Sunday, September 25, 2011

Ukahaba Dar...
Biashara haramu ya ngono ikihusisha watoto wadogo na wanafunzi imeshamiri nchini na inalijengea taifa picha ya aibu mbele ya jamii pana ya kimataifa, ze UTAMU Jumamosi lina ripoti kamili ya madanguro, gesti na hoteli maarufu zinazoendesha ‘unyambilisi’ huo jijini Dar es Salaam.
Uchunguzi wa blog hii umebaini kuwa, nyuma ya biashara hiyo kuna vigogo ambao wanajitajirisha kwa kuwauza watoto wa kike wa kati ya miaka 11 hadi 14 ambao wanaelezwa kuwa na soko zaidi ukilinganisha na wale wenye umri ulioyoyoma.
Kwa wiki kadhaa chumba chetu cha habari kimekuwa kikipokea ujumbe mfupi kutoka kwa watu walioomba hifadhi ya namba zao kuwa kuna wafadhili wa biashara hiyo ambao huwachukua wasichana wadogo vijijini kisha kuwamwaga jijini Dar kwa ahadi ya kuwatoa kimaisha, lakini huishia kuwafanyisha biashara hiyo haramu inayostahili kupingwa kwa nguvu zote.
Ilifahamika pia kuwa, kuna baadhi ya watu huwashawishi wanafunzi wa kike jijini Dar ambao huaga kwao kuwa wanakwenda shuleni, lakini huishia kwenye madanguro, gesti na hoteli maarufu kwa ajili ya kuuza miili, hivyo kuwafanya wazazi kuwa na matumbo joto wanapowabaini.
Ze utamu Jumamosi lilifanya mahojiano na wasichana hao wadogo wanaojiuza sehemu mbalimbali jijini Dar ambapo walikuwa na haya ya kusema:
WA KWAZA (SINZA): “Huwa natoroka shule na kwenda kujiuza kwa wanaume ili kujikimu kimaisha. Fedha ninayopewa ya matumizi huwa haitoshi.”
WA PILI (BUGURUNI): “Kawaida nafanya mapenzi na wanaume 5 hadi 6 kwa usiku mmoja.
WA TATU (KINONDONI): “Malipo kwa tendo moja ni 10,000. Saba za tajiri, tatu za kwangu.
WA NNE (TEMEKE): “Kazi ni ngumu lakini kwa sababu ni shida, nafanya.”
RIPOTI YA BBC
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC iliyoibua mjadala hivi karibuni na kuwaweka watu presha juu, watoto wanaojihusisha na biashara hiyo walieleza jinsi walivyodanganywa kuzamia jijini Dar kufanya kazi nzuri za kuwapatia mkate wao wa siku, lakini wakaishia kwenye biashara ya ukahaba.
Watoto hao walieleza kuwa, kutokana na ugumu wa maisha vijijini walipata matumaini kuwa jijini kuna matunda, lakini walipofika wakawa wakifugwa kama watumwa kwa kazi moja tu, kuuzwa kwa wanaume wapenda ngono za rejareja.
Katika mjadala huo ulioendeshwa kwa siku tatu, vitoto hivyo vibichi viliweka wazi kuwa wanapochukuliwa na wanaume hulipwa Sh. 50,000 lakini huambulia Sh. 10,000 kwani fedha nyingine huchukuliwa na tajiri.
MMILIKI WA DANGURO
ALIRITHI KWA BIBI YAKE
Kwa mujibu wa mmoja wa wamiliki wa madanguro hayo machafu (jina tunalo),  biashara hiyo alirithishwa na bibi yake kwa hiyo haoni hatari kwa sababu hakusoma hivyo kazi hiyo anaiona ni halali.
Bila aibu, mwanamke huyo mchafuzi aliendelea kubwabwaja kuwa ana ‘kocha’ maalumu wa kuwafunza watoto hao namna ya kujituma wanapokuwa ‘kazini’ na wanaume.
GESTI, HOTELI NA MADANGURO
HATARI NI HAYA
Uchunguzi uliofanywa na mtandao wa Jamii Forums ulibaini kuwepo kwa gesti, hoteli na madanguro hatari sehemu tofauti jijini Dar.
Ilibainika kuwa sehemu hizo ni pamoja na hoteli maarufu zilizopo Sinza Madukani, Sinza-Mori, Sinza Afrikasana,  Ubungo External, Makuburi, Mbezi, Majumba Sita-Ukonga, Uwanja wa Taifa, Saba Saba, Kawe, Kunduchi, Buguruni na Magomeni.
Pia, kuna hoteli maarufu za nyota tatu katikati ya jiji maeneo ya Posta na Kariakoo katika viunga vya Mnazi Mmoja zinazofanya biashara hiyo hasa kwa wanandoa wanaofanya kazi maeneo hayo ‘wanaocheza nje kapu’ kwenye ndoa zao.
WAZIRI SOFIA SIMBA ANASEMAJE?
Akizungumzia ishu hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sofia Simba (pichani), mbali na kukiri kuwepo kwa hatari hiyo, alidai kuwa wizara yake inajitahidi kutekeleza na kulinda maslahi ya watoto ingawa hakueleza jinsi wanavyokabiliana nayo.
KUTOKA ZE UTAMU BLOG
Ukweli ni kwamba hali ni mbaya kupita maelezo.
Tunatoa wito kwa idara zote zinazohusika kunusuru kizazi cha kesho kwa kuwaepusha na mateso wanayoyapata huku janga la ukimwi likichukua kasi. Pia, tunaiomba jamii kupinga kwa nguvu zote kwa kuripoti kwenye vyombo husika uwepo wa biashara hiyo haramu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...