi mwa bintiye baada ya kuzidiwa na kipigo ambapo alitoka nduki huku watu wakimkimbiza kwa kushangilia.


BINTI HEWANI LAIVU
Akizungumza na Ijumaa baada ya ‘mbaya’ wake kumchomoka huku akibubujikwa na machozi, binti huyo alisema kuwa siku moja kabla ya sekeseke hilo namba ya simu ya mama yake ilimpigia saa 4:30 usiku.

“Cha kushangaza, nilipopokea sauti ya upande wa pili haikuwa ya mama bali ilikuwa ya mwanaume wangu,” alisema binti huyo kwa uchungu.

Alisema kuwa jamaa huyo alikuwa akiongea kwa kujiamini na nyodo akimuuliza mpigaji ni nani na kwa nini alipiga simu usiku huo kwani wao wamelala, hawataki usumbufu.
“Niliielewa vizuri sauti ya bwanaa’ngu kwani tumeishi pamoja muda mrefu na tuna mtoto wa mwaka mmoja na nusu, nilishangaa sana, nilipomuuliza mama unalala na bwanaa’ngu, bila shaka akashtuka na kunijibu kwa kubabaika, “ alisema.

Alisema kuwa siku ya tukio hilo, wakati akiwa nyumbani hapo akimsubiri mama yake huyo ambaye alilala kwa bwanaa’ke huyo, alipigiwa simu na  mwanaume huyo na kumweleza kuwa hivi sasa yupo na mama hivyo yeye akae pembeni.
Baada ya kutia timu nyumbani, ndipo pakachimbika na kuzuka kwa timbwili hilo.
Hadi tunang’oa nanga eneo la tukio mama huyo alikuwa hajarejea nyumbani baada ya kupokea kichapo ‘hevi’.

HATIMAYE VENGU AINUKA KITANDANI...




MUNGU ni mkubwa! Hatimaye dua za Watanzania zimesikika kwa staa wa Kundi la Orijino Komedi aliyepo Hospitali ya Appolo nchini India kwa matibabu, Joseph Shamba ‘Vengu’ (pichani) ambaye ameinuka na kukaa mwenyewe kitandani...

Kwa mujibu wa chanzo makini ambaye ni mtu wake wa karibu, mbali na hatua hiyo, pia nyota huyo ameanzishiwa mazoezi ya kuongea baada ya kitambo kirefu kutomudu kuzungumza.


Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa, jitihada kubwa zilifanywa na madaktari wa Hospitali ya Appolo ili kuhakikisha kuwa Vengu anarudi katika hali yake ya kawaida.


“Dalili zimeanza kuonekana, hivi sasa Vengu yuko katika hali nzuri, anaweza kuinuka na kukaa kitandani ila bado anapewa mazoezi ya kuongea,” kimesema chanzo hicho.


Habari zaidi zilisema kuwa kinachomfanya Vengu kushindwa kuzungumza vizuri ni kupoteza kumbukumbu kwa muda mrefu na kufanya mdomo wake kuwa mzito.


“Jumatatu (Machi 27, mwaka huu) madaktari walianza kumfanyisha mazoezi ili aweze kuzungumza vizuri, ingawaje haijulikani zoezi hilo litachukua muda gani,” kilisema chanzo hicho na kudai kuwa kama Vengu angeachwa Tanzania, asingefikia katika hatua aliyonayo sasa.


Mbali na kufanyishwa zoezi hilo la kuzungumza, pia Vengu ameanza kufanyishwa mazoezi ya viungo ili kumfanya aweze kutembea mwenyewe.


“Madaktari wameonekana kufurahishwa na hatua hiyo na wanamfanyisha mazoezi ya viungo na kumzoesha kuongea kama unavyojua ana siku nyingi hajazungumza,” kilisema.
Baada ya kupata taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta ndugu wa karibu wa Vengu ambaye anaishi jijini Dar lakini hakuweza kupatikana kuzungumzia hali ya staa huyo.


Hata hivyo, HOT POT ilifanikiwa kumpata mchumba wa Vengu ambaye ni Miss Kinondoni 2011/12, Stella Mbuge na kumuuliza kama ana taarifa zozote kuhusiana na mgonjwa huyo, naye alisema ameambiwa na kaka wa Vengu kuwa sasa jamaa yake yuko katika hatua ya kufanyishwa mazoezi ya kuongea.


“Kaka yake amefurahishwa na hali ya Vengu na amenihakikishia kwamba qnaendelea vizuri, kwa sasa anaweza kuinuka na kukaa mwenyewe ila wanamfanyia mazoezi aweze kuongea tena,” alisema kwa kifupi Stella.


Vengu alianza kuumwa mwaka 2009 ambapo Agosti, mwaka jana alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi akisumbuliwa na ugonjwa unaoshambulia sehemu ya kichwa, hasa ubongo.

Saturday, March 24, 2012

Haijawahi kutokea; asiye na mikono,miguu...



