Friday, September 30, 2011

Kanumba, Ray: Hatumtaki Aunt....


Masupastaa wawili wakubwa katika tasnia ya filamu Bongo, Steven Charles Kanumba na Vincent Kigosi ‘Ray’ wanadaiwa kuchochea kumpiga chini mcheza sinema ‘seksi’, Aunt Ezekiel Grayson kutumika katika muvi zao kwa mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha ZE UTAMU ndani ya sanaa hiyo, kuna kikao kilichokaa katika Viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar kikiwahusisha waigizaji hao kilichofikia uamuzi huo huku sababu ikimumung’uywa.

ZE UTAMU lilipododosa ‘sosi’ ya ishu hiyo ya kufungiwa kwa staa huyo namba moja kwa mauzo ya filamu, chanzo hakikuwa tayari kuweka bayana mkanda kamili.

“Uamuzi uliofikiwa kwa mara ya kwanza ulikuwa ni kumfungia kwa mwaka mmoja, lakini ghafla waliibuka baadhi ya wasanii wakasema kama ana kosa asamehewe au afungiwe japo miezi mitatu.

“Wadau walipoanza kugawanyika, muafaka haukufikiwa lakini suala la kufungiwa likabaki palepale na wasamabazaji wa filamu wa Steps Entertainment wakapelekewa taarifa,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Baada ya kuzitia kibindoni habari hizo, ‘vuvuzela’ wa UTAMU alimvutia waya Afisa Uhusiano wa Steps Entertainment, Seles Mapunda ambapo alikiri kuwepo kwa ishu hiyo, lakini akabainisha kuwa anachojua yeye siyo kwa mwaka mmoja bali ni miezi mitatu.

Walipotafutwa Kanumba na Ray kwa nyakati tofauti hawakuwa tayari kutoa ushirikiano.

Kwa upande wake Aunt alisema hajui chochote juu ya yeye kufungiwa. Kwa mujibu wa mashabiki wa filamu za Kibongo waliozungumza na gazeti hili walikuwa na haya ya kusema:

“Duh makubwa! Yaani ina maana Aunt hatutamuona tena kideoni? Inabidi Kanumba Ray wafikirie upya uamuzi wao kwani Aunt ni jembe kwenye filamu.”

1 comment:

  1. dah dada aunt byebye nahis itakua kingono zaid

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...