Thursday, September 1, 2011

BURUDANI ZA SIKUKUU YA EID EL FITR DAR

Mr. Guiness ambaye ni Costa Siboka, akionesha uso wa tabasamu wakati akipelekeshwa puta na mnenguaji wa Akudo, Nadine Esalaa (aliyeinama).

Mashabiki wa Akudo wakiserebuka.

Waislamu duniani kote, jana walisherehekea Sikukuu ya Eid El Fitr ambapo hapa nchini watu mbalimbali walijirusha viwanja vya starehe kuadhimisha sikukuu hiyo. Yafuatayo ni baadhi ya matukio yaliyonaswa na kamera yetu usiku wa kuamkia leo katika viwanja mbalimbali vya jijini la Dar es Salaam.

‘Prezdaa’ wa Bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ Christian Bella  (katikati) akiongoza kikosi chake katika makamuzi yaliyofanyika ufukwe wa Msasani Beach Club.

MASHAUZI CLASSIC YAFUNIKA TRAVERTINE
Mashauzi akipagawisha mashabiki.

Ni furaha tupu kwa mashabiki.

Shabiki aliyevamia jukwaa ili kuserebuka baada ya kupandwa na midadi.

Bendi ya Mashauzi Classic inayoongozwa na Aisha Makongo ‘Isha Mashauzi’ ilifunika ile mbaya katika onesho lililofanyika Hoteli ya Travertine.

                                 EXTRA BONGO YAPAGAWISHA MEEDA, SINZA
Mashabiki wa Extra Bongo wakimshangilia mmoja wa wanenguaji wa bendi hiyo.

Macho ya mashabiki hawa yakiwafuatilia wakata nyonga ukumbini.
Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, usiku wa kuamkia leo ilifanya makamuzi ndani ya ukumbi wa Meeda uliopo Sinza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...