Saturday, December 31, 2011

http://zeutamuplus.blogspot.com/ WISHES YOU A HAPPY NEW YEAR 2012


MAHABA: Kabla ya ndoa jiulize, kwa nini umempenda?


IMEBAKI siku moja kabla ya kumaliza mwaka huu na kuanza mwingine kwa ridhaa yake aliyeumba Mbingu na Dunia. Rafiki, huu ni wakati wako wa kufanya tathmini ya jumla ya mwaka huu katika maisha yako ya kimapenzi.

Wakati tunaelekea ukingoni mwa mwaka huu, ni vyema kama utajiuliza; umefanya nini kwa ajili ya penzi lako? Mpenzi wako anakufurahia au anakuona kero?
Ndoa yako inaendeleaje? Je, umekuwa mbabe na kumnyanyasa mwenzako? Una nyumba ndogo au unamheshimu mwenzi wako? Maswali haya yatakuongoza na kukuweka kwenye mstari mzuri wakati unaingia mwaka mpya.

Rafiki yangu, ni vizuri kama utamaliza mwaka ukiwa na tabasamu la nguvu na mwenzako, haina maana yoyote kununiana. Kama mmependana kweli, basi mkubali kwamba kuna kukosana na kuombana msamaha. 

Hakuna mkamilifu wa kila kitu ndugu zangu. Watu wanakosea sana, kukosea ni sehemu ya ukamilifu wa binadamu. Tafuta amani ya kudumu kwa mwenzi wako. Acha kusikiliza maneno ya watu. Wewe ndiye umemchagua, hivyo mwenye kibarua cha kumuweka sawa, anaendelea kuwa wewe mwenyewe!

Umeelewa rafiki? Hizo ndizo salamu zangu za Krismasi na Mwaka Mpya. Sasa narudi katika mada yetu ya leo, mada ambayo itabadilisha kabisa fikra zako katika sayari ya mapenzi.
Yapo mambo muhimu sana ambayo watu wamekuwa wakiyapuuza kabla ya kufanya uamuzi wa kuingia kwenye ndoa. Rafiki, ukishaingia ndani ya ndoa, hakuna njia ya kutoka tena, hata ikiwepo si sahihi. Inakuchafua. Inaharibu historia ya maisha yako ya uhusiano.

Uamuzi wa ndoa si wa kujaribu. Unatakiwa kujihakikishia kwamba ni kweli umevutiwa na kila kitu cha mwenzako, kwamba utakuwa naye katika shida na raha. Hayo ndiyo mambo ya kuzingatia.
Nimeshaandika mengi kuhusu sifa za anayetakiwa kuoa au kuolewa, lakini nasogea mbele zaidi na kuangalia sababu za kumpenda mtarajiwa wako katika ndoa. 

Zipo sababu za msingi sana ambazo unatakiwa kuwa nazo kabla ya kuingia kwenye ndoa ambayo mimi hapa kwenye All About Love naiita kifungo!
Twende tukaone.

KWA NINI UJIULIZE
Lazima nifafanue hili kwanza kabla ya kuendelea. Hivi unafikiri ni kwa nini ni lazima kujiuliza sababu za kumpenda mwenzi wako?
Yes! Ni kwa lengo la kujiwekea usalama katika ndoa yako ijayo. Kujiandalia amani na pumziko la kweli. Kwenye mapenzi ya dhati pekee ndipo vinapopatikana vitu nilivyotaja hapo juu.

Kwa maneno mengine kuwa na majibu ya swali linalosomeka kwenye kichwa cha mada hii ni kujihakikishia ndoa bora. Tuendelee kujifunza. 

NI MWENZI WA NDOTO ZAKO?
Jambo kubwa kuliko yote ambalo unatakiwa kuliangalia kwa jicho la tatu ni kama mwenzi huyo ni wa ndoto zako. Je, yukoje? Rafiki, siku zote kabla ya kuamua kufanya chochote lazima ujiulize kama ndicho ulichokuwa ukikifikiria.
Hata kwa upande wa mwenzi wako, lazima ujiridhishe, ni kweli ni yule uliyekuwa unamtarajia? Ana sifa unazohitaji? Acha tabia ya kujifariji kwamba utampenda taratibu ndani ya ndoa, hicho kitu hakipo.

Hakuna kujifunza kupenda katika ndoa, lazima ujihakikishie mwenyewe kuwa mwenzi wako ni yule mwenye sifa ulizokuwa ukizitarajia. Hili ni la msingi, maana unaweza kuwa naye siku mbili, ukatamani mwingine nje, kwa  nini? Kwa sababu si yule mwenye sifa ulizotarajia.
 
NI SURA, UMBILE?
Kuna baadhi ya watu utawasikia wakisema: “Mpenzi wangu ananivutia sana, yaani ni mzuri sana. Najua hata nikitoka naye, marafiki zangu watanisifia kwa kuchagua vizuri...”
Hizi ni fikra potofu ndugu zangu. Mapenzi ya kweli hayapo kwenye sura wala umbile la mtu. Vipo vigezo vya muhimu kabisa vya kuzingatia tofauti na uzuri wa sura.

