Friday, June 1, 2012

MKE WA HARTMAN AMLIWAZA MAMA KANUMBA



Muigizaji filamu, Mayasa Mrisho ‘Maya’, akimrekebisha nguo mke wa Hartman baada ya kuwasili nyumbani kwa mama Kanumba.

Gumzo la kuliwazana limekolea.

Ni vicheko mtupu.

Hartman akiwa na mkewe baada ya kufika nyumbani kwa marehemu Kanumba.

Mariam akiwa na muigizaji, Jenifer Kyaka ‘Odama’.

Mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ naye alikuwepo.

Mwandishi na mpiga picha wa mtandao huu, Shakoor Jongo (kulia) akiteta jambo na muigizaji Maya.

MKE wa mkurugenzi wa kampuni ya Hartman Production, Mariam Hartman, leo ametinga nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba Sinza Vatican jijini Dar kwa ajili ya kwenda kumpa pole mama wa muigizaji huyo Bi Flora Mutegoa. Mariam alikuwa akitokea nchini Uingereza ambapo anapoishi.
Akizungumza kwa niaba ya mkewe, Hartman Mbilinyi, ambaye aliongozana na mkewe mahali hapo alisema kuwa siku ya tukio la msiba wa Kanumba mkewe alikuwa Uingereza hivyo hakupata nafasi ya kuhudhuria msiba, ndipo alipopanga kuja nchini kwa ajili ya kutoa pole.
“Katika watu walioumia na msiba huu mke wangu ni mmojawapo kwani marehemu alikuwa mtu wake wa karibu sana,” alisema Hartman.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...