Sunday, September 25, 2011

TWANGA PEPETA, EXTRA BONGO ZARINDIMA DAR

 Sehemu ya watu waliofurika.

 Wadau waliokosa viti wakiwa wamesimama.

BENDI ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ usiku wa kuamkia leo imefanya onyesho maalum la kuwaburudisha mashabiki wake na mastaa mbalimbali katika Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam. Katika onyesho hilo bendi hiyo ilitangaza uzinduzi wa albam yake ya 11 utakaofanyika Novemba 6 mwaka huu. Yafuatayo ni baadhi ya baadhi ya matukio yaliyojiri kwenye onyesho hilo.

 Msanii wa filamu, Steven Kanumba ‘The Great’ akifungua shampeni kuwatakia afya njema waliohudhuria ukumbini.

 Mfanyabishara maarufu jijini Dar, Pius Ruta ‘Mzee wa Pamba’, amkimtunza mwanamuziki wa Twanga, Dogo Rama.

 Mashabiki wakisugua kisigino.    

Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ usiku wa kuamki leo imefanya makamuzi kwenye ukumbi wa Meeda uliopo Sinza jijini Dar es Salaam.
 Mnenguaji wa bendi hiyo, Mwantum Athuman (mwenye blauzi nyeupe) akiserebuka na mashabiki wa bendi hiyo.

Kutoka kushoto ni wanenguaji Aisha Madinda, Otilia Boniface na Mwantum Athuman wakikamua.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...