Saturday, June 9, 2012

INATISHA...



IPO taarifa ya kutisha kuwa Desemba 21, 2012 (siku nne kabla ya Krismasi) ndiyo mwisho wa dunia lakini yameibuka madai kwamba mpango huo ni njama za Jamii ya Siri inayomuabudu Shetani (Lucifer), Freemasons.
Habari zinasema kuwa Freemasons wamepanga kuiangamiza dunia Desemba 21 kutokana na malengo mawili, mosi likiwa kuwafanya watu wasisherehekee Krismasi ya mwaka huu, pili ni kuhakikisha Yesu atakaporudi asikute mtu.
Mtandao mmoja wa Marekani unaopingana na falsafa za Freemasons pamoja na jamii nyingine za siri kama Illuminati na Skull & Bones, umeandika kwamba ubashiri unaoeleza kuwa Desemba 21 mwaka huu ni mwisho wa dunia, ni kusudio la Shetani.
Umebainisha kuwa Freemasons kupitia Lucifer wanayemuabudu, wanasuka mpango mzito wa kuiangamiza dunia ili kutimiza kile wanachokiita kumshinda Yesu pamoja na ahadi yake kwa wanadamu wote duniani.
Inazidi kubainishwa kwamba kwa vile maandiko yanasema Yesu alisema atarudi, basi Freemasons wanataka dunia iteketee kabla ya ujio wake ili kutimiza azma ya Lucifer kuwapoteza wanadamu kutoka kwenye mamlaka za Mungu.
Mwandishi wa mtandao huo ambaye amejitambulisha kwamba ni mchungaji wa kanisa, alisema kuwa dunia isihadaike na propaganda kwamba utabiri wa Desemba 21 ni wa kisayansi, bali waukemee na kumuomba Mungu azuie hilo kutokea kwani ni mpango wa Shetani.
UTABIRI ULIVYOANZA
Profesa wa Chuo Kikuu cha British Columbia, alikuwa wa kwanza kubainisha kwamba asteroidi (sayari ndogo zinazoizunguka dunia), mojawapo itaanguka duniani kwenye Bara la Antaktika, hivyo kuipa mtikisiko mkubwa dunia.
Japo profesa huyo hakueleza kama huo ndiyo utakuwa mwisho wa dunia lakini alibainisha kwamba ni ngumu kupata picha halisi kwa sababu asteroidi itakayoiangukia dunia ni kubwa kwani ina ukubwa wa mita za mraba 800.
Taarifa ya profesa huyo, ilichapishwa kwa siku mbili kwenye tovuti ya has.ubc.ca kisha kuondolewa kabla ya wanasayansi wa McMurdo Station nchini Marekani, wanaoelekeza tafiti zao Bara la Antaktika kutengeneza kiumbo mithili ya baluni lenye ncha kuonesha litakavyotua juu ya dunia na kuiangamiza.
Wanasayansi wa Canada-France-Hawaii Telescope wanaofanya tafiti zao kwenye volkano ya Mauna Kea, Hawaii, Marekani nao waliiboresha ncha ya asteroidi na kuionesha ikiwa kali zaidi kwamba itakapotua duniani, itachimba sayari ya dunia kabla ya kuiangamiza.
Mwanasayansi aliyebobea kwenye elimu ya anga, Chris Hadfield, raia wa Canada ambaye ni Rais wa Taasisi ya Association of Space Explorers, alibainisha kuwa asteroidi itakayoiangukia dunia, itapoteza uelekeo wake kilomita 700 juu ya dunia, hivyo kuiangukia.
WANASAYANSI WENGINE WAPINGA
Taasisi ya utafiti wa kisayansi ya nchini Marekani, Nasa, imeeleza kwamba katika uchunguzi wake, haijabaini hicho kinachobainishwa kuwa ni kuangamia kwa dunia Desemba 21, mwaka huu.
Nasa wameeleza kuwa hizo ni propaganda, kwani sayari ya dunia ipo kwenye mhimili wake, kwa hiyo hakuna tishio la kuangamia.
NI TISHIO LA PILI
Mei 21, mwaka jana, mchungaji aliye pia Kiongozi wa Kanisa la Christian Apologetics & Research Ministry la Chanhassen, Minnesota, Marekani, alitabiri kwamba ndiyo ingekuwa mwisho wa dunia na miezi mitano baadaye, yaani Oktoba 21, kingefuata kiama.
Hata hivyo, hilo halikufanikiwa lakini wanasayansi na baadhi ya viongozi wa kidini wanaoamini Desemba 21, mwaka huu, husherehesha hoja zao kwa kumbukumbu za kalenda za biblia za kale ambazo wanadai zinathibitisha kwamba Desemba mwaka huu dunia itaangamia.

1 comment:

  1. UONGO MTUPU. JIFUNZE KUFANYA RESEARCH YENYE VITHIBITISHO...ACHA UDANGANYIFU KWA WATU WENYE KIWANGO CHA ELIMU YA CHINI.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...