Thursday, September 29, 2011

MLELA NA AUNTY...



MUIGIZAJI mwenye sauti ya kiume katika filamu za Kibongo, Yusuf Mlela ameiminyia mavumbini skendo inayomtafuna kwamba anatoka kimapenzi na msanii mwenzake, Aunt Ezekiel Grayson (pichani).
Akizungumza hivi karibuni jijini Dar, Mlela alisema kuwa, anawashangaa wazushi wanaoneza madai hayo lakini akasema anajua ni kutokana na jinsi wanavyogandana na msanii huyo kama kumbikumbi maeneo mbalimbali.
Aliongeza kuwa, licha ya kwamba Aunt ni msanii mwenzake lakini pia wameshibana ile mbaya, akaomba watu wasiwatafsiri vinginevyo.
“Unajua mimi na Aunt wote tunaishi kwa kutegemea sanaa, hicho ndiyo kitu kinachotufanya tuwe karibu, zaidi ya yote huwa tunakuwa kampani moja tunapokwenda disko au kwenye sherehe mbalimbali, ila kila mmoja ana mtu wake,” alisema Mlela.






Alipobanwa kuhusu kualikwa kwenye mashindano ya Miss Tanzania 2011 na kadi yao kuonekana kama ya Mr & Mrs huku wakiingia ukumbini hapo kama wanandoa, Mlela alijitetea:
“Watu wanaotualika kwenye sherehe zao ndiyo walitupa kadi moja. Hata siku ile ya Miss Tanzania tulipewa kadi ya mwaliko moja tu ikiwa na majina yetu, ndiyo maana ulituona vile.”
Mbali na Miss Tanzania 2011, katika harusi ya msanii mwenzao, Irene Uwoya iliyofungwa jijini Dar es Salaam mwaka 2009, wawili hao pia walikuwa beneti hali iliyoibua maswali kibao kwamba huwenda wawili hao ‘wanaduu’.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...