Sura hubadilika ndugu zangu, binadamu wanazeeka, kuna kuugua na matatizo mengine ambayo yanaweza kubadilisha mwonekano ambao ulikuvutia. Je, yakitokea ndiyo utakuwa mwisho wa kumpenda?
Kama leo hii unamuoa kwa sababu umevutiwa na matiti yake madogo, akishazaa na kunyonyesha kisha yakaanguka, ndiyo mwisho wa kumpenda? Umempendea ngozi yake nyororo, akipata ‘aleji’ ya mafuta, ngozi ikaharibika na kuwa na mabakamabaka utakuwa mwisho wenu?

Wewe mwenye mpango wa kuolewa na mwanaume mwenye kigezo cha kifua cha kimapenzi, kesho akifutuka na kuwa na kitambi utamuacha? Rafiki yangu, kiukweli ni kwamba kigezo cha uzuri wa sura na umbile si sahihi kabisa katika kuchagua mwenzi. Vipo vitu vingine muhimu zaidi vya kuangalia.

Kama ulikuwa unaishi katika dunia ya fikra hizo, hama ndugu yangu. Wiki ijayo nitakupa sifa bora zaidi za kuzingatia kabla ya kuamua kufunga ndoa na mwenzi wako. Bila shaka utaanza mwaka vizuri, maana hata fikra zako zitakuwa mpya kabisa.
Je, unatarajia kuoa hivi karibuni? Wiki ijayo nitakufungua kuhusu sifa anazotakiwa kuwa nazo huyo mwenzi wako. Si ya kukosa rafiki.
HERI YA MWAKA MPYA!

BREAKING NYUZZZZZ........



Mpiganaji John Ngahyoma afariki dunia
HABARI ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE INAELEZA KUWA,ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA ITV/RADIO ONE MIAKA YA NYUMA NA BAADAE KUHAMIA KWENYE SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA UINGEREZA (BBC),BW. JOHN NGAYOMA AMEFARIKI DUNIA MAPEMA LEO ASUBUHI.
HAYATI NGAHYOMA AMBAYE AMEFIKWA NA MAUTI LEO AKIWA HOSPITALI AMBAKO ALIKUWA AKIPATIWA MATIBABU YA MARADHI YALIYOKUWA YAKIMSUMBUA KWA MUDA MREFU AMBAPO ALIENDA MPAKA NCHINI INDIA KWA MATIBABU YA MARADHI YAKE HAYO BILA MAFANIKIO.
MSIBA UPO NYUMBANI KWA MAREHEMU MAENEO YA TABATA SEGEREA NA TARATIBU ZOTE BADO ZINAENDELEA KUFANYIKA.
HIVYO TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI TUTAKAVYOKUWA TUNAZIPATA.
GLOBU YA JAMII IMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA SANA TAARIFA HIZI ZA MSIBA WA MPIGANAJI WA SIKU NYINGI KATIKA TASNIA HII YA HABARI,BW. JOHN NGAHYOMA NA INATOA POLE KWA NDUGU WOTE WA MAREHEMU NA TUKO PAMOJA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MAJONJI.
TUNAMUOMBEA KWA MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI.

Comedy ZONE


SOFTWARE ENGINEER AND HIS WIFE CHATING...

Wife: "Hey dear, I am logged in..."
Husband: "Loading..."

Wife: "Would you like to have some snacks hny?!"
Husband: "Hard disk full..."

Wife: "Have you brought the I phone 4 u promised?!"
Husband: "Bad command or file name..."

Wife: "But I told you about it in morning..."
Husband: "Erroneous syntax, abort, retry, cancel..."

Wife: "Owky... Forget it...!!! N where's your salary??!"
Husband: "File in use, read only, try after some time..."

Wife: "At least give me your credit card, I can do some shopping..."
Husband: "Sharing violation, access denied..."

Wife: "I made a mistake in marrying you..."
Husband: "Data type correct.."

Wife: "You are useless..."
Husband: "By default..."

Wife: "And who was there with you in the car this morning?!"
Husband: "System unstable press ctrl, alt, del to Reboot..."

Wife: "What is the relation between you & your Receptionist?!"
Husband: "Invalid user... Thats the only user with write permission..."

Wife: "What is my value in your life?!"
Husband: "Unknown virus detected..."

Wife: "Do you love me or your computer?!"
Husband: "System error... Too many parameters.."

Wife: "I will go to my dad's house..."
Husband: "Program performed good operation, it will Close..."

Wife: "I will leave you forever."
Husband: "Entry accepted... Close all programs and log out for another User..."

Wife: "It's worthless talking to you..."
Husband: "Shut down the computer..."

Wife: "I am going.."
Husband: "Command accepted... Its now safe to turn off your computer!!!"

