Wednesday, April 11, 2012

KANUMBA; MASHARTI MANNE ALIYOMWEKEA LULU ILI KULINDA PENZI LAO



                                     Steven Charles Kanumba.

                                 Elizabeth Michael ‘Lulu’.
BADO taifa linaombeleza kifo cha msanii nyota wa filamu za Bongo, Steven Charles Kanumba kilichotokea Aprili 7 mwaka huu nyumbani kwake, Sinza, Dar es Salaam.

Kifo cha msanii huyo kinamhusisha msanii nyota wa kike wa tasnia hiyo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye anasemekana aligombana naye kwa mambo ya mapenzi na kumsukuma.

Lulu alishikiliwa na polisi wa kituo cha Oysterbay cha jijini Dar es Salaam kwa mahojiano zaidi kufuatia kifo cha mpenzi wake huyo.

Hapo ndipo kwenye habari! Kwamba, kumbe marehemu Kanumba na Lulu walikuwa wapenzi! Ni vigumu kwa watu kuamini au kukubali, lakini ukweli unabaki kuwa huo.

Baada ya taarifa hizo, timu ya hot pot iliingia kazini ili kuchunguza siri hiyo nzito iliyodumu kwa takribani zaidi ya miezi sita.

MWANZO WA MAPENZI
Kwa mujibu wa watu wa karibu na marehemu Kanumba ambao walifunguka baada ya kifo huku wakiomba kusitiriwa kwa majina yao, wawili hao walianza uhusiano wakiwa katika safari moja ya sanaa mjini Moshi, Kilimanjaro. Safari hiyo ilihusisha kundi zima la Bongo Movie Club.

Kanumba ndiye aliyemtongoza Lulu na kukubaliwa na kuanzia hapo uhusiano wao ulianza rasmi. Lulu alianza kwenda nyumbani kwa Kanumba bila kipingamizi.

Majirani wa Kanumba wanakiri kuwa, mara kadhaa Lulu alikuwa akifika nyumbani hapo na ilifika wakati walikuwa wakipika na kupakua kama mke na mume.

MPANGO WA KANUMBA
Kwa mujibu wa habari hizo, marehemu kumtaka Lulu kimapenzi hakukuwa kwa ajili ya kujifurahisha nafsi bali kumuoa kwa ndoa na kuwa mke na mume.

“Lakini nataka kusema jambo zuri, usidhanie Kanumba alimtaka Lulu ili kumtumia tu, hapana! Alipanga naye maisha, alishamtamkia kumuoa,” alisema mmoja wa watoa taarifa.


UTAMBULISHO ULISHAANZA
Uchunguzi wa kina uliofanywa ulibaini pia kuwa, Kanumba alishaanza hatua ya awali ya maandalizi ya uchumba wao kwa kumpeleka Lulu kwa watu wake wa karibu na kumtambulisha.
Mtu ambaye kuna uhakika alishakutanishwa na Lulu ni msanii na mama mlezi wa wasanii Bongo, Husna Poshi ‘Dotnata’.

Inadaiwa kuwa, Kanumba alifunga safari na Lulu hadi nyumbani kwa Dotnata, Ubungo ya Riverside, Dar ambapo aliweka wazi uhusiano wake na msanii huyo na mipango ya kumuoa.

Habari za ndani zinadai kuwa Dotnata, mbali na kushtuka alimuuliza Lulu kama atatulia baada ya kuwa na Kanumba kwa lengo la kufunga ndoa ambapo msanii huyo alisema ameshatulia.
Aidha, habari zinasema kuwa, Kanumba alimhakikishia Dotnata kuhusu uhusiano wake na Lulu huku akisisitiza si wa kuchezeana.

HOT POT ilipata nafasi ya kuongea na Dotnata kuhusu madai hayo ambapo alikiri.
“Ni kweli, Kanumba aliwahi kumleta Lulu kwangu, akaniambia ameamua kuwa naye na mipango yao haikuwa mibaya kwani ilikuwa kuja kufunga ndoa. Nilimuuliza Lulu kama atatulia, akanijibu ameshatulia,” alisema Dotnata.

MASHARTI 4 ALIYOMWEKEA LULU ILI KULINDA PENZI LAO
Wakiwa ndani ya mapenzi motomoto, inadaiwa Kanumba alihisi penzi lao lingeweza kuvuja kabla ya muda aliotaka yeye, hivyo alimpa masharti manne Lulu ili kulilinda penzi hilo na mikono ya mapaparazi.

SHARTI NAMBARI MOJA
Lulu hakutakiwa kuzungumza na mwandishi yeyote wa habari kuhusu uhusiano wao na kama ni kusema, basi msemaji mkuu angekuwa Kanumba mwenyewe.

“Lulu aliambiwa kuwa asije akalianika penzi lao kwa watu, hasa waandishi wa habari. Na kama ni kuliweka wazi, basi mwenyewe ndiye angekuwa msemaji mkuu,” kilisema chanzo chetu.

SHARTI NAMBARI MBILI
Kanumba alimwambia Lulu anapokwenda na kutoka nyumbani kwake, alitakiwa kupanda taksi moja yenye ‘tinted’ inayopaki Kituo cha Vatican City Hotel, Sinza.
Kituo hicho kipo umbali wa mita kama thelathini kutoka nyumbani kwa marehemu.

SHARTI NAMBA TATU
Lulu alitakiwa kuachana na tabia za zamani, hasa za kupatikana kwenye vilabu vya usiku huku akiwa amelewa, sambamba na kuepuka vituko mbalimbali ambavyo vingeweza kumchafua katika jamii.
“Kama vile haitoshi, Lulu alipigwa marufuku kwenda kwenye vilabu vya usiku akiwa peke yake au na kampani mbaya.

“Pia akaambiwa aepuke vituko vya hapa na pale ambavyo vikinaswa na waandishi wa habari na kuandikwa vitamharibia sifa katika jamii,” kilisema chanzo.
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, kwa kutii sharti hilo ndiyo maana miezi ya hivi karibuni, Lulu alikauka kwenye vyombo vya habari.

SHARTI NAMBA NNE
Kanumba, kwa vile alishajua mipango ya baadaye na Lulu ni kuishi pamoja, alimtaka aachane na wanaume wake wa zamani na kuanza kurasa mpya na yeye, jambo ambalo Lulu alilitii.
Lakini katika yote, inaonekana marehemu alisahau kuweka masharti juu ya matumizi ya simu kwani ndiyo tatizo lililoibukia hapo na kusababisha kifo.

Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.  

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...