Thursday, September 8, 2011

Agnes: Kiuno changu kina milioni mbili

MWANADADA anayefanya freshi kwenye filamu ambaye pia ameuza nyago kwenye  video mbalimbali za muziki wa Bongo Fleva, Agnes Gerald amedai kuwa, kiuno chake amekiremba kwa cheni ya dhahabu ya gramu ishirini.

Agnes a.k.a Masogange aliyasema hayo hivi karibuni baada ya paparazi wetu kumuuliza juu ya picha za hivi karibuni alizozipiga ambapo moja ilimuonesha akiwa amekianika kiuno chake kikiwa kimezungukwa na ‘kamba’ ya gharama kubwa.

Alisema kuwa, kiuno ni sehemu muhimu sana katika mwili wake hivyo haoni hatari kutumia kiasi kikubwa cha fedha kukifanya kionekane bomba.

“Hiyo unayoona ni cheni ya dhahabu ambayo ni gramu 20, nimenunuliwa na mpenzi wangu. Hata hivyo, nakipenda sana kiuno changu, ndiyo maana siyo jambo la ajabu kutumia fedha nyingi kukifanya kiwe na mvuto,” alisema Agnes.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...