Wednesday, December 28, 2011

2011 MWAKA WA TABU



Gharama za maisha kwa wananchi wa kawaida zimekuwa kubwa sana katika  kipindi chote cha Sikukuu ya Krismasi hadi kuelekea Mwaka Mpya, hii inatokana na bei za bidhaa mbalimbali kupanda maradufu, hali iliyowafanya baadhi ya wananchi kusema kuwa 2011 ni mwaka wa tabu.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa hali hiyo imetokana na mfumuko wa bei ambao umezidi kuongezeka kama taarifa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu inavyoonesha.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mfumuko wa bei kwa Julai mwaka huu (Bajeti ya mwaka wa Fedha 2011/2012 ilipokuwa inaanza) ulikuwa ni asilimia 13, hadi kufikia Novemba umefikia asilimia 19.2.
Tayari bei za vyakula katika masoko ya Mwenge, Kariakoo, Buguruni, Mahakama ya Ndizi, Tandika, Afrikasana, Mbagala, Tandale jijini Dar es Salaam zimekuwa juu kupita kiasi na kuwafanya wananchi kulalamikia hali hiyo.
Katika masoko hayo, bei za vyakula zimepanda sana, kwa mfano kwa kilo mchele (za zamani zikiwa kwenye mabano) unauzwa Sh. 2,000 (Sh.1500), Unga wa sembe unauzwa Sh.1,000 (Sh. 800), Nyama ya ng’ombe Sh. 7,000 (Sh.5,000), dagaa wa Kigoma sh. 19,000 hadi Sh. 20,000 (14,000) na mboga ya jamii ya kunde Sh. 1,900 (Sh. 1,300).
Aidha, kuku wa kienyeji waliokuwa wakiuzwa kati ya Sh.8,000 na 10,000, sasa wanauzwa kati ya Sh. 15,000 hadi 19,000.



Uchunguzi wetu umebaini kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa kama mchele, sukari, nyama na samaki umekua maradufu ambapo bei ya mchele imekua kwa asilimia 50, sukari asilimia 50, nyama asilimia 30 na samaki kwa takribani asilimia 40.
 Bidhaa hizi zote ni muhimu sana kwa afya ya binadamu hasa (watoto) ambao  wanasisitizwa kula vyakula vyenye protini.
Akizungumzia mfumuko huo wa bei, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameandika katika mtandao wake kuwa, hii maana yake ni kwamba, bajeti ya serikali iliyopitishwa na bunge Juni 2011, imepunguza uwezo wa kununua bidhaa na huduma kwa takribani asilimia 6, sawa na shilingi 780 bilioni zimeyeyuka katika kipindi cha miezi minne tu ya utekelezaji wake.
“Kutokana na kasi ya ukuaji wa mfumuko wa bei ni dhahiri kwamba, itakapofika mwishoni mwa mwaka wa bajeti, serikali itakuwa imepoteza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kununua bidhaa na kutoa huduma kwa zaidi ya robo ya bajeti yake,” amesema Zitto.
Aidha, Ofisi ya Takwimu imeonesha kuwa wakati mfumuko wa bei za vyakula ulikuwa asilimia 14.8 Julai, mwaka huu, umefikia asilimia 24.7 hadi kufikia Novemba 2011.
Ukilinganisha na bei za vyakula mwaka 2010, mwananchi amepoteza uwezo wa kununua chakula kwa zaidi ya robo kati ya Novemba 2010 na Novemba 2011.
Jumla ya vyakula ambavyo mwananchi alinunua kwa shilingi 10,000 mwaka 2010, sasa atanunua kiwango kilekile kwa shilingi 12,500. Bei za vyakula zimeongezeka kwa kiwango hiki ilhali kipato cha mwananchi  kikiwa kimebaki pale pale, hivyo mwathirika mkubwa ni mwananchi wa kawaida hasa wa kijijini ambaye mapato yake ni madogo.




Uchunguzi zaidi umebaini kuwa, kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula, mfumuko wa bei wa mafuta ya taa na gesi asilia unapaa kwa kasi, kwani mafuta ya taa yamepanda kwa asilimia 71 kati ya Novemba mwaka 2010 na  Novemba 2011, bei ya gesi asilia imepanda kwa asilimia 35.
Wataalamu wa mazingira wanasema madhara ya hali hii ni makubwa mno kwa maana wananchi watakimbilia kwenye matumizi ya mkaa na kuni, hata hivyo, bei za mkaa zenyewe zimepanda kwa asilimia 24.
Wachunguzi wa mambo ya uchumi wanasema mfumuko wa bei unawasukuma Watanzania wengi hasa walalahoi  kwenye dimbwi la umasikini uliotopea, unapunguza uwezo wa serikali kutoa huduma za jamii kupitia bajeti yake na hata kutimiza mipango ya miradi ya maendeleo kama vile miundombinu ya barabara, umeme, bomba la gesi, madaraja n.k.
Baadhi ya wachumi, akiwemo Dk. Ngali Maita waliliambia gazeti hili juzi (Jumapili) kuwa ili kuondoa tatizo sugu la sukari nchini, serikali iruhusu na kutoa vivutio kwa wazalishaji binafsi wa bidhaa hiyo.
Kuhusu vyakula watu binafsi wahamasishwe katika kuzalisha mpunga katika mabonde makubwa na kuhimiza uzalishaji mashambani na fedha zielekezwe kujenga miundombinu ya barabara vijijini.
Dk. Ngali alishauri vyakula vilivyolundikana katika mikoa ya Rukwa, Mbeya na Iringa vinunuliwe mara moja na serikali na kusambazwa katika mikoa yenye upungufu wa vyakula na iongeze kasi ya  kununua bidhaa hasa sukari kutoka nje na isimamie bei ili  kupunguza upungufu wa bidhaa (scarcity) katika masoko.
Dk. Ngali aliishauri serikali kutengeneza kiwanda cha gesi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani haraka ili kupunguza bei ya gesi, kuepuka kuagiza gesi kutoka nje na hivyo kuokoa fedha za kigeni na kutengeneza ajira hapa nchini.
Alisema mfumuko wa bei katika bidhaa ya mafuta ya taa unatokana na uamuzi wa kulinganisha bei ya bidhaa hiyo na diseli ili kuondoa tatizo la uchakachuaji wa mafuta, hali ambayo inawaumiza walalahoi.
Alishauri sera ya matumizi ya serikali iangaliwe upya kwa kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi yasiyo ya lazima kama vile posho nono na badala yake fedha nyingi zielekezwe katika uwekezaji wa shughuli za umma.
“Matumizi mengine ya serikali yanaongeza fedha kwenye mzunguko ama kwa kuwalipa watu wachache posho mbalimbali n.k au kwa kununua bidhaa na huduma bila mpango, hivyo kusukuma bei kuwa juu kinyume na uhalisia wa soko na kuwafanya walalahoi kuumia,” alisema Dk. Ngali ambaye pia ni mwanasheria.
Alionya kuwa tusipochukua hatua za haraka tutazidisha mfumuko wa bei na kufikia kiwango cha juu kabisa ambacho kilifikiwa mwaka 1994 (33%) na hivyo viwanda kushindwa kukopa kwenye mabenki, wazalishaji wadogo watashindwa kulipa mikopo yao kwenye taasisi za fedha na hivyo kufunga uzalishaji.
Kutokana na takwimu hizo, wananchi wengi wamesheherekea Sikukuu ya Krismasi kwa unyonge huku wenye nazo wakila raha.

