Wednesday, February 29, 2012

MAHABA: MWENZI WA MAISHA NI ZAIDI YA MVUTO AU UZURI!

SINA shaka marafiki zangu mtakuwa wazima wa afya njema na maisha yanaendelea kama kawaida. Kama ndivyo ni furaha kwangu. Ninajua kwamba mpo tayari sasa kufuatilia mada niliyowaandikia leo.

Yes! Hapa ndipo kwenye kisiwa cha ujuzi wa mambo ya mapenzi. Ukiwa mdau wa ukurasa huu, mapenzi hayatakusumbua kabisa. Hebu twende tukajifunze katika mada niliyowaandalia.
Zipo sifa nyingi za mwenzi sahihi; baadhi yake ni umpende, akupende, akuvutie, awe na tabia njema, akubalike, atoke familia yenye maadili n.k, lakini vijana wa sasa huhadaika zaidi na mvuto wa sura na maumbile ya mtu wakifanya kama kipimo kikuu cha anayefaa kuwa mwenzi wa maisha, ni makosa.


Uzuri wa nje pekee siyo kati ya sifa muhimu zaidi za kumfanya awe na sifa za kuwa mwenzi wako wa maisha. Mapenzi huanzia moyoni, jiridhishe kwanza ndipo ukubali kumwingiza katika moyo wako. 


Kumbuka kuwa unapoamua kufunga ndoa na mtu ni ahadi ambayo mmeahidiana mbinguni na duniani, ni ahadi ambayo inapaswa kutenganishwa na kifo tu, siyo vinginevyo! 
Kamwe usifanye majaribio katika mapenzi, hayajaribiwi wala kujaribika! Pia, lazima umchunguze kama penzi lake ni la dhati. Katika mada zangu mbalimbali nimekuwa nikiainisha sifa za mpenzi mwenye mapenzi ya dhati, lakini kwa kukukumbusha kidogo ni kwamba, anayekupenda huwa mvumilivu, anakusikiliza pia mwenye kuwajali ndugu, marafiki na jamaa zako, anayekuheshimu na kutambua thamani yako. 


Anayetakiwa kuwa mwenzi wako wa maisha lazima awe makini na mwenye akili za kimaisha. Siyo lazima awe na elimu ya darasani, haijalishi ni mwanamke aliyekulia kijijini au mjini, lakini hapa tunaangalia uwezo wake wa kufikiri. 
Hata hivyo, inategemea wewe umepanga kuishi na mwanamke wa aina gani, lakini mwanamke ninayemzungumzia hapa ni yule mwenye uwezo wa kutosha wa kufikiri na kupambanua mambo.
Mwenye uwezo huu ni yule ambaye ukimwambia una matatizo fulani, anakuwa mstari wa mbele kukusaidia kwa hali na mali.


Mtu anayepokea mambo kwa kusikitika, hana maana kwamba anakupenda. Anatakiwa kukupa mbinu. Lazima uwe na mtu mwenye mbinu. Mwenye uwezo wa kufikiri na kupambanua mambo.
Asiye sahihi utampima hata kwa vitu vidogo tu, si wa kujishughulisha, anaishia kupiga mizinga kila siku! Asipokuambia kuhusu simu, atasema vocha, atahitaji kununuliwa nguo, pafyumu na vitu vingine vinavyofanana na hivyo.


Hawezi kuzungumzia mambo ya maendeleo. Hana mawazo chanya. Mawazo yake yanaishia kwamba wewe ni kila kitu kwake, akutegemee kwa kila kitu – akuchune. Hawezi kuwa mwenzi sahihi, hata kama ana uzuri wa kiwango gani.


Mwanamke wa aina hii unapaswa kumchunguza mapema ili usije ukaoa mzigo! Suala la uwezo wa kufikiri lina umuhimu mkubwa sana katika maisha ya sasa, ni bora mkakosa mali lakini mkawa na uwezo wa kufikiri na kutatua matatizo mbalimbali ya kimaisha.
Ni vyema pia ukajiridhisha, ni mwanamke wa ndoto yako? Unatakiwa kujiuliza juu ya uliyotarajia kwake, ni kweli unayapata yote? Hapa kuna vipengele viwili ndani ya hiki kimoja - kabla ya uhusiano na ndani ya uhusiano.


Nikianza na kabla ya uhusiano, hapa namaanisha kwamba, ana sifa zote ambazo ulikuwa unatarajia kwa mpenzi wako ajaye, ambaye ndiye huyo unayetarajia kuingia katika uhusiano naye? Ni kweli ana kila kitu kinachokuvutia kiasi kwamba hutathubutu kumsaliti? 
Ukishajiridhisha na hilo, unaweza kuingia katika uhusiano lakini siyo kwa kiasi kikubwa, hapa namaanisha kwamba, unaingia katika kipindi cha urafiki ambacho huweki kila kitu wazi, hivyo katika kipindi hiki utaweza kujua kama unapata kile ulichotarajia.


Chunguza tabia zake kwa makini katika kipindi hiki, toka naye katika matembezi ya pamoja, huku ukiwa umemweka katika kipimo ambacho hata yeye mwenyewe atakuwa hafahamu. Lazima mwisho utaweza kugundua kwamba, chaguo lako lilikuwa sahihi au lah.


Lingine lenye msingi, anatakiwa awe mtu wa kujali. Hata kama ni mzuri kiasi gani, ana mvuto kiasi gani, anakubalika na marafiki zako kiasi gani, lakini vyote hivyo vinaweza kupoteza maana kama hataonyesha anavyojali thamani yako wewe kama mpenzi wake.


Ninapozungumzia kujali, ninakuwa nimekwenda mbali zaidi, anavyojali familia yako, marafiki na hata wewe mwenyewe! Hutakiwi kuwa na mwanamke ambaye akili yake haiwazi chochote juu ya maisha. 
Mwanamke anapaswa kuwa makini, akili ziwe zinafanya kazi sawasawa na awe na mchango mkubwa wa mawazo kwenye familia. Sifa ya mvuto wake, inaweza kuharibiwa na kukosa uchangamfu na unyenyevu. 


Mwanamke hata kama ni mzuri kwa kiwango gani, akipoteza sifa hizi, uzuri wake ni kama unakuwa umepungua. Uchangamfu huu uanzie kwako, asiwe mwanamke mkimya kupitiliza, hali ambayo inaweza kutafsiriwa kwamba anaringa!


Lakini pia, uchangamfu huu anatakiwa auonyeshe hata kwa rafiki zako pamoja na ndugu zako. Mwanamke mwema ni yule mwenye unyenyekevu kwa mumewe pamoja na ndugu zake.
Marafiki, uzuri wa mwanamke hauna maana ya ubora wa kuwa mke. 



Siyo kila mwanamke anaweza kuwa mke! Mchunguze kwa makini.

MWINGIRA AKIRI KUNUNUA CHANGU


Nabii Josephat Mwingira.

ANAYEJIITA Mtume na Nabii, Josephat Elias Mwingira wa Kanisa la Efatha la jijini Dar es Salaam ambalo anadai ni la mwisho tayari kwa unyakuo,  amekiri kununua  changudoa ‘changu’ Mererani,  mkoani Arusha.

Mwingira amekiri hilo katika kitabu chake alichokiandika na kukisambaza sehemu mbalimbali  nchini kikiwa na kichwa cha habari kisemacho ‘Wito Wangu na Kusudio Langu’ ambapo amesema alibobea kwa kufanya zinaa na machangudoa.

Katika kitabu hicho chenye kurasa 34, Mwingira amesema licha ya uzinzi alibobea pia katika ulevi na kwamba siku moja akiwa na kahaba (Changu) huko Mererani Arusha alitokewa na Bwana Yesu ambaye alimuambia aachane na mambo hayo na amfuate yeye ili amtumikie.

Hata hivyo, Mwingira amesema licha ya wito huo wa Yesu, wakati huo alikuwa kwenye mazingira ambayo hayakuwa mazuri kwa sababu  alikuwa katika hali ya ulevi na mshiriki wa mambo mengi ya kidunia.

CHANGU ALITIMUA
“Yule dada (Changu) alipoona hali hiyo, akakimbia nikabaki peke yangu. Bwana Yesu akasema, mimi ninakutaka wewe uache maovu yote na unitumikie,” amesema Mwingira.
 Ameongeza kuwa baadaye wakati Yesu alipotaka kuondoka ikabidi amshike miguu na kumng’ang’ania na akamuambia,  “Usiniache!”.

Alifafanua kuwa Yesu akamshika bega la mkono wa kulia akasema, “Nitakuwa na wewe”, halafu akatoweka na baada ya hapo ndipo alipoanza kuombea watu.
Mwingira amekiri kuwa hata baada ya ‘kumuona’ Yesu, aliendelea kunywa pombe lakini ikawa anaitapika na akawa anatokewa na Kristo ndotoni au anatuma Malaika na kumuelekeza watu ambao atakwenda kuwaombea uponyaji kutokana na matatizo yao.

MCHUNGAJI AMPINGA
Hata hivyo, mchungaji mmoja ambaye hakutaka jina lake kuandikwa alipokisoma kitabu hicho alipingana na Mwingira, akasema Yesu hawezi kumtokea mtu akiwa katika harakati za kufanya ukahaba.

“Mungu anachukia sana ukahaba na mifano ipo. Aliteketeza Sodoma na Gomora ikawa jivu kutokana na watu wa kule kuendekeza ukahaba, aliunguza mji wa Babeli kutokana na mambo hayohayo, sasa siyo rahisi mtu atokewe na Yesu wakati yupo katika harakati za uhakaba,” alisema mchungaji huyo.
Aliongeza: “Mtu anaweza kutokewa na shetani la ngono kama atakuwa anaendekeza mambo hayo na baadaye kuwa moto kwelikweli wa uzinzi, hivyo kila mtu achukue tahadhari.”

Monday, February 27, 2012

ORIJINO KOMEDI KUSHNEY!!!!






KUNDI la wachekeshaji la Orijino Komedi linaloundwa na mastaa, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Joseph Shamba ‘Vengu’, Slivery Mujuni ‘Mpoki’, Alex Chalamila ‘MacRegan’ na Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’ chini ya Sekioni David ‘Seki’, linadaiwa kwisha huku kila mmoja akijiingiza katika fani nyingine ili kujipatia mkate wa siku.

UPEKUZI WABAINI SIRI NZITO
Kwa muda mrefu sasa, malalamiko ya mashabiki wa mastaa kuwa michezo yao mipya haionekani kama zamani huku wakidaiwa kurudiarudia ya zamani.

Kwa mujibu wa vyanzo makini vilivyozungumza, kundi hilo linaloruka hewani kupitia Runinga ya TBC 1, linadaiwa lilimaliza mkataba wake tangu Januari Mosi, mwaka huu na kusitisha uandaaji wa vipindi vipya.

INASIKITISHA
Ilidaiwa kuwa vijana hao watafutaji wamekuwa kwenye wakati mgumu kimaisha kwani walitarajia kulamba mkataba mpya hivyo baada ya kuona kimya, kila mmoja akaanza kusaka ‘ngawira’ katika fani nyingine.

MASANJA
Ilielezwa kwamba Masanja amejikita kwenye muziki wa Injili akiwa kwenye ‘tizi’ la uchungaji, utangazaji na ushereheshaji.

MPOKI
Kama ilivyo kwa Masanja, pamoja na kwamba alianza muziki wa Kizazi Kipya akiwa bado anachekesha kideoni, Mpoki sasa amejikita katika Bongo Fleva na utangazaji huku akiuza nyago kwenye video za wasanii wa muziki Bongo.

VENGU
Kwa upande wake Vengu yuko kwenye matibabu nchini India baada ya kusumbuliwa na maumivu sehemu ya kichwa kwa muda mrefu.

JOTI
Joti kwa sasa anajihusisha na muziki wa kizazi kipya huku kukiwa na taarifa kwamba pia amekuwa akilamba dili za ushereheshaji.

WAKUVWANGA NA MACREGAN
Jamaa hao wakali wa kuchekesha walidaiwa kuwa kwa sasa hawaonekani kideoni lakini wamekuwa wakilamba shavu kwenye shughuli za ushereheshaji.

