Sunday, June 17, 2012

HAWA NDIO WALIOPIGWA CHUPA KWENYE UGOMVI WA CHRIS BROWN NA DRAKE.



Anaitwa Hollie ni raia wa Australia ambae muda mfupi baada ya kuingia club ndio akakutana na vita vya chupa ambapo moja ilimpiga usoni.
Ikiwa leo ni jumamosi, Kwenye blog ya Necole stori ya Drake na Chris Brown kupigana club tena kwa kurushiana chupa imeshika nafasi ya kwanza katika stori popular wiki hii, imesomwa sana na imeongelewa pia.
Chanzo cha ugomvi huo kwenye club ya usiku ya W.I.P huko New York inadaiwa ni Chris Brown kumuagiza muhudumu ampelekee Drake pombe, wote walikua kwenye club moja na inajulikana wana beef ambayo imetokana na kumgombania Rihanna na ni beef ambayo ilionekana twitter kama wiki mbili zilizopita.
Sasa baada ya Drake kupelekewe ile oda akakasirika sana na kumfata Chris Brown alipokua na kuanza kumuwakia, wakapandishiana na wakaanza kugombana kuhusu Rihanna, Drake akampiga usoni CB na kumchana na chupa pia.
Huyu ni Pat mlinzi wa Chris Brown ambae nae alipigwa chupa na kupelekwa hospitali.
Chris Brown akiwa nje ya club baada ya ugomvi kutokea.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...