RIPOTI KUU YA MAFURIKO DAR



JANGA la mafuriko lililolikumba Jiji la Dar es Salaam baada ya mvua kubwa iliyoambatana na radi kunyesha Desemba 20 na 21, mwaka huu, ndiyo habari ambayo inaitikisa nchi, hii ni ripoti kamili ambayo huwezi kuipata popote zaidi...
Baadhi ya wakazi wana hali mbaya, wengine wamepotelewa na ndugu zao hivyo kuifanya Krismasi yao kuwa mbaya kutokana na majonzi mazito waliyonayo.
Timu ya Uwazi iliingia mitaani kwa siku tano mfululizo tangu siku ya tukio na kukusanya mambo mengi ambayo yanatia simanzi.
Zipo familia ambazo kwa sasa hazina makazi, maisha yao ni magumu, kila kitu wameanza upya baada ya madhara hayo ya mafuriko.

HARUFU BONDE LA MSIMBAZI
Taarifa ya serikali iliyotolewa wiki iliyopita inaeleza kwamba, idadi ya watu waliofariki imefikia 38, huku wawili kati yao wakiwa hawajatambuliwa, lakini Uwazi limeelezwa kwamba waliokufa ni wengi zaidi.
Kwa mujibu wa wakazi wa maeneo ya Jangwani na Kigogo, wamesema kwamba kuna hofu ya kuwa wamekufa watu wengi zaidi ya idadi iliyotajwa na serikali hasa kutokana na harufu kali iliyopo katika Bonde la Msimbazi.
“Harufu ni kali, bila shaka kuna watu wengine ambao wamo chini, serikali inapaswa kutumia vifaa vya kisasa kwa ajili ya kukagua eneo hili ili kujua kama kuna maiti nyingine,” Ali Rashid, mkazi wa Kigogo, Dar aliwaambia waandishi wetu.
Joseph Lucas aliyejitambulisha kuwa ni mkazi wa Jangwani, alisema: “Kwa hali ilivyokuwa ni vigumu kuamini kuwa wamekufa watu 38 pekee. Inaweza kuwaingia akilini watu ambao hawaishi maeneo haya, lakini sisi ndiyo tunajuana.
“Ipo haja ya serikali kufanya uchunguzi zaidi, harufu inayotoka Bonde la Msimbazi ni ishara tosha kwamba kuna maiti zipo chini. Halmashauri ya Jiji inapaswa kuingia kazini ili tuwe na uhakika na ndugu zetu.”

WAFARIKI FAMILIA NZIMA
Habari ya kusikitisha zaidi ni kwamba, ipo familia ya watu watano, wakazi wa Vingunguti Dampo wamefariki dunia kutokana na madhara ya mafuriko hayo.
Watu hao ni Severina Luhwagila (27), Bakari Kihoo (10), Agnes Kihoo (5), Jeremia Kihoo (5) na Nehemia Lubida ambaye umri wake haukutajwa.
Severina ndiye mama wa familia hiyo yenye watoto watatu, Bakari, Agnes na Jeremia ambapo Nehemia ni msaidizi wa kazi za nyumbani.
Akisimulia kisa hicho, jirani wa familia hiyo, Jackson Geka, alisema: “Ilikuwa ni alfajiri ya Desemba 20, mwaka huu, nilisikia mvua kubwa ikianza kunyesha. Sikuweza kulala tena, nikatulia nikisikilizia, maana ni wazi niliona hatari kubwa mbele yangu.
“Ghafla nikaona maji yakiingia ndani, kwa tahadhari nikaanza kuitoa familia yangu na kuihamishia sehemu nyingine. Niliporudi asubuhi nikaanza kuangalia mazingira. Nilishtuka sana kuona nyumba yangu na ya jirani yangu zimeanguka kabisa.
“Nilianza kuhaha kuwatafuta, lakini sikufanikiwa kwa vile sikuwa na vifaa vya kuzamia kwenye maji. Baadaye nikaambiwa na majirani zangu kwamba walisombwa na mafuriko.”
Geka alisema, maiti nne zilipatikana baadaye,  isipokuwa moja ya Bakari ambaye jitihada za kuutafuta mwili wake bado zinaendelea.

