Thursday, September 29, 2011

Kanumba, Internet, Sharapova waumbuka...



ILIKUWA ni bonge la ‘pati’, sherehe au tafrija kama siyo burudani ndani ya Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam wakati Bendi ya African Stars ‘International Twanga Pepeta’ ilipokuwa ikiburudisha katika Usiku wa Mastaa.

Katika burudani hiyo, iliyofanyika Jumamosi iliyopita wasanii Steven Kanumba (pichani) na wakatanyonga wa bendi hiyo, Lilian Tungaraza ‘Internet’ na Asha Said ‘Sharapova’ waliumbuka baada ya shampeni kuwagomea kufunguka.

Ilichukua muda mrefu shampeni za mastaa hao kuweza kufunguka huku umati wa watu waliohudhuria usiku huo ukiwa umeshakata tamaa.

“Hivi vitu vinataka mazoea, inaonekana Kanumba, Internet na Sharapova hawana uzoefu wa kufungua shampeni,” alisema staa mmoja usiku huo.






Naye mtangazaji wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kinachorushwa na Redio ya Times ya jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida wa G’ aliweza ‘kuharibu vibaya vibaya’ baada ya kufungua shampeni yake kwa mbwembwe na kuufanya umati umshangilie.

Mkurugenzi wa Twanga, Asha Baraka aliwashukuru mastaa wote waliohudhuria na kuwataka kuwepo kwa wingi siku ya uzinduzi wa albamu ya 11 ya bendi yake katika Viwanja vya Leaders usiku wa Septemba 6 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...