NDIYO MWISHO WA KUVUNJA WATU MBAVU?
Ilielezwa kuwa kuonekana kwao wakijishughulisha na mambo mengine bila kurekodi vipindi vipya, inawezekana ndiyo mwisho wa kuvunja watu mbavu.

Tukizungumza na mastaa hao kujua kulikoni, lakini wamekuwa wakirusha mzigo kwa Seki kuwa ndiye mwenye ‘a na be’ ya hatima ya kundi hilo hivyo aulizwe yeye.
Akizungumzia ishu hiyo, meneja wa programu hiyo wa TBC1, Mwanga Slay alikuwa na haya ya kusema:
“Kwa taarifa kamili ni vizuri mkazungumza na Seki kwa sababu yeye ndiye anayeweza kulizungumzia.”

SEKI VIPI?
Juhudi za kumpata Seki hazikuzaa matunda baada ya simu yake kutokupokelewa kila ilipopigwa hivyo bado zinaendelea.

Saturday, February 25, 2012

ISHARA ZA MWANAUME AMBAYE HANA NIA AU HATAKI KUWA NA WEWE KATIKA MAHUSIANO YA KUDUMU (NDOA) NA WAKATI KIPINDI HICHOHICHO ANAKUTAMKIA NENO “NAKUPENDA”...


1.HAPIGI SIMU, BALI HUTUMIA SMS

Je, Kijana Huyu Aliyekwambia Anakupenda Huwa Anawasiliana Nawe Kwa Njia Ya Ujumbe Mfupi Kuliko Anavyokupigia? Kama Utaona Hivyo, Basi Una Kila Sababu Ya Kuanza Kuitilia Shaka Nia Ya Kijana Huyu Wa Kiume, Kwani Kwa Hakika Hana Nia Yoyote Ya Dhati Ya Kuendelea Kuwa Nawe.

Kijana Wa Kiume Anapompenda Msichana, Hutamani Muda Wote Kuisikia Sauti Yake. Anapokuwa Anasisitiza Kutumika Kwa Ujumbe Mfupi Maana Yake Hana Haja Sana Ya Kusikia Sauti Yako. Naam, Ujumbe Mfupi Wa Maneno Si Njia Rahisi Sana Ya Kuwasiliana, Lakini Zaidi Ni Njia Rahisi Zaidi Ya Kuepuka Mawasiliano Na Kutoa Majibu Mafupi Kwa Mtu Ambaye Usingependa Kuwasiliana Naye.

2.ANA SABABU ZA KUCHELEWA

Unaweza Kubaini Katika Mikutano Yako Miwili-Mitatu Na Kijana Aliyekwambia Anakupenda, Kwamba Si Mtu Wa Kujali Wala Kutunza Muda. Naam, Yawezekana Katika Mara Mnazokutana, Mara Nyingi Zaidi Anachelewa Kuliko Anavyowahi. Unaweza Kudhani Kuwa Kijana Huyu Ana Mambo Mengi, Au Si Mzuri Katika Upangiliaji Wake Wa Muda, Lakini Kwa Hakika Hupaswi Kumtafutia Visingizio Hata Kama Unampenda, Kwani Kuna Uwezekano Mkubwa Kuwa Kijana Huyu Hana Mpango Na Wewe.

Kijana Wa Kiume Akikupenda Na Kupenda Kuendelea Kuwa Nawe, Lazima Tu Atakuwa Na Msukumo Wa Kutaka Kukutana Na Wewe Na Hatapenda Kukuudhi Kwa Kuchelewa. Mtu Huyu Hata Kama Atakuwa Amebanwa Vipi Kazini Ni Rahisi Sana Kutafuta Muda Wa Kukutana Na Wewe. Kinyume Chake Atakuwa Ni Mtu Wa Visingizio Vya Kuchelewa Na Wakati Mwingine Kutofika Kabisa Katika Eneo La Miadi – Hususan Kama Ameshakupata.

3.ANAWASILIANA NA MPENZI WA ZAMANI

Mwanamume Asiye Na Mpango Wa Kuendelea Kuwa Nawe Anapokuwa Amekutongoza Na Pengine Mmekutana Mara Moja Au Mbili, Atakutaarifu Kwa Kuendelea Kuwasiliana Na Mpenzi Wake Wa Zamani.

Kwa Hakika, Hakuna Jambo Ambalo Humsahaulisha Mwanamume Mpenzi Wa Zamani Kama Kumpata Mpenzi Mpya Anayempenda Kwa Dhati. Iwapo Ataendelea Kuwasiliana Na Kuzungumza Na Mpenzi Wake Wa Zamani, Hiyo Ni Ishara Kuwa Hajamalizana Na Mpenzi Wake Huyo Wa Zamani Na Pengine Bado Anatarajia Kurudiana Naye. Lakini La Muhimu Zaidi Ni Kwamba, Mwanamuke Huyu Hakupendi Kama Unavyodhani Na Wala Hajawa Tayari Kuwa Nawe Kama Mpenzi Au Mchumba.

4.HAKUTAMBULISHI KWA MARAFIKI

Mwanamume Akikupenda, Hususan Vijana Katika Zama Hizi, Lazima Tu Atakutambulisha Kwa Marafiki Zake, Maana Atakuwa Anajisikia Fahari Kwa Kufanya Hivyo, Hususan Kama Anahisi Wewe Ni Mwanamke Maridadi.

Kwa Hulka, Lazima Tu Kijana Wa Kiume Atataka Kujionesha Kwa Watu Anapokuwa Na Kimwana Maridadi Na Anayempenda Kwa Dhati. Usipoona Dalili Zozote Za Jambo Hili, Basi Chukulia Tu Kuwa Kijana Huyu Wa Kiume Hajakupenda Kama Unavyodhani.

5.HUEPUKA WATU KUWAONA PAMOJA

Mwanamume Asiye Na Mpango Wa Kuendelea Kuwa Nawe Katika Uhusiano, Hujitahidi Kuepuka Watu Kuwaona Pamoja. Ni Kweli Kuwa Si Vijana Wote Wa Kiume Wanaopenda Mapenzi Ya Maonesho Ya Kushikana Mikono Wanapotembea, Lakini Kama Ameridhika Nawe Lazima Tu Kwa Kiasi Fulani Atataka Umma Ujue.