BABA WA FAMILIA
Akizungumza na UTAMU akionekana dhahiri kuwa na majonzi mazito, baba wa familia hiyo iliyopotea yote aitwaye Erasto Kihoo (27), alisema ana maumivu makali moyoni mwake, kwani amepoteza nyumba na familia yake kwa jumla.
“Nimeteseka sana na maisha, hatimaye mimi na marehemu mke wangu tukadunduliza na kupata kakibanda ketu (nyumba), lakini leo hii nimepoteza kila kitu. Mke wangu, wanangu na msichana wangu wa kazi. Nina majonzi mazito sana.
“Si rahisi kuelezea kwa mdomo jinsi ninavyoteseka na kuungua moyoni, lakini Mungu aliye juu ndiye anayeona mateso yangu,” alisema Kihoo akijizuia kutoa machozi, lakini alishindwa.
 Kihoo hakuwepo siku ya tukio, ambapo alisema alikuwa safarini Iringa alipokwenda kumtembelea baba yake mzazi aliyekuwa mgonjwa sana.
“Naumia sana, maana inawezekana kama ningekuwepo, ningeokoa familia yangu. Sijui nitaanzia wapi?” alisema akizidi kulia.
Alisema, alisafiri siku moja kabla ya tukio (Desemba 19, mwaka huu) ndipo nyuma yakatokea maafa hayo ambayo yamemuachia maumivu makali sana maishani mwake.
Anaendelea kusimulia kwa uchungu: “Mpaka siamini kilichotokea, namaliza mwaka nikiwa sina mke tena wala watoto. Mungu anipe ujasiri, kwa nguvu zangu siwezi. Sitaweza...siwezi kabisa.”

MAAFA MENGINE
Wakati huohuo, mkazi mwingine wa Vingunguti, Hamis Kasimu Nyau,19, ameripotiwa kufariki katika mafuriko hayo.
Akisimulia chanzo cha kifo cha Hamis, mama mzazi wa marehemu huyo aitwaye Jamila Malunda, alisema mwanaye alifariki alipokuwa akifanya jaribio la kuvuka Mto Msimbazi uliojaa maji kwa ahadi ya kupewa Tsh. 1500.
“Kuna kijana alimwambia avuke mto kama anaweza, kwa malipo ya 1500, sasa kwa sababu alizihitaji hizo fedha bila kujua madhara ambayo angeweza kuyapata, akakubali kuvuka, lakini kwa bahati mbaya hakutoka,” alisema mama Malunda.
Aliongeza: “Siamini kama 1500 tu ndiyo imemtoa uhai mwanangu. Yaani nina majonzi sana.”
Kijana mwingine aliyepoteza maisha ni Nia Abdallah,19, mkazi wa Buguruni Kwa Mnyamani ambaye alikuwa katika harakati za kujikoa lakini alisombwa na maji na kuokotwa katika mto unaounganisha Mto Msimbazi.
Mafuriko hayo pia yamesababisha majonzi kwa familia nyingine ya Buguruni Kisiwani baada ya kijana wao mpendwa Ariro  Masiku, 28, kufariki  baada ya kuzolewa na maji.
Habari zinasema kuwa Ariro ambaye alikuwa anafanya kazi ya ulinzi katika kampuni moja jijini Dar es Salaam, alifariki dunia Desemba 21, mwaka huu, saa 5:40 asubuhi wakati akitoka kazini.
Marehemu Ariro aliteleza kwenye maji yaliyokuwa yakienda kwa kasi wakati akiangalia wakazi wa Buguruni walioathirika na mvua hizo wakihama kwenye maeneo yao kukimbia hatari.
Marehemu Ariro ameacha mke, Jessica Ariro na watoto wawili, Latifa na Debora, ambao  kwa sasa wapo kwa mjomba wao Mbagala, Dar.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa wakati wowote kutokea juzi Jumapili, kwenda kijijini kwao Lolwe, Nyaongo,  Wilaya  ya Rorya mkoani Mara kwa mazishi.

FAMILIA HII NAYO HAKUPONA MTU
Kigogo, Dar es Salaam, waandishi wetu walioneshwa nyumba nyingine ambayo ilidaiwa kuwa hakupona hata mtu mmoja.
Jirani wa nyumba hiyo, Samuel aliliambia Uwazi kuwa familia ya Mzee John, hakuna aliyenusurika kwenye mafuriko hayo.
“Sisi majirani tunaamini wote wamekufa kwa sababu hata nyumba imezolewa na watu wote waliokuwa wanaishi kwenye nyumba hiyo hawajaonekana mpaka leo,” alisema Samuel na kuongeza:
“Ile nyumba ilikuwa na watu kama saba hivi akiwemo mwenye nyumba, tunafuatilia lakini hakuna matumaini kama wapo salama.”  

MAONI YA WANANCHI
Wakizungumza na UTAMU kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini, wananchi wa Vingunguti walisema wameshangazwa na serikali kwa kutokuwa nao bega kwa bega katika maafa hayo.
“Nilitegemea serikali ingetoa misaada ya magari ya kubebea miili ya marehemu kwenda kuzika, maji ya kunywa, vyakula au hata baadhi ya viongozi kuhudhuria maziko, lakini jambo hilo halikufanyika.
“Sisi watu wa Vingunguti tunaona kwamba serikali imetusahau kabisa kama vile sisi siyo Watanzania. Tumeumizwa sana na hilo, lifikishe hili ndugu mwandishi, tunajua watasoma,” alisema mkazi mmoja wa Vingunguti Dampo.

