Friday, September 23, 2011

Mastaa wageuza vyumba vyao madanguro...


Imegundulika kuwa, baadhi ya mastaa micharuko Bongo wanaoishi peke yao wamekuwa wakisababisha usumbufu mkubwa kwa wapangaji wenzao kufuatia kugeuza vyumba vyao kuwa madanguro.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, mastaa wanaofanya hivyo ni wale wanaobadili wanaume kila kukicha huku wengine wakigeuza miili yao vitega uchumi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya watu wanaoishi na mastaa kwenye nyumba zao walisema kuwa, mbali na kufanya vyumba vyao gesti, wapo wanaovigeuza madanguro kwani huishi zaidi ya mmoja huku wanaume wakipishana usiku na mchana.

“Hapa kwenye nyumba yetu tunaishi na msanii mmoja wa filamu anaitwa Jennifer Paulo, mara nyingi hakai hapa lakini ana marafiki zake ambao muda mwingi ndiyo wanashinda hapa.

“Wale wadada nadhani ni machangudoa kwani wanaume wamekuwa wakipishana kila saa, sasa imekuwa ni kero kwetu tunaoshinda nao,” alisema Jamila Kigaula wa Manzese, Dar es Salaam.

Utamu ilimtafuta Jennifer kwa njia ya simu, alipopatikana alisema: “Wale ni marafiki zangu lakini hilo la kukigeuza chumba changu danguro au gesti ndo kwanza nalisikia kwako.”

Naye Mama Suzan wa Kinondoni Mkwajuni alisema kuwa, katika nyumba yake alimpangisha msanii mmoja wa muziki (jina tunalihifadhi) lakini anajuta kwani msichana huyo kila siku anaingia na mwanaume mpya.

“Najuta kumpangisha, mchana hashindi hapa lakini kila siku anarudi na mwanaume mwingine hadi watu wanalalamika kuwa nimepangisha changudoa kwenye nyumba yangu,” alisema mama huyo.

Katika kujua ukweli wa habari hizi, utamu ilizungumza na baadhi ya mastaa wanaoishi kwenye mageto peke yao na hivi ndivyo walivyofunguka kuhusu skendo hiyo:

BADRA: Mimi kweli nina kwangu na mara moja moja wanakuja mashoga zangu nalala nao ila kwa kweli hilo la kuingiza wanaume pale kwangu halina nafasi, najiheshimu kuliko wanavyonifikiria.

MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’: Ni uamuzi tu, mtu anaweza kujiamulia kwenda kulala kwa shoga yake anayemtaka au unapanga chumba na unaita mashoga zako unakaa nao kama ninavyofanya mimi, hatujali hayo yanayosemwa.

SNURA MUSHI: Mimi hapa naishi na mama yangu mdogo na sionagi tatizo mashoga zangu kuja kuishi hapa kwani si wanakuja kulala tu?

Kama ni wanaume zao, wanaenda kukutana nao huko huko kisha asubuhi au usiku wanarudi.

REHEMA FABIAN: Ni jambo tu la kawaida mtu kuishi na mashoga zake kwani ni suala la kupeana kampani.

Kuhusu kuingia ndani na mwanaume wake ni sawa tu, akija naye wanafanya mambo yao sebuleni na mimi akija wangu naingia naye chumbani.
SKYNER ALLY ‘SKAINA’:

Hiyo ni tabia mbaya mtu kukaribishwa sehemu kisha ukawa unaleta mabwana zako, unampa sifa mbaya mwenye chumba chake mwisho wa siku wewe ukiondoka mwenzio nyuma unamuachia matatizo.
ZUENA MOHAMMED ‘SHILOLE’:

Mi’ nilikuwa nikiishi na Flora Mvungi lakini kila mtu akitaka kufanya mambo yake anaondoka anaenda hukooo, tunakutana baadaye au asubuhi...


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...