Kwa Hakika, Kijana Wa Kiume Anapokuwa Amempenda Msichana Kwa Dhati, Hujikuta Akifanya Hata Mambo Ambayo Zamani Alikuwa Hadhani Kuwa Anaweza Kuyafanya, Ikiwa Ni Pamoja Na Kuonesha Mapenzi Hadharani, Japo Kwa Idhara Ndogo Ndogo. Kwa Tamaduni Za Magharibi Ni Kawaida Kumbusu Mpenzi Hadharani Au Kumzungushia Mkono Kiuononi, Au Kumshika Mkono, Au Kumbusu. Lakini Afrika Hata Kutoka Naye Nje Mkizungumza Huwafanya Watu Washuku Jambo. Kama Hukuliona Hilo Kwa Mpenzi Wako, Basi Chukulia Tu Kuwa Unapoteza Muda.

6.HAZUNGUMZII MIPANGO YA BAADAYE

Unapokuwa Unazungumza Na Mwanamume Ambaye Ana Mpango Wa Kuwa Nawe Katika Kipindi Chake Cha Maisha Yaliyobaki, Lazima Tu Utambaini Akiingiza Mambo Yanayohusiana Na Maisha Ya Baadaye Mkiwa Pamoja. Kwa Hakika, Utambaini Mwanamume Huyu Akitumia Nafsi Ya Kwanza Wingi Tena Katika Muda Wa Baadaye, Yaani Akizungumza Mambo Ambayo Atafanya Na Wewe Miaka Ijayo.

Iwapo Atazungumzia Klabu Fulani Aliyoiona Karibuni Lakini Akawa Hagusii Kuwa Mtakwenda Huko Siku Moja – Tena Mbaya Zaidi Akawa Anasema Kuwa Huwa Anakwenda Pale Mara Kwa Mara, Basi Tambua Kuwa Hauko Katika Mipango Yake Ya Baadaye.

7.HAKUNA MATENDO YA MAHABA

Mwanamume Asiye Na Mpango Wowote Na Wewe Si Aghalabu Kukufanyia Jambo Ambalo Utaliona La Kimapenzi Au La Kimahaba, Hususan Anapokuwa Amefanikiwa Kufanya Mapenzi Na Wewe. Ukiona Hivi, Shtuka Mapema Na Anza Kuangalia Ustaarabu Mwingine.

Haina Maana Kuwa Asipokununulia Maua Basi Hana Mpango Nawe, Lakini Angalau Mara Moja Moja Akufanyie Jambo Au Angalau Atoe Kauli Ambayo Itakusisimua Na Kukufanya Ujione Wa Thamani Na Wa Pekee Machoni Pake.

8.MIPANGO UNAPANGA WEWE

Iwapo Utabaini Kuwa Asilimia 80 Ya Mambo Mnayofanya Pamoja Unayaanzisha Wewe, Basi Una Kila Sababu Ya Kuutilia Shaka Mustakabali Wa Uhusiano Wenu.

Kama Ilivyobainishwa Awali, Mwanamume Akikupenda Atataka Mwe Pamoja Muda Mwingi, Lakini Kama Utabaini Kuwa Mipango Mingi Unaanzisha Wewe Na Unazungumza Naye Kwenye Simu Ijumaa Na Mnamaliza Bila Mwanamume Huyu Kuonesha Dalili Za Kutaka Kuwa Nawe Wikiendi, Japo Kwa Kinywaji, Basi Chukulia Kuwa Mwanamume Huyu Hana Nia Yoyote Ya Kuwa Nawe Kwa Muda Mrefu Zaidi.

9.HANA MPANGO NA WATU WAKO

Mwanamume Anayekupenda Atajishughulisha Na Mambo Yanayohusiana Na Watu Wako Wa Karibu, Hususan Ndugu, Jamaa Na Marafiki Zako. Iwpao Utabaini Kuwa Mwanamume Huyu Haulizi Swali Lolote Kuhusiana Na Familia Yako Au Marafiki Zako, Basi Tambua Kuwa Hana Mpango Wowote Wa Maana Na Wewe. Kumbuka Mwanamume Akikupenda Hujaribu Kuwafahamu Na Kuwapenda Watu Wako, Maana Amependa Boga Na Sheria Ni Kwamba Lazima Upende Na Ua Lake.

10.HAKUMBUKI LOLOTE LA MAANA

Ni Wazi Kuwa Hujakaa Sana Na Mwanamume Huyu, Lakini Angalau Kuna Mambo Muhimu Umefanya Naye Ambayo Anapaswa Kuyakumbuka. Kama Hawezi Kukumbuka Tarehe Muhimu Za Uhusiano Wenu, Mathalani Tarehe Mliyokutana Mara Ya Kwanza, Au Siku Mliyofanya Mapenzi, Basi Yamkini Mwanamume Huyu Hana Mpango Wowote Wa Dhati Wa Kuendelea Kuwa Nawe.

USIPOTEZE MUDA

Hakuna Mtu Mwenye Lengo La Kukuvunja Moyo, Lakini Ujumbe Ulio Dhahiri Ni Kwamba, Kama Unafikiria Uhusiano Wa Kudumu Na Mtu Kisha Akawa Anaonesha Ishara Zilizobainishwa Hapa, Basi Tambua Tu Kuwa Huyo Si Wako Na Atakupotezea Muda Wako Bure. Wala Usijaribu Kumlazimisha, Maana Mambo Ya Kulazimisha Huwa Hayadumu.

Ni Muhimu Sana Kuhakikisha Kuwa Mtu Unayetaka Kujenga Naye Uhusiano Wa Kudumu Anakupenda Kwa Dhati. Wala Haipendezi Kumng’ang’ania Mtu Ambaye Mapenzi Yake Kwako Ni Nusu Nusu. Hakikisha Kuwa Mtu Unayempenda Na Unayetaka Kuwa Naye Ni Yule Ambaye Amekuzimikia Na Atamani Sana Kuwa Nawe. Mtu Huyu Utampata, Hususan Kama Wewe Mwenyewe Utaweka Jitihada Za Makusudi Na Kujiweka Katika Hali Ya Kupendwa Na Kupendeka.