BOXING DAY NA MARAHA YA COCO BEACH DAR


Watu wakifurahia mandhari ya bahari.
 Mabembea ya chini yalikuwa kivutio kwa watoto.

KATIKA kuhitimisha sikukuu ya Krismas (Boxing Day) jana, watu wengi wakiwemo wale waliokuwa na familia zao, walizuru mwambao wa Bahari ya Hindi maeneo ya Coco Beach ambako walijiachia vilivyo katika ufukwe huo wa upepo mwanana jijini Dar es Salaam ambako walipata fursa ya kuogelea, kunywa na kula kwa furaha kubwa.
Mtandao huu wa ulitembelea eneo hilo na linakuletea matukio kadhaa yaliyokuwa eneo hilo mashuhuri jijini.
 
Mabembea makubwa yaliwajumuisha hata watu wazima.

Mcheza sinema, Miriam Jolwa (Jini Kabula) alikuwepo.

Comedy ZONE


  • Jamaa mmoja mlev ucku aldumbukia kwny shmo reeefu na kuvunjka mikona na miguu yote.bac asubuh wa2 walpoamka wakamkuta hvo wakaamua kumsaidia.wakamrushia kamba aing'ate kwa meno cz alkua kavunjka mikono.wakawa wanamvuta ile imebak kdg tu.. Kuna m2 akampa pole...jamaa c akajbu "asantee" puuuuuh! Chn akaanguka tn.akaambiwa ang'ate tn kamba na sasa acseme k2.ilee kavutwa tn imebak umbak kdg tu kuna m2 akamwambia "jtahd hvohvo ucongee k2"jamaa c akajbu "sawaaa" puuuuuuh! Chn,wadau wakazla kumsaidia..

MAJI NI DAWA KUBWA LAKINI HATUJUI!


Kheri ya Krismasi mpenzi msomaji, natumaini umekula, umekunywa na umefurahia maisha, sasa ni wakati wa kuutibu mwili wako kama baada ya kula na kunywa kwenye sikukuu hii vimekuletea ‘mgogoro’ tumboni.
Bila shaka kila mtu anafahamu umuhimu wa maji, lakini si watu wote wanafahamu kuwa maji ni dawa pia, licha ya kutumika kwa ajili ya kunywa ili kukata kiu.
Nchini Japan na nchi nyingine nyingi za Bara la Asia, ni jambo la kawaida kwa watu wake kunywa maji kwanza asubuhi kabla ya kula kitu chochote.
Tabia hii ina faida kubwa kwa afya ya binadamu na hata utafiti wa kisayansi uliofanywa, umethibitisha thamani ya maji katika kuponya, kuzuia au kudhibiti magonjwa kadhaa yanayosumbua watu wengi.
Chama Cha Madaktari wa Japan (Japanese Medical Society) kimethibitisha kuwa maji yana uwezo wa kutibu, kwa asilimia 100, magonjwa sugu na maarufu yafuatayo, iwapo mtu atafuata kanuni na taratibu za kunywa maji hayo kama tiba:
Kuumwa kichwa, maumivu ya mwili, mfumo wa moyo, moyo kwenda mbio, kifafa, uzito mkubwa, pumu, kifua kikuu, uti wa mgongo, ugonjwa wa figo, magonjwa ya mkojo, kutapika, vidonda vya tumbo, kuharisha, kisukari, saratani, ukosefu wa choo, matatizo ya macho, tumbo, hedhi, sikio, pua, nk.

JINSI YA KUTUMIA MAJI KAMA TIBA
Ili maji yatumike kama tiba, kunywa kiasi cha lita moja na robo (glasi nne kubwa) za maji safi na salama (yasiwe maji baridi) asubuhi na mapema kabla ya jua kuchomoza na kabla ya kupiga mswaki.
Baada ya kunywa kiasi hicho cha maji, usile wala kunywa kitu kingine hadi baada ya dakika 45 au saa moja. Baada ya muda huo, sasa unaweza kusafisha kinywa na kula mlo wako wa asubuhi kama kawaida.
Aidha, mara baada ya kula mlo wako wa asubuhi, usile wala kunywa kitu chochote hadi baada ya muda wa saa mbili kupita. Hivyo hivyo utafanya baada ya mlo wako wa mchana au jioni.
Kwa wale wagonjwa ambao hawawezi kunywa kiasi cha maji cha lita 1 na robo kwa wakati mmoja, wanaweza kuanza kwa kunywa na kiasi kidogo watakachoweza na kuongeza taratibu hadi kufikia kiwango hicho cha glasi nne kwa siku.
Utaratibu huu wa kunywa maji ulioelezwa hapo juu, una uwezo wa kutibu maradhi yaliyotajwa hapo awali na kwa wale ambao hawana maradhi yoyote, basi wataimarisha afya zao zaidi na kujipa kinga itakayowafanya waishi maisha yenye afya bora zaidi.

