Friday, September 23, 2011

Kigogo elimu anaswa gest...

Tukio hilo la kuchafua sifa ya ndoa, lilijiri hivi karibuni mjini Morogoro ambako Rose aliaga kwa mumewe anakwenda kikazi.
Kapu la habari lililosheheni picha za video na mnato liliwasilishwa mezani pa gazeti hili hivi karibuni na mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sarah huku maelezo yakimtuhumu Rose kujivinjari na mumewe katika faragha haramu.


SAKATA LILIVYOKUWA
Simulizi ya kwanza kusikilizwa  kutoka kwa mtoa habari wetu ilieleza kwamba, mtumishi huyo wa wizara ambaye amejazia mwili alidaiwa kuingilia ndoa ya mtu kwa kutumia safari zake za kikazi kula nyama ya ulimi na mume wa mtu huyo aliyetajwa kwa jina moja la Kesi ambaye hatimaye alinaswa naye.

 “Kuna watu waliniambia kuwa, Kesi ambaye ni mume wangu anatembea na mwanamke huyo, nikaanza kufuatilia hatua kwa hatua kwa kuwatumia watu wakiwemo watumishi wa hoteli aliyofikia Rose na mume wangu.

“Sikupenda kuwaingilia chumbani na kuwaharibia starehe zao, nilichotaka mimi ni ushahidi, nilitumia ujanja wangu kupenyeza kamera nikapata picha,” alisema Sarah huku akifungua kompyuta mpakato yake (laptop) na kuonesha tukio zima.


ROSE NAYE NI MKE WA MTU
Baada ya kujionea picha hizo za aibu, mwandishi wetu alifungua ukurasa wa tafakuri ambapo alimtuhumu mume wa mwanamke huyo kuwa ndiye chanzo cha  tatizo kwa kusema huenda alimficha Rose juu ya ndoa yake.

“Mbona na yeye Rose ni mke wa Kanali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (jina kapuni), sasa unaposema mume wangu ana tatizo nashindwa kuelewa unamaanisha nini?” alihoji Sarah wakati akisawazisha hali ya mwandishi kutaka kumtetea kigogo huo.

USAWA WA HABARI
Katika kuzingatia weredi wa habari, dawati la blog hii lililazimika kumtafuta kwa njia ya simu ya kiganjani mtumishi huyo wa wizara ya elimu ili athibitishe tuhuma za kudandia mume wa mtu huku yeye naye akiwa na kiapo cha ndoa. Alipopatikana mahojiano yalikuwa hivi:

Mwandishi: Habari yako dada Rose?
Rose: Nzuri, naongea na nani?
Mwandishi: Naitwa (mumunya jina kwa usalama).

Rose: Ndiyo, unasemaje?
Mwandishi: Aaa, hapa kuna tuhuma zako kwamba unatembea na mume wa mtu na kwamba hivi karibuni ulikuwa naye ndani ya gesti moja mjini Morogoro, lakini pia zipo picha za video na mnato zikionesha mambo machafu mliyoyafanya huko, sijui unajua chochote kuhusu hili?
Rose: We uko wapi, …kama ni ofisini nakuja sasa hivi kuziona hizo picha, nitakujibu nikifika.




ROSE NDANI YA UTAMU
Pamoja na foleni za Jiji la Dar es Salaam, dakika 27 baada ya Rose kuahidi kutinga katika ofisi za ZE UTAMU, alipiga hodi mapokezi akiwa na mwanamume aliyemtambulisha kuwa ni mumewe.

Bila kuchelewa, wawili hao wakiwa na sura ya kama wanaosema ‘msitubambikie uongo WA BLOG yenu’ waliomba kuziona picha, jambo ambalo liliwapa wakati mgumu wahariri kukubali zoezi hilo lifanyike mbele ya mwanaume huyo.

“Sikiliza kijana, huyu ni mke wangu, sasa unataka kuficha nini, umempigia simu, kaniambia, sisi tukakubaliana tuje wote kama mwili mmoja, sasa wewe unakataa nini…au ulikuwa na mambo yako?” alihoji kwa ukali mume wa mwanamke huyo.

WAKATI WA KUONA PICHA
Baada ya timu ya dawati la ze utamu kuzidiwa nguvu lilikubaliana na ombi la wanandoa hao kuona picha hizo kwa pamoja, hivyo walipelekwa kwenye kompyuta na kuanza kufunguliwa kifurushi kimoja baada ya kingine cha sinema yote.

“Mume wangu tulikuwa tumekaa tu hapa, huyu kaka alikuja kunitembelea chumbani, umeona nimevua nguo?” Rose alijitetea kwa mumewe baada ya kifurushi cha kwanza kufunguliwa na kuwaonesha wakiwa wamekaa kitandani na jamaa.

Hata hivyo, mwanamke huyo alibadilisha maelezo baada ya kufunguliwa video ya pili iliyowaonesha wakiwa katika ‘kikilikakala’ za watu wazima walizokuwa wakifanya gesti siku hiyo ambapo Rose alijikuta akisema: “Mume wangu huyu kaka alinilazimisha mimi nilikuwa sitaki kabisa.”

Kauli hiyo ya mtumishi huyo wa umma mbele ya mumewe ilikuwa kama kutia nazi kwenye supu kwani kimsingi video iliwaonesha wawili hao wakishirikiana ipasavyo hali iliyomfanya mumewe ashushe pumzi na kusema kama wafanyavyo Wanaijeria kwenye filamu pale wanapohamaki:
“heee.”

Mpaka mwisho wa sinema hiyo yenye dakika chache lakini zenye ‘machungu’, wanandoa hao waliondoka wakiwa ‘wamelowa’ jasho mbendembende.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...