Friday, February 24, 2012

MASAA 120 KABLA YA NDOA: BI. HARUSI ANASWA AKIJIUZA...




 Mwanahamisi Hamis akifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Sokoine Drive, Dar es Salaam.

 Mwanahamisi Hamis (wa kwanza kushoto) akiwa na wenzake Salima Juma na Halima Amir kizimbani.

Mwanahamisi akitafakari jambo.


AMA kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Usemi huu unakamilishwa na tukio la hivi karibuni ambapo msichana aliyefahamika kwa jina la  Mwanahamisi Hamis, mkazi wa Buguruni, Dar es Salaam na wenzake wawili, Salima Juma na Halima Amir, walipandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Sokoine Drive, Dar na kusomewa shitaka la kunaswa sehemu ya wazi wakidaiwa kujiuza.

Wakati kesi ikiendelea, ilibainika kuwa Mwanahamisi ni Bi. Harusi mtarajiwa na vikao vya harusi vilikuwa vikiendelea huku ndoa yake ikitarajiwa kufungwa mwishoni mwa mwezi huu, takribani saa 120 kuanzia leo.

Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi, mnamo Februari 16, mwaka huu, majira ya saa saba usiku, washitakiwa hao walikamatwa maeneo ya Buguruni wakifanya vitendo haramu vya ukahaba.

Washitakiwa wote walikiri kutenda kosa hilo lakini walimuomba hakimu anayesikiliza kesi yao, Timothy Lyon awasamehe kwa vile ilikuwa mara yao ya kwanza kufikishwa mahakamani hapo kwa kosa hilo.

Pamoja na ombi hilo, mwendesha mashitaka Magodi alimuomba hakimu kutoa adhabu kali kwa washitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine wenye vitendo kama vyao.

Baada ya msumari huo wa mwendesha mashitaka, hakimu aliahirisha kesi hiyo na kuwanyima dhamana washitakiwa mpaka Februari 20 (leo).

Hata hivyo, Mheshimiwa Lyon alimhukumu mshitakiwa Salima Juma kwenda jela miezi 6 kufuatia kuonesha utovu wa nidhamu mahakamani pale alipomtaka hakimu atengue maamuzi ya awali.

Kifungo hicho kilimfanya Salima kuangua kilio akiwa haamini masikio yake.
Wakati huo huo, watu waliodaiwa kuwa ni miongoni mwa wanakamati wa harusi ya Mwanahamisi walionekana wakihaha mahakamani hapo kumnasua Mwanahamis kwenye aibu baada ya hakimu kuwanyima dhamana.

“Hii sasa aibu jamani, yule Mwanahamisi ni Bi. Harusi mtarajiwa, badala ya kutulia nyumbani anazurura hovyo usiku wa manane mpaka anafedheheka kiasi hiki,” alisema mwanamke mmoja aliyedai ni mwanakamati wa harusi hiyo.

Hata hivyo, mwanamke huyo alifunga ‘bakuli’ lake kufuatia kugundua kwamba alikuwa akihojiwa na paparazi baada ya kujitambulisha kwa ajili ya kupata data zaidi za harusi hiyo.

Mastaa wakiri kushea mabwana



Wema.
Shilole.

Uwoya.


MINONG’ONO ya muda mrefu kuhusu mastaa wa kike Bongo kuchangia wanaume, sasa imepata majibu baada ya kuthibitika kwamba vitendo hivyo vimeshamiri sana miongoni mwao...

Habari zisizo na shaka zinasema kwamba mastaa hao wamekuwa wakipangwa bila kujijua na wakati mwingine wakiwa na taarifa ya mchezo mzima huku wakijua kufanya hivyo ni kuhatarisha afya zao.

MAMBO HADHARANI
Chanzo chetu, ambacho ni miongoni mwa mastaa wanaowika kwenye tasnia ya filamu, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, alisema mtindo huo upo sana na umekuwa ukiibua mabifu baina yao.
“Haya mambo yapo, yaani hakuna amani kabisa, unakuta staa ana mpenzi wake, lakini bila kujua mwenzake anaanza kujitongozesha kisha naye anatoka naye,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza:
“Hata huu mgogoro wa Wema (Sepetu), Wolper (Jacqueline) na Uwoya (Irene) chanzo chake kilikuwa mambo hayo hayo, sema walikuwa wanashindwa tu kuweka wazi.

“Ukweli Wema alikuwa analalamika kwamba Wolper anajipitisha tena kwa Diamond, wakati mwanzoni alimuacha akiwa hajawa maarufu. Uwoya naye hakuwa na imani na Wolper kwa madai kwamba alikuwa anajigonga kwa Ndikumana.”

Maelezo ya mnyetishaji wetu huyo yalienda mbali zaidi, yakisema kwamba, imefikia hatua staa akiwa na uhusiano na mwanaume wake anamficha kwa rafiki zake ili asitegwe.
“Hasa huku kwetu kwenye filamu ndiyo kuna haya mambo zaidi. Sijui hawaoni kinyaa?” alisema.

MASTAA WAFUNGUKA
Kwa nyakati tofauti lilifanya mahojiano na baadhi ya mastaa wa tasnia mbalimbali Bongo kuhusu madai haya, ambapo wengi walikiri.

Mmoja wa mastaa hao ambaye hakupenda kuandikwa jina lake kwa kuhofia kunyimwa dili, alisema wasichana ndiyo wamekubuhu zaidi kwenye mchezo huo ambao si wa kistaarabu.
“Nakwambia ukionekana unapendeza, unatunzwa vizuri na mwanaume wako, nao wanamuwinda ili wamtie mkononi. Ni tabia ya hovyo sana,” alisema msanii huyo, mweupe mwenye figa namba nane.
Mastaa waliopata kuzungumza na Ijumaa na kutoa ushirikiano ni Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, Aunt Ezekiel, Jacqueline Dustan, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Baby Joseph Madaha, Lucy Komba na Belina Mgeni, soma walichokisema hapa chini.