UNAWEZA KUPONA BAADA YA MUDA GANI?
Yafuatayo ni baadhi ya magonjwa na idadi ya siku zake za kupona zikiwa kwenye mabano kama ilivyothibitishwa na watafiti:
Shinikizo la damu (High Blood Pressure) (siku 30), vidonda vya tumbo (siku 10), kisukari (siku 30), saratani (siku 180) na kifua kikuu (siku 90).
Kwa mujibu wa watafiti, tiba hii haina madhara yoyote, hata hivyo katika siku za mwanzo utalazimika kukojoa mara kwa mara. Ni bora kila mtu akajiwekea mazoea ya kunywa maji kwa utaratibu huu kila siku katika maisha yake yote ili kujikinga na maradhi mbalimbali.

KUNYWA MAJI ILI UWE NA AFYA NJEMA NA UBAKI MCHANGAMFU SIKU ZOTE!

Saturday, December 24, 2011

BABU LOLIONDO JELA MIAKA 7




Mchungaji Ambilikile Masapile ‘Babu Ambi’ wa Samunge, Loliondo, Arusha, atapanda kizimbani kukabili kesi za madai na jinai, hii ni kwa mujibu wa wakili maarufu, Mabere Nyaucho Marando.
Wakili huyo alisema, endapo mahakama itamkuta na hatia ya kutenda jinai, Babu Ambi, anaweza kuhukumiwa kifungo kisichopungua miaka saba jela.
Marando alisema, kesi ya jinai ambayo Babu Ambi anafunguliwa ni ile ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kwamba aliwahadaa watu kuwa dawa yake inatibu, wakati hakuna mtumiaji aliyepona.
Aliongeza kuwa kesi ya madai, inafunguliwa kwa sababu anatakiwa alipe fidia za watu waliopoteza maisha na wote waliosafiri kutokana sehemu mbalimbali wakitumia gharama kubwa kwa dawa isiyotibu.
Marando alifafanua, Babu Ambi, anaweza kukumbana na kifungo hicho endapo atakutwa na hatia kutokana na sheria ya jinai namba 302.
“Nipo makini na suala hili, hawezi kupona, nitasimamia kesi na tutamfunga,” alisema Marando na kuongeza:
“Nina taarifa nyingi kuhusu watu waliokufa, hakuna aliyepona.
Mazingira ya kisheria, yanatoa picha rahisi kuwa Babu atakutwa na hatia.”
Kutokana na msimamo huo, Marando aliwataka wale wote waliotibiwa na Babu Ambi lakini hawakupona, waende kwake kwa sababu amedhamiria kuisimamia kesi hiyo.
“Kiukweli babu aliwadanganya watu kuwa anatibu magonjwa sugu, lakini watu walipokwenda na kupata kikombe, hawakupona, na hawezi kuthibitisha mahakamani kuwa dawa yake imethibitishwa na serikali kuwa inatibu magonjwa aliyoyasema,” alisema Marando.
Aliongeza kuwa yupo tayari kuandaa kesi hizo na ndugu wote waliokunywa dawa na hawakupona, wanaweza kwenda kwake ili wakusanye ushahidi wa kutosha.
“Ni jambo linaloumiza, nitasimamia kesi hiyo na nitahakikisha anafungwa si chini ya miaka saba kama sheria inavyosema...ama zake ama zetu, alisababisha wagonjwa wa Ukimwi kuacha kutumia ARV, wengine wakatoroka hospitalini kwenda kwake na wengi wamepoteza maisha,” alisema Marando.
Wakili huyo aliigeukia serikali na kuilaumu kwa kumruhusu Babu kuwapa dawa watu wakati ikijua kuwa ilikuwa haijafanyiwa majaribio ya kitaalamu kujua kuwa kama inatibu au la.
Alisema anaweza kumfungulia kesi ya madai mchungaji huyo kwa kuwa wagonjwa wengi waliuza mali au kuchukua akiba zao na kusafiri hadi Samunge wakijua kuwa watapona baada ya kunywa dawa yake.
“Badala ya kupona wengi walifariki dunia huku wengine wakibaki masikini na hawajapona kutokana na udanganyifu mkubwa uliofanywa na Babu huyo na sasa hawawezi tena kupata mali nyingine,” alisema Marando.
Mwanasheria mwingine, Dk. Ngali Maita alipohojiwa kwa simu alisema atakuwa tayari kumsaidia mawazo ya kisheria Marando ikiwa atahitajika kwa kile alichodai, Babu alidanganya watu kuhusu tiba ya kikombe.
“Ni kitu kibaya sana alifanya Babu wa Loliondo, amesababisha maafa makubwa kwa jamii na mbaya zaidi hadi sasa uchunguzi wa dawa yake upo gizani, serikali haisemi chochote licha ya kuahidi wananchi kuwa watataarifiwa… hii ni mbaya na ni hatari,” alisema Dk. Ngali.
WAGANGA WA DAR
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Waganga wa Tiba Asilia jijini Dar es Salaam, Maneno Tamba  alisema alishangazwa sana na serikali kumruhusu Babu kufanya tiba bila kufuata sheria ya tiba asili ya mwaka 2002.
“Sifa za kutibu kiasili zimebainishwa na sheria, kwamba pamoja na sheria nyingine mtoa dawa ni lazima awe chini ya mganga wa jadi kwa miaka mitatu ndipo anaweza kusajiliwa.
Je, Babu alisajiliwa? Inafaa ashitakiwe,” alisema Tamba.
TAMOPHA
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (Tamopha), Julius Kaaya alilithibitishia gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita alipohojiwa kwa njia ya simu kuwa,  wanachama wake 14 waliopelekwa kwa Babu kutibiwa kwa majaribio, hakuna hata mmoja aliyepona.
ALICHOSEMA BABU
Babu wa Loliondo alijipatia umaarufu mapema mwaka huu baada ya kutangaza kwamba amezungumza na Mungu kwenye ndoto na kumuonesha dawa inayoitwa Mugariga inayotibu Ukimwi, Kisukari, Moyo, Kifafa na magonjwa mengine sugu.
Mchungaji Masapila alisema dawa yake ambayo ni dozi ya kikombe kimoja ilikuwa na gharama ya shilingi 500, hali iliyofanya maelfu ya watu wakiwemo mawaziri, wabunge na wafanyabiashara kwenda kwake huku wakitumia magari na wengine kukodi helikopta.
Hivi sasa idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa huko ni ndogo sana na Babu anadai hali hiyo imetokana na kupigwa vita na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa jadi.

