Thursday, September 22, 2011

JOKATE AJIVUNJIA HESHIMA...


Mrembo anayesifika kwa kujiheshimu kuliko mamisi wengi waliopita Miss Tanzania, Jokate Mwegelo, amejivunjia heshima kwa kuvaa kivazi tata kilichomuonesha maeneo yasiyofaa kuangaliwa.

Jokate aliyeshika nafasi ya pili Miss Tanzania 2006, alitinga Mlimani City hivi karibuni kwenye Fainali za Miss Tanzania 2011 lakini alipokaa, mambo yakawa hadharani.

Gauni alilovaa, lilikuwa linasaidiwa na kamba ili kumsitiri kidogo lakini lilifunuka sehemu kubwa, hivyo kuacha wazi maungo yake.

UTAMU inayo picha inayomuonesha Jokate akijitahidi kulikusanya gauni lake na kujifunika ili maeneo ya faragha yasizidi kukaa wazi, ingawa ilishindikana, hivyo sehemu nyingine ikabaki ikichungulia nje.

Baadhi ya watu waliomuona Jokate, walioneshwa kushangazwa kabla ya mmoja wa waratibu wa Miss Tanzania ngazi ya kanda, Dar es Salaam (jina tunalo) kusema: “Jokate anaanza kupoteza uelekeo, uvaaji huu unamvunjia heshima.”

Mwandishi alimfuatilia Jokate kuzungumza naye lakini ilikuwa ngumu kutokana na mrembo huyo kuwa ‘bize’ baada ya matokeo yaliyompa ushindi Salha Israel kutangazwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...