Nicholas Vujicic ‘Nick’ (wa kwanza kulia) wakati wa harusi yake na Kanae Miyahara.
Nick akiwa na mpenzi wake Kanae. 

KIJANA Nicholas Vujicic ‘Nick’, hawezi kuisahau Februari 10, mwaka huu kwani ndiyo siku aliyofunga ndoa na msichana Kanae.
Siku ya ndoa yao, watu maalum walialikwa na baada ya hapo waalikwa walijichana kwa vinywaji na chakula baadaye maharusi hao wakaenda kufunga fungate Hawaii, Marekani.
Wazazi wa Nick, Dushka na mumewe Boris wenyeji wa Australia wanasema siku alipozaliwa mtoto wao huyo miaka 29 iliyopita walikata tamaa kama angeweza kuwa na maisha mazuri.
Hata hivyo, Mungu alimjaalia, akasoma na sasa ana shahada ya kwanza ya Mipango na Uhasibu aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Griffith, Logan, Australia.
Anaweza kuandika kwenye kompyuta na anamudu kusugua meno yake kwa kutumia mdomo.
Jijini Logan, amefungua shirika lake lisilo la kiserikali la watu waishio bila mikono na miguu yeye akiwa afisa mtendaji mkuu (CEO) na ni mhubiri wa Neno la Mungu na amekwisha tembelea nchi zaidi ya 25 duniani. “Nimekuwa nikiwapa matumaini watu wenye ulemavu kwamba wanaweza kuishi maisha mazuri,” anasema Nick.

Tuesday, March 20, 2012

KUU WA KITENGO CHA UKAGUZI APIGA PICHA CHAFU



HUWEZI kuamini lakini ndiyo ukweli kwamba, bosi wa kitengo cha ukaguzi wa mahesabu katika idara moja ya serikali jijini Tanga, Olestar (pichani) ‘amefotolewa’ picha chafu huku akionekana kufurahia...

Licha ya kupiga picha hizo katika mikao tofauti, baadhi ya picha zinamuonesha bosi huyo akiwa mtupu huku mwanaye akiwa pembeni.

Picha zilizotua katika meza ya gazeti hili zinamuonesha bosi huyo akifanya vituko ambavyo si vya kistaarabu ambavyo haviwezi kuanikwa kwa uwazi zaidi ili kulinda maadili.

Katika picha hizo, pia Olestar alionekana akiwa amevaa nguo vizuri kabla ya kuanza kuingia kwenye majaribu ya kufanya zoezi la kuzisaula moja baada ya nyingine.

Tukio la ajabu, ni kwamba katika moja ya picha hizo, bosi huyo ambaye anakiongoza kitengo hicho nyeti, alionekana akiwa mtupu huku ameshika simu akivalia rozari shingoni. 

“ Huu ni upuuzi, mwanamke huyu anaonekana kuwa na heshima zake anayejua dini, hawezi kufanya ujinga kama huu,” alilaani mmoja wa watu waliozushuhudia picha hizo.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari, mwanamke huyo alipiga picha hizo kwa lengo la kuziweka kwenye CD na kuwaonesha wanaume pale wanapokwenda nyumbani kwake kupitia runinga.

“ Picha hizo ameziweka kwenye CD ili kuwahamasisha wanaume wanaokwenda nyumbani kwake,  huwa anawawekea  katika runinga ili wamuone jinsi alivyoumbika na kuwahamasisha kwa ngono,” kilisema chanzo hicho.

HOT POT iliwasiliana na bosi huyo kwa simu yake ya mkononi ili kupata ufafanuzi wake na kutaka kujua kwa nini amefanya kitendo hicho kilicho nje ya  maadili ya Kitanzania.

Alipopatikana, bosi huyo aling’aka kupiga picha hizo, lakini baada ya kubanwa, alikiri na kuahidi kumtuma dada yake katika ofisi za blog hii kwa lengo la kuzitambua.

“Mimi najiheshimu sana, siyo malaya kama unavyonifikiria, lakini hata hivyo, inawezekana nitamtuma dada yangu aje hapo ofisini kwenu ili azikague,” alisema.

Hata hivyo, pamoja na kuongeza jitihada za kuwasiliana na bosi huyo, hakuna mtu alionekana katika ofisi hili kwa ajili ya kuzitambua picha hizo.

Hatua za  mwisho alizochukua bosi huyo ni kuweka mgomo wa kupokea simu za blog hii...

MASHINE YA KUINUA MATITI YATUA DAR


Mashauzi.
Nisha.

WACHINA wamezua kizaazaa kingine Bongo baada ya kuingiza mashine ya kusimamisha matiti yaliyolala...

Saa kadhaa baada ya ishu hiyo kuripotiwa na moja litokalo kila siku nchini, mapaparazi wetu walifika katika saluni inayotoa huduma hiyo iitwayo Blue Palace, iliyopo Mapambano, Sinza jijini Dar es Salaam na kushuhudia wanawake waliotimba mahali hapo wakitaka kuhudumiwa.