Ze Utamu plus+++ inawatakia wasomaji wake wote Merry Christmas



Comedy ZONE



Mke wa Kelvin anajivunia mume mtulivu, hashindi baa na hatongozi
videmu. Akitoka kazini huenda kucheza basketball na hurudi nyakati za
dinner. Siku moja mkewe akamhurumia. Anachoka na kazi. Mtu gani
asiyependa starehe japo kidogo? Mke akamlazimisha outing, Kelvin
akabisha lakini taxi ikafika. Gonga Club & Lodge.

Walipofika mlangoni tu, mlinzi akaita, Mambo Kelvin! Poa
Nilidhani huwa huji club, inakuwaje mlinzi anakufahamu? mke akauliza
Yule mgambo, mchana analinda ofisini kwetu, usiku anapiga part time
hapa akajibu Kelvin.

Wakachagua meza. Kukaa tu tayari mhudumu ameshaleta castle lager.
Akamuuliza mama anakunywa nini. Mhudumu alipoondoka mama akauliza,
amejuaje unakunywa castle kama hakufahamu?

Wakati Kelvin anajikanyaga aanze vipi kujitetea, mhudumu wa vyumba
akawa amefika na kuuliza.
Mkuu kama kawaida nimekuandalia namba tano, nendeni tu vinywaji
nitawaletea huko huko

Kufikia hapo mama akawa hana simile tena, akanyanyuka akitukana kama
chizi. Akatoka nje mbio na kuingia katika taxi iliyokuwepo pale.
Wakati anapatana bei na dereva, Kelvin naye akaingia. Mama
yakamporomoka matusi kibao na kilio juu. Alipovuta kamasi na kupiga
kwikwi akamsikia dereve anasema.

Duh, eee bwana Kelvin huyu malaya uliyeokota leo balaaaaaaaaaaaaaaa!

Mamaa akazimiaaaazzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz

MAFURIKO YAENDELEA KULETA ADHA KUBWA KWA WAKAZI WA DAR


Baadhi ya wakazi wa Kigogo wakiwa juu ya paa la nyumba yao.

Wakazi Tandale wakiwa wamejikusanya kushuhudia mafuriko hayo.

Kijana aliyejitambulisha kwa jina la Ally mkazi wa Kigogo akitoka ndani ya nyumba yao iliyozungukwa  maji ambapo alimwambia mpigapicha wetu kwamba  watoto na baadhi ya ndugu zake aliwaacha ndani ya nyumba hiyo.

Wakazi hawa wa Mwananyamala Kisiwani wakivuka  eneo hilo wakiwa wamenyanyua baiskeli zao.

Wakazi wa Mwananyamala Kisiwani wakiwa juu ya paa la nyumba yao baada ya kushindwa kutoka kutokana katika nyumba hiyo.

Kina mama wakitoka katika nyumba yao iliyozingirwa maji.

Hawa walishindwa pia kwenda kufanya shughuli wakaishia kusubiri juu ya nyumba yao.

Mama na mwanawe wakitoka ndani ya nyumba yao Mwananyamala.

Kijana mkazi wa Mwananyamala Kisiwani akitoka ndani ya nyumba yao iliyojaa maji.

Mzee wa Mwananyamala Kisiwani akijiokoa na hatari ya mafuriko.

Wakazi wa Mwananyamala Kisiwani wakiwa na godoro lao juu ya paa la nyumba.

Wakazi wa Tandale wakijaribu kujiokoa baada ya kukaa ndani kwa muda mrefu.

Kijana akiwa haamini baada ya kukuta nyumba yao imezungukwa na maji wakati familia yake ikiwa ndani.

MVUA kubwa iliyoanza alfajiri ya leo jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, imesababisha  adha kubwa kwa wakazi wa jiji hili ambapo wengi wao walijikuta katika matatizo makubwa baada ya nyumba zao kuzingirwa na kujaa maji. Mpigapicha wetu alitembelea baadhi ya maeneo ya Mwananyamala Kisiwani, Kigogo na Tandale na kujionea hali mbaya iliyosababishwa na mafuriko hayo ambapo  baadhi ya watu walilazimika kupanda  juu ya mapaa ya nyumba zao na wengine hawakuthubutu kutoka ndani kabisa kutokana na nyumba zao kuzungukwa na maji.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...