Thursday, September 22, 2011

Comedy ZONE

NDOA NDOANO

Mume na mke walikuwa wamebishana siku nzima kutokana na matatizo yao ya ndoa... So mwisho wa siku wakaamua kuchuniana.... Kesho yake yule jamaa alitakiwa asafiri na ndege ya alfajiri sana hivyo bila kuharibu utaratibu wa kumuongelesha mkewe akaamua kumuandikia note, "Naomba uniamshe sa kumi na nusu asubuhi..." Kabla hawajalala akamuwekea juu ya mto wake ili aone vizuri then ye akatangulia kulala ili awahi kuamka....

Kulipokuchwa, jamaa kushtuka na kucheki saa, ni saa mbili na nusu... Akapatwa na hasira sana kwa sababu ya kukosa ndege... Akaamua kuamka ili aweze kumuuliza viizuri kwanini hajamuamsha... Ile anainua kichwa kikaratasi kikadondoka... Akakifungu na kukuta kimeandikwa...
"AMKA, NI SAA KUMI NA NUSU..."

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...