Saturday, April 21, 2012

JE, KANUMBA ALIKUWA NI FREEMASON?!?
MENGI yamesemwa na yanaendelea kusemwa kwamba, mpaka kifo chake, Marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ alikuwa mwanachama wa imani ya Freemason (wajenzi huru) ambayo inashika kasi katika nchi za Kiafrika, lakini mama wa marehemu, Flora Mtegoa ametoa tamko juu ya tuhuma hizo za mwanaye.

                     
Akizungumza na waandishi wetu hivi karibuni nyumbani kwa marehemu Kanumba, maeneo ya Vatican City Hotel, Sinza jijini Dar, mama Kanumba alisema amesikia kuwa mwanaye alikuwa muumini wa imani hiyo yenye utata duniani.


Lakini akasema: “Namjua Kanumba, alikuwa mwanangu, mambo yake mengi nilikuwa nayajua maana tulikuwa tunaishi kama marafiki, habari hizo si za kweli.
“Watu wanasema sana, sijui wanatumia vigezo gani? Mwanangu alikuwa muumini mzuri sana wa Kanisa la African Inland Church (AIC), sasa huo u-Freemason aliuchukulia wapi?”

 
Akizidi kumimina maneno kwenye kalamu za waandishi wetu, mama Kanumba alisema kuwa kama ni suala la picha ambazo watu wanasema alipiga akiwa na mapozi ya imani hiyo, ni kwa kutokujua lakini si kweli kwamba alikuwa muumini wa jamii hiyo.

“Huo ni uzushi uliopitiliza,” alisema mama Kanumba.VIGEZO VYA WATU MITAANI
Wengi mitaani wamekuwa wakisema baadhi ya picha za marehemu Kanumba zilionesha viashiria vya kuwa mfuasi wa imani hiyo ambayo mpaka sasa Watanzania wengi hawaijui vizuri.


KIGEZO CHA PICHA
Zipo baadhi ya picha ambazo marehemu Kanumba anaonekana akiashiria alama za Freemason. Mfano, kuna picha ambayo mkono wake wa kulia ameweka vidole mfano wa pembe za mbuzi.

 Aidha, kuna picha marehemu amevaa tisheti nyeusi yenye picha kubwa ya fuvu la binadamu linalodaiwa kuwa miongoni mwa nembo za Freemason. Picha nyingine marehemu amevaa cheni yenye kidani ambacho kinasadikiwa ni utambulisho wa u-Freemason.

SUTI YA MAZISHI
Miongoni mwa magumzo yaliyotikisa siku ya kuuaga mwili wake ni suti nyeusi aliyovalishwa ambapo upande wa kushoto wa koti kuna nembo inayotafsiriwa ni ya Freemason.


Waandishi wetu waliwasiliana na mama wa marehemu na kumuuliza nani aliyemvisha koti hilo, yeye alijibu kwa kifupi:
“Sijui ni nani?”

KASI YA MAFANIKIO
Kigezo kingine ambacho baadhi ya watu wamekuwa wakikiamini kwamba marehemu alikuwa muumini wa dini hiyo ni kasi ya mafanikio yake.


Hapa Kanumba akiwa na Land Cruiser Lexus V8 mpya, aliyoinunua October mwaka jana inayogharimu millioni 78 million kabla ya kifo chake...     
Wengi wanasema kuwa marehemu Kanumba alikuwa mcheza filamu kama wengine, wakiwatolea mfano akina JB, Rich, Frank, Pastor Muyamba, Claud, Dk. Cheni na wengineo, lakini yeye kasi ya maendeleo ilikuwa kubwa zaidi ukilinganisha nao.

Kwa sababu hiyo, baadhi ya watu wakasema kuwa wamesikia mtu anapokuwa Freemason anawezeshwa kwenye shughuli zake kwa kuwa na bahati ya kutajirika.

MVUTO NAO WATAJWA
Baadhi ya watu wamekuwa wakitaja mvuto aliokuwa nao marehemu kwamba nao ni dalili tosha kuwa alikuwa kwenye imani hiyo.

 Wengi waliodai wana elimu kuhusu Freemason walisema kuwa, mara nyingi mwanachama wao hupoteza maisha wakati nyota yake ikiwa inawaka sana.Walitoa mfano wa marehemu Pepe Kalle, kwamba alipotoa albamu ya Cocktail aliwika sana na ndipo alipoaga dunia ghafla.

KANUMBA NA MASTAA WENGINE
Bado wengi wanazidi kuamini kifo cha ghafla cha Kanumba kinafanana na cha maarufu wengine duniani, marehemu Michael Jackson ‘The Jacko’, Whitney Houston na Madilu System ambao pia walihusishwa na u-Freemason. 

RAMSEY NOAH ANYOOSHEWA KIDOLE
Watu hao wanaopepeta huko mitaani kuwa marehemu Kanumba alikuwa muumini wa imani hiyo walizidi kuibua mapya ambapo wanaamini nyota wa filamu za Nollywood (Nigeria), Ramsey Noah naye ni mwanachama wa dini hiyo.

Wakadai mcheza filamu huyo alikuja Bongo na kucheza na Kanumba Filamu ya Devil’s Kingdom ambayo sehemu kubwa ya stori ni maisha ya imani ya Freemason.
 “Mimi nina wasiwasi na Noah (Ramsey), yule jamaa nasikiasikia naye ni muumini, sasa alikuja hapa kwetu (Tanzania) akacheza na marehemu filamu ya Devil’s Kingdom, huenda alimuingiza mwenzake kwenye imani hii,” alisema Rukia, mkazi wa Ubungo Kibangu jijini Dar.