MTAALAMU WA KICHINA
Ilifahamika kuwa saluni hiyo inayomilikiwa na Sarafina Mtweve na meneja wake, Trust Mwembe ina mtaalamu wa Kichina aliyetajwa kwa jina la Ciisy Pang (23), ambaye ndiye anayetoa huduma hiyo.
Pamoja na gharama ya huduma hiyo kuwa kubwa kuanzia Sh.150,000 kwa kichwa, lakini bado idadi kubwa ya wanawake ilishuhudiwa ikifika mahali hapo kuulizia huduma bila kujali kiwango cha fedha.
Hata hivyo, gazeti hili lilipotaka kushuhudia kifaa kinachofanya kazi hiyo kiitwacho Beauty machine (mashine ya urembo), ilishindikana kwa maelezo kuwa hawafanyi kazi siku ya Jumatatu pamoja na kwamba wateja walikuwa wa kumwaga.

ETI INAREJESHA HESHIMA KWENYE NDOA!
“Fedha ni nini mbele ya kurejesha heshima ndani ya ndoa? Hakuna kitu kinachonigombanisha na mista wangu kama kulegea matiti yangu baada ya kunyonyesha mtoto wetu wa kwanza. 

“Nahisi amepunguza upendo kwa ajili hiyo, lakini sasa nimepata mkombozi,” alisema mama mmoja aliyekutwa nje ya saluni hiyo Jumatatu wiki hii akiwa na wenzake.

“Asikudanganye mtu, matiti magumu yana mvuto wake, wanaume wengi hawapendi yaliyolegea kama uji, kwa taarifa yenu sasa mtatukoma, tutakuwa vigori,” alisema mwanamke mwingine aliyekuwa anasubiri huduma.

Ingawa alielezwa kwamba afike siku ya pili yake,  lakini aligoma na kuendelea kung’ang’ania eneo hilo akihitaji huduma hiyo.

MASHINE INAFANYAJE KAZI?
Ilifahamika kuwa, mashine hiyo ina uwezo wa kusimamisha matiti ya kila saizi kwa kuwa huambatanishwa na vibakuli maalumu kulingana na ukubwa anaohitaji mteja.

Kazi kubwa ya mashine hiyo ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti ambayo huchukua wiki tatu mpaka sita kutegemeana na aina ya mteja na juhudi zake.

“Kwanza unapaswa ujue kuwa hatutumii dawa yoyote katika zoezi hili, mteja akifika, kinachotumika ni mashine tu ambayo hutumia umeme kama zilivyo dryer  za nywele.

“Baada ya kumlaza mteja kitandani, tunachukua kitu mfano wa bakuli mbili kulingana na ukubwa wa matiti yake, tunayatumbukiza humo, kisha tunawasha mashine,” alikaririwa mtaalamu huyo wa Kichina na kuongeza:

“Tunaiwasha mashine kwa dakika 45, mteja atachagua siku mbili katika wiki za kufanya zoezi hili mpaka litakapokamilika.”

MASTAA WAENDA KWA SIRI
Wakati huo huo, habari za kuaminika zinadai kuwa baada ya kunyaka mchongo huo zaidi ya mwezi mmoja kabla ya kuripotiwa, baadhi ya mastaa wamekuwa wakiibuka saluni hapo kwa siri ili kupata huduma.

HOT POT ililizungumza na baadhi ya mastaa kama wana taarifa zozote kuhusu huduma hiyo ambapo kila mmoja alikuwa na lake la kusema:

JACQUELINE PENTZEL
 ‘JACK CHUZ’
“Kama itakuwa ni tiba asili ni bomba lakini kama material (vifaa) yanayotumika ni feki, lazima kutakuwa na madhara. Siwezi kuthubutu kukitumia hivi hivi.”

MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’ (pichani)
“Mh! Tukiangalie kwa makini hicho kifaa jamani, tusije tukamkufuru Mungu bure kwa vitu ambavyo havina maana. Hapo lazima kutakuwa na madhara hata kama si ya moja kwa moja lakini kwa baadaye kuna madhara makubwa.”

SALMA JABU ‘NISHA’
“Naogopa kansa, lakini ngoja nikakifanyie uchunguzi kwanza nione kama hakina madhara, labda ninaweza kwenda ila kwa sasa, aku! Naogopa kupata maradhi ya kujitakia.”

BABY MADAHA
“Aaah! Sana tu, mambo ya urembo na mimi tena! Hata usiulize lazima niende tu, mambo mengine baadaye lakini urembo kwanza.”

KUNA MADHARA?
Kila kitu kina faida na na madhara yake ambapo kwa mujibu wa Dk. Innocent Mosha wa Kitengo cha Patholojia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ni vigumu kwa wataalamu wa afya kugundua madhara ya mashine hizo kwa haraka hadi pale uchunguzi utakapofanyika.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...