KABULA
“Tabia hiii ipo sana, kikubwa ni tamaa...mtu akiona upo na fulani anajua unafaidi, hivyo na yeye anajiingiza akijua atapata kama unavyopata kumbe hajui ni nyota ya mtu tu.”

AUNT
“Hiyo tabia ipo na si nzuri, kila mtu anatakiwa kumheshimu mtu ambaye alikuwa na uhusiano na rafiki yake ili kujenga heshima.”

JACQUELINE
“Tabia hiyo ni mbaya sana na ipo kwa mastaa wa hapa kwetu Bongo. Kiukweli haileti picha nzuri kabisa kwa jamii, unashindwa kueleweka.”

SHILOLE
“Najua kwamba wapo mastaa wenzetu wenye tabia hiyo, ila nawatahadharisha, kwangu mimi mtu asijaribu kabisa, nitamwangamiza! Siyo tabia nzuri, kwa kweli inakera.”

MADAHA
“Hiyo ipo kweli na ni kujivunjia heshima, unajua mwanaume wa shoga yako ni sawa na shemeji yako kwa dada’ko, sasa inakuaje unatembea naye? Inaudhi sana. Kiukweli hata jamii haituelewi.”
BELINA
“Mastaa wengi wamefanya kama ndiyo mchezo siku hizi, naamini ni tamaa tu ndiyo inawaponza na si kingine. Mtu aliyetembea na rafiki yako ni shemeji yako na hao wanaume wanatudharau sana kwa mtindo huo.”

LUCY
“Tabia  hiyo ni mbaya na ipo kwa mastaa wengi, kama tukiendelea hivi, hii heshima ambayo tunaililia, hatuwezi kuipata kamwe. Ni lazima mastaa tubadilike, tuheshimiane.”

WAKIRI KUAMBUKIZANA UKIMWI
Baadhi ya mastaa waliopata kuzungumza na Ijumaa walikiri kwamba mchezo huo ni hatari na ni rahisi kuambukizana ukimwi.

Jacqueline Pentenzel ‘Jack wa Chuz’, aliye staa katika kiwanda cha filamu Bongo, alisema: “Wapo wasanii wanadaiwa kuwa na ngoma, lakini piga picha kwa mapenzi yetu haya, unatoka kwa msanii huyu unakwenda kwa yule bila kinga, nini kitatokea? Lazima kuna kuambukizana hapo.”

Mwingine aliyezungumzia hilo ni Aunt ambaye alikuwa na haya ya kusema: “Mtu yeyote asipotumia kinga wakati wa kufanya mapenzi hiyo inakuwa ni ngono zembe na lazima atapata ukimwi ikiwa anayefanya naye atakuwa na maambukizi.”

"Mawazo"-Diamond(Official Video)



Thursday, February 23, 2012

DIAMOND KUFUNGA NDOA USIKU





Naseeb Abdul ‘Diamond’.

Natasha.

Wema Sepetu.

MWANAMUZIKI ‘sharobaro’, Naseeb Abdul ‘Diamond’ ameianika dhamira yake ya kutaka kuoa ndani ya siku chache zijazo huku akidai tukio hilo litafanyika usiku.
Diamond ambaye aliwahi kuwa mchumba wa msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu aliyasema hayo hivi karibuni akiwa nchini Afrika Kusini alipokuwa akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu juu ya maisha yake ya kimapenzi na kimuziki.


Alisema, mwaka huu hautaisha bila kufanya tukio hilo muhimu ambalo amekuwa akishauriwa na ndugu zake kulitekeleza haraka.


Anamuoa nani?
Huku kukiwa na minong’ono kuwa huenda msanii huyo akamuoa demu aliyewahi kudaiwa kutoka naye aitwaye Natasha au Miss Tanzania namba 2, 2006, Wema Sepetu, Diamond alisema:
“Najua wengi wanataka kumjua mchumba wangu ila itakuwa ni mapema mno kumtambulisha, wala siyo hao ambao watu wanawatajataja, tena mchumba wangu wa sasa siyo staa.”


Kwa nini ndoa usiku?
“Nimeamua tu, nitaifunga baada ya swala ya Inshah (saa mbili usiku). Ishu ya lini nitafanya hivyo nitawaambia baada ya kinyang’anyiro cha Tuzo za Kili kuisha maana sasa hivi nimeelekeza mawazo na nguvu zangu huko.


“Mchumba wangu nitamtambulisha siku ya fainali ya Kili Awards. Wadau wangu wanipe tu sapoti katika kipindi hiki ili hata pale nitakapokuwa naoa niwe na furaha ya kupata tuzo,” alisema Diamond.
Oktoba mwaka jana, Diamond alimvisha pete ya uchumba Wema lakini uchumba wao haukudumu kufuatia kutokea mazingira ya kutokuelewana kati yao.

UWOYA MIMBA NJE YA NDOA?




GUMZO kubwa jijini Dar es Salaam kwa sasa ni madai kuwa Irene Pancras Uwoya ana mimba kwa mara nyingine huku mwanaye Krish akiwa na takribani miezi nane tu!!!

ISHU ILIANZA DESEMBA, MWAKA JANA
Madai ya Uwoya kuwa ‘ameshiba’ tena nje ya ndoa kabla hata Krish hajafikisha miezi nane, yalianza kuzagaa Desemba, mwaka jana, ‘kitumbo’ kikiwa na miezi takribani miwili.

ETI KITUMBO KINA ZAIDI YA MIEZI MINNE
“Tunapozungumza sasa hivi, ujauzito wa Uwoya umetimiza miezi minne, anaingia wa tano, kama mnataka ushahidi, mtafuteni mpate picha ya tumbo lake halafu mlinganishe na siku za nyuma baada ya kujifungua Krish,” alisema mmoja wa mashosti zake wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina.

HAIONEKANI KAMA ILE YA KRISH
Ilidaiwa kuwa mwanzoni Uwoya hakugundua kama ilivyokuwa mimba ya Krish kwani hadi inatimiza miezi minne hakugundua chochote hadi alipokwenda kupima.

