Saturday, June 9, 2012

MUUMINI AMPACHIKA MIMBA BINTI WA MWINGIRA



IMEDAIWA kuwa binti wa Kiongozi wa Kanisa la Efatha, Josephat Mwingira (pichani) aliyetajwa kwa jina la Love amepachikwa mimba na muumini mwenzake ambaye walikuwa wakisali katika kanisa hilo...
Habari zilizonaswa zinasema kuwa binti huyo ambaye alikuwa ni kipenzi cha baba yake, alikuwa na uhusiano usiofaa na mvulana mmoja ambaye alikuwa muumini kanisani hapo.
Hata hivyo, habari za kupachikwa mimba msichana huyo ziliwashangaza waumini wengi kutokana na tabia ya baba yake, Mchungaji Mwingira kumsifu mara kwa mara mbele za waumini kuwa ni msichana mwenye hekima, adabu na ni msomi mzuri.
“Baada ya msichana huyo kujazwa mimba, amefukuzwa nyumbani kwa Mwingira na sasa amekimbilia kwa baba yake mkubwa, Temeke jijini Dar es Salaam,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kupata taarifa hizo katika Kanisa la Efatha, makao makuu kwa lengo la kupata ufafanuzi wa baba yake lakini kiongozi mmoja kanisani hapo alikataa kumruhusu mwandishi kuonana na Mwingira akidai kuwa suala hilo ni la binafsi, hivyo aondoke.
“Kama ni kuhusu mambo hayo ya mimba ya mtoto wa kiongozi, ondoka, hayo ni mambo binafsi,” alisema mtu huyo aliyedai kuwa ni kiongozi kanisani hapo.
Mwandishi wetu alikwenda hadi Temeke, nyumbani kwa kaka yake Mwingira ambako inadaiwa kuwa ndiko aliko Love lakini hakufanikiwa kumkuta binti huyo na badala yake alijibiwa na mfanyakazi wa ndani kuwa msichana huyo kwa wakati huo hakuwepo.
Habari tulizozipata wakati tunakwenda mitamboni zinasema Love tayari ameshajifungua.
Jitihada za kumtafuta Love au Josephat Mwingira kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo zimegonga mwamba.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...