Saturday, June 9, 2012

JB ATUSUA KIMATAIFA




Jacob Steven ‘JB’.
MKONGWE mwenye heshima tele kunako game la sinema za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’, ameanza kutusua kimataifa na sasa yupo mbioni kuhamishia makazi yake nchini Zambia.
Akizungumza na Tollywood Newz, wikiendi iliyopita jijini Dar, JB alisema amepata shavu hilo kutoka kwa waandaaji wa filamu nchini humo na tayari wameshakamilisha taratibu zote za yeye kwenda huko kwa ajili ya kufanya kazi za sanaa.
“Lakini kinachonikwamisha kwa sasa ni mkataba nilionao hapa Bongo, nikimaliza basi nitakwenda huko kwa sababu masilahi ni makubwa zaidi ya hapa nyumbani,” alisema JB na kuongeza:
“Kimsingi nitahamia huko na familia yangu kabisa, pia nitaongozana na wasanii wachache. Shughuli zote za filamu nitakuwa nazifanyia huko. Kiukweli jamaa wamenipa dau kubwa sana, ni mara tatu ya fedha ninayopata (kwa kila filamu) hapa nchini.”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...