‘MMECHELEWA KUJUA’
Akizungumza  kwa sharti la kutochorwa jina lake, rafiki kipenzi wa Uwoya alionekana kushangazwa kwa kitendo cha kumhoji jambo ambalo limeshakuwa wimbo wa taifa.
“Ngoja niwachane laivu, kusema kweli mmechelewa kujua kwani wasanii wote wanajua ishu hiyo,” alisema rafiki huyo.

NI YA NJE YA NDOA?
Madai mengine ya kushtua ni kuwa mimba hiyo ni ya nje ya ndoa ambapo baada ya mumewe Hamad Ndikumana ‘Kataut’ kuchezwa na machale, alilifikisha suala hilo kwa wazazi wa Uwoya ambapo familia ilikaa kikao.

“Janet (shosti wa Uwoya) alikuwepo kwenye kikao lakini alichomolewa kwa sababu fulani fulani, nasikia ni mmoja wa watu waliohusika kuvujisha ishu hiyo,” alisema mdaku wetu aliyenasa mkanda kamili.
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa hadi kikao hicho cha saa kadhaa kinamalizika, hakikueleweka kufuatia Uwoya kutia ngumu kumtaja mhusika huku aking’ang’ania kuwa mwenye mali ni Ndiku.

ETI UWOYA ALISHAURIWA KUICHOROPOA, AKAGOMA
Kwa mujibu wa staa mkubwa wa kike wa filamu ambaye Uwoya anamheshimu (jina linahifadhiwa), mwanzoni mama Krish alishauriwa kufuata uzazi wa mpango kwa kuichoropoa mimba hiyo ili kuweka uwiano kati ya Krish na mtoto mwingine atakayezaliwa, lakini staa huyo aligoma.
“Uwoya anapenda sana watoto ‘so’ alikataa kuichoropoa na kama utakumbuka hivi karibuni alisema kuwa atazaa mpaka basi kwa sababu anataka kuwa na kichanga kila mara.

UWOYA LAIVU
Baada ya ishu hiyo kuendelea kushika kasi mithili ya moto wa kifuu katika ulimwengu wa mastaa wa Kibongo, Amani lilifanya mahojiano na Uwoya ambapo mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo;
Hotpot: Mambo vipi Uwoya?
Uwoya: Poa, najua kuna jambo ‘so’ ulizeni niwape ukweli wenu.

Hotpot: Kwanza hongera kwa ujauzito wa mdogo wake Krish.
Uwoya: Teh, teh, tehee! Nani kawaambia?

Hotpot: Habari zilizozagaa kila kona ya Jiji la Dar zinasema wewe ni mjamzito wa miezi minne unakwenda wa tano, je, ni kweli?
Uwoya: Mh! Yaani mtaani wanasema nina mimba? Naomba ieleweke kuwa sina ujauzito.

Uwoya aliyefunga ndoa na Ndiku mwaka 2009 na kujaliwa mtoto mmoja wa kiume mwaka jana, Krish, hakuwa tayari kufafanua juu ya ama mimba hiyo ni ya nje ya ndoa au la, zaidi ya kung’ang’ania kuwa hana kibendi.

UGONJWA HATARI ZAIDI YA UKIMWI WAGUNDULIKA: Ni ugongwa unaokadiriwa kuja kuua nusu ya watu dunia nzima....



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhpAmLzl32iyQ3Y-I5K8gVIkAdsc7TzHCX4a6cmmnBenRfym5ZNTU4b7dkYisUdMGlis286IhgmGJQP7dj0S4I-QsJiy-uoqwbOBHrxJpoQh9NMhoSaed8ZjBhHt_XqbGqLzbzNYPuUDu8/s1600/HIV+Virus+AIDS+History%252C+Symptoms%252C+Causes%252C+Diagnosis%252C+Prevent%252C+Handling+chronic.jpg

WANASAYANSI nchini Uholanzi wametengenezea virusi vinavyotishia kuua nusu ya watu duniani kote, vinavyoelezwa kuwa ni hatari zaidi ya vile vya Ukimwi.

Kwa mujibu wa habari zilizoenea duniani kote hivi karibuni zilizofichuliwa na Gazeti la Corriere della Sera la nchini Italia, Kituo cha Tiba cha Erasmus cha Uholanzi ndicho kilichohusika na utengenezaji wa virusi hivyo vya kuambukiza vinavyoweza kuua kwa kasi ya ajabu.

Gazeti hilo liliandika kuwa, utengenezaji huo uliokamilika mwishoni mwa mwaka jana uligundua kuwa virusi hivyo ni aina ya virusi vya mafua ya ndege vya H5N1 na kwamba vina uwezo wa kuambukizwa kwa njia ya hewa kwa mamilioni ya watu.

Mtaalamu wa Kituo cha Tiba cha Erasmus cha Uholanzi, Ron Fouchier alisema kuwa kirusi hicho kimepatikana kwa kufanya mabadiliko katika kirusi cha H5N1 (kile cha mafua ya ndege).
Ron aliongeza kuwa virusi hivyo ambavyo ni aina ya bakteria wanaohifadhiwa kwenye chupa ni miongoni mwa virusi hatari zaidi ambavyo vimekwishatengenezwa hadi sasa.

Utengenezaji wa virusi hivyo umezusha wasiwasi mkubwa huku wataalamu wakihoji hekima na sababu ya kupoteza mamilioni ya fedha kwa ajili ya ishu hiyo ambapo makundi ya kigaidi kama Al-Qaeda, Al-Shabaab na Boko Haram yakiinasa, yatamaliza watu duniani.

Tuesday, February 21, 2012

Mastaa wampongeza Kanumba kumchana baba yake...


Steven Kanumba.

KATIKA hali isiyotarajiwa na wengi, baadhi ya mastaa wa filamu Bongo wamempongeza mwenzao Steven Kanumba kwa kitendo cha kumchana baba yake. 

Kanumba wiki iliyopita kupitia Kipindi cha Take One kinachorushwa hewani kupitia Clouds TV alimtolea uvivu ‘mshua’ wake, Mzee Charles Kusekwa akidai amechangia katika mateso aliyoyapata utotoni mwake.

Baada ya Kanumba kueleza hayo, baadhi ya watu wakiwemo wasanii wenzake walimshangaa na kueleza kuwa kitendo alichokifanya si cha kiungwana kwani mzazi ni mzazi tu, hata kama amekosea si sahihi kumdhalilisha.

Hata hivyo, wapo wasanii waliompongeza msanii huyo kwa uamuzi aliochukua wakidai ni njia sahihi ya kutoa machungu yake!!!

LAANA: Wake za watu wavua nguo HADHARANI



DUNIA imekwisha! Kitendo cha wake za watu kuvuana nguo hadharani tena mbele ya watoto kilichojiri hivi karibuni mjini hapa, kimetafsiriwa kuwa ni laana...

NI TUKIO LA AIBU
Tukio hilo la aibu lililoshuhudiwa na paparazi wetu lilijiri Jumapili iliyopita kwenye sherehe ya kumtoa nje mtoto aliyekuwa anatimiza siku 40 tangu alione jua, lilisababisha bibi wa mtoto huyo aliyetajwa kwa jina moja la Bi Matha kuangua kilio kwa kushindwa kuvumilia uchafu huo.

Katika shughuli hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Bi Matha, mtaa wa Kibodya jirani na Msikiti wa Mwembesongo mkoani hapa, ilipambwa na matukio makuu matatu.

Tukio la kwanza lilikuwa ni Maulidi ya kumtoa nje mtoto huyo lillilofanywa na Madrasa ya Alhasaniyyah ya Msikiti wa Kingo mjini hapa ambapo watu walikula nyama ya mbuzi, maandazi na chai.

Tukio la pili ni baada ya masheikh waliofika kumuombea dua mtoto huyo kuondoka eneo hilo, mama wa mtoto aliyetajwa kwa jina moja la Amina kwa kushirikiana na mashosti zake, walianza shughuli ya kusasambua kwa kuligombea sanduku la zawadi za mama mtoto ambapo zoezi hilo liliongozwa na bendi ya matarumbeta.

‘KUFULI’ NJE
Wakati wakiendelea kusasambua, mmoja wa wanawake hao, alipanda juu ya meza ambapo baadhi ya mashosti zake walimvua khanga aliyokuwa amevaa hivyo kumfanya aache wazi sehemu zake nyeti.

HAIJAWAHI KUTOKEA
Katika tukio hilo ambalo halijawahi kutokea, wanaume walikuwa wakitokwa udenda huku watoto nao wakishuhudia uchafu huo wa mama zao.

Tukio la tatu lilikuwa ni disko la usiku maarufu kama kigodoro, huku ndiko kulifanyika matukio ya laana kubwa ambapo vitendo vya ngono vilichukua nafasi kubwa.
Baada ya kuwepo kwa mvutano mkubwa baina ya ‘memba’ wa familia hiyo ambao hawakukubaliana na shughuli hiyo ya kusasambua, ‘polisi’ wa Ijumaa alizungumza na wahusika mmoja baada ya mwingine.

BIBI WA MTOTO ANASEMAJE?
Bi Matha ambaye alishindwa kuvumilia vitendo hivyo vilivyoitia aibu familia na kufikia hatua ya kukosa amani, aliliambia Ijumaa kuwa hakupendezwa na vitendo vilivyofanywa na binti yake kuruhusu mashosti zake kuvuana nguo kwenye shughuli ya mjukuu wake.

BABA AFUNGUKA
Kwa upande wake baba mzazi wa mtoto huyo aliyetajwa kwa jina moja la Abdallah alikuwa na haya ya kusema:
“Nilimkataza mke wangu jambo hilo lakini alikaidi kwa kujitetea kwamba naye huwa anawachangia wenzake kwenye matukio kama hayo hivyo ilikuwa zamu yake kuchangiwa. 

“Kwa kuwa shughuli ilikuwa inafanyika kwa mama yake nikawa sina uwezo wa kuzuia, lakini niseme tu kwamba mimi nina hofu ya Mungu ndiyo maana niliamua kumtoa mwanangu kwa kumsomea dua ya Maulidi.”

MAMA ASHANGAA
Naye mama mzazi wa mtoto huyo, Amina Said alijitetea kuwa anashangaa watu kugeuza suala hilo kuwa ‘mjadala wa kitaifa’ wakati ni jambo la kawaida.

DINI INARUHUSU?
Ili kusikia kauli ya viongozi wa dini  kuhusiana na tukio hilo, Ijumaa lilizungumza na ustadhi wa madrasa ya Alhasaniyyah, Sheikh Thenei Jaafar ambapo alikiri kusononeshwa na kulaani vikali tukio hilo.

Denti anaswa gesti :YADAIWA ALIKUWA AKIUZA MWILI..




DENTI mmoja aliyefahamika kwa jina la Rehema mwenye umri wa miaka 15, hivi karibuni alinaswa gesti akidaiwa kufanya biashara haramu ya ukahaba.

Rehema alikamatwa katika gesti moja iliyopo maeneo ya Buguruni Malapa jijini Dar kufuatia operesheni iliyoendeshwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum na baadae kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Sokoine Drive kwa ajili ya kusomewa mashitaka.

Baada ya kufikishwa mahakamani hapo, Mwendesha Mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi alisema binti huyo hawezi kufunguliwa mashitaka kwenye mahakama hiyo isipokuwa anatakiwa kupelekwa kwenye mahakama ya watoto iliyopo Kisutu jijini.

Hata hivyo, baadae binti huyo aliyekuwa amevaa kichangu aliachiwa huru na alipozungumza na mwandishi wetu alidai kuwa, akiwa kwa wazazi wake huko Mwanga mkoani Kilimanjaro alichukuliwa na mwanamke mmoja aliyemtaja kwa jina la Vero kwa lengo la kuja kumtafutia kazi.

“Baada ya kufika Dar, sikutafutiwa hiyo kazi matokeo yake niliwekwa kwenye gesti iliyopo Buguruni Malapa na kufanyishwa ukahaba,” alisema binti huyo.
Akaongeza kuwa, kutokana na mazingira magumu anayoishi akipatikana mtu wa kumsafirisha hadi kwao, atashukuru.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...