Ili kunogesha habari hizo, ilidaiwa kuwa baadhi ya waigizaji wa filamu hiyo akiwemo Ramsey mwenyewe walipatwa na masahibu ambapo ukiacha Kanumba aliyefariki, staa huyo wa Nigeria alipata ajali huku Kajala Masanja akisota Segerea hivyo inawezekana walibumburua siri za Freemason kupitia Devil’s Kingdom, jambo ambalo waumini wa imani hiyo hawakulipenda.

Hawa ni viongozi wa mbalimbali wanaodaiwa kuwa ni freemason, na hiyo ni Alama ya Pyramid(inaheshimiwa na sana na Freemason)
 
 

The Great naye mh...!! Bonge la Pyramid arif
 
Haya sasa Collin Powel naye anadaiwa kuwa ni freemason, na hapo kwenye nyekunfndu ndo alama yenyewe


mh.....Ze Great naye alikuwemo?


KUTOKA KWA MHARIRI
Hakuna muda maalumu ambao mtu amepangiwa kupata utajiri, umaarufu au ushawishi hivyo sisi tumejaribu kuwasilisha kile kinachosemwa mitaani ambapo tunaamini mama mzazi wa marehemu Kanumba amemaliza utata hivyo mjadala huo umefungwa rasmi.

6 comments:

 1. FREE MASON NI UMOJA KAMA KILIVYO KIKUNDI CHA AKINAMAMA WA KIJIJI CHA MTIMWEMA, KWANI KAWAZUIA MISWE NA IMANI YENU? KUFANIKIWA NI JITIHADA ZA KUFANYA KAZI KWA BIDII........NANI ASIYEELEWA KANUMBA KATOKA WAPI?,,,,,,,,,,,,,,KWANINI MLITAKA AISHI MAISHA MAREFU? LAZIMA KILA MTU AWE NA PLAN YA MAISHA YAKE, PANGA UNATAKA UISHI MIAKA 70 ILI UFANYE NINI, SIYO KULA NA KULALA TU,,,,,,,,,,,IF ALIWEZA KUACHIEVE KATIKA UMRI MDOGO NI HARD WORKING, SASA KAMA YEYE ALIKUWA NI FREEMASON NDO AKAACHIEVE MAISHA,,,,,,,,,NINYI AMBAO NI WA MUNGU NANI KAWAZUIA KUACHIEVE? AU MUNGU WENU HANA UWEZO HUO?

  ReplyDelete
 2. +kweli mnachekesha sasa hapo kanumba ameshika tumbo pia ni alama ya u free mason!#@??? heheheheheheheheheheeeee wonders will never cease. huyu kaka alikuwa ni hardworking na mzungu alisema hard work pays na mapozi mengine mtu akipiga picha huwa anayabuni mwenyewe,sio eti kwasababu ya imani. wale mnasema kwamba alifanikiwa kwa haraka, tumieni common sense, hata nyie mkifanya kazi kwa kujituma lazima mtafanikiwa tu. This guy alikua na kipaji cha ku act na alikua serious na kazi yake lakini most of the Tanzanians wako lazy na hampendi kujituma ndo maaana mtaendelea kumfikiria kila anayefanikiwa ni freemasons. NOTHING COMES ON A SILVER PLATE YOU HAVE TO WORK FOR IT, KANUMBA WAS AMBITIOUS AND HARD WORKING, VERY CREATIVE IN HIS WORKS AND THAT'S WHY HE MADE IT IN LIFE. FREE MASON'S WANAWEZA KUKUPA HELA LAKINI SIO AKILI SASA WEWE UNAEDHANI KANUMBA ALIKUA MEMBER ANGALIA MIKANDA YAKE UNIAMBIE KAMA KUNAHATA MOJA ALIYE ACT UTUMBO, KADRI ALIVYOKUA ANAENDELEA KUPANDA NDIVYO ALIKUA ANATOA VITU VYA UKWELI. SASA NYIE ENDELEENI KULALA WENZIO WAKIJITUMA MNASEMA NI FREE MASONS, :-) EMPTY MINDS ARE DEVILS WORKSHOP, NO WONDER YOU HAVE SUCH SATANIC THOTS!!!!

  ReplyDelete
 3. maisha ni malengo na mipango watanzania wengi hatuendelei kwa sababu tuna uwezo hafifu wa kufikili na hii yote ni kuendekeza majungu. NA LINGINE NASEMA KWA HELUFI KUBWA WENGI NI WAFWATA MKUMBO NA WENGI WASEMAJI HUO UVUMI NI MASIKINI NA HAWANA KAZI MAALUM

  ReplyDelete
  Replies
  1. kweli mkuu hapo umenena kwa maneno hayo bila shaka wewe ni msomi na nimependa usemi wako mana mtu ambaye yuko bize na mambo yake hawezi kufuatilia pumba lyk dat BY MBOMBI AU WA MPWAPWAAAAAAAAAAAA

   Delete
 4. ni kawaida tuh hata kama alikuwemo pia na ww humo.

  ReplyDelete
 5. Hisia za watu huja baadae naamini mamake mzazi

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...