Mwanasayansi alikuwa akisafiri kwenye MV spice kutoka pemba kuelekea unguja, pembeni yake alikuwa amekaa na mpemba, baada ya ukimya akaamua kumuuliza yule mpemba aliyekaa naye maswali ya kizushi... "Hivi kijana umesoma kweli??
Mpembai: "Ahaaa, mie... Mie nmesomo soma mpaka darasa la sabah yakhe..."
Mwanasayansi: "Sawa, hivi unajua sociology, psychology, entomology, cytology au angalau hata criminology kidogo??"
Mpemba: "Sijui hata kimoja yakhe, kwani vipi..."
Mwanasayansi: "Kweli we ni mpuuzi sana na maisha yako yatazidi kuwa magumu sana na unakusa asilimia 90 ya kuishi vizuri..."
Yule mpemba ilimuuma sana, akaamua kunyamaza na kuendekea na safari... Baada ya muda ile boti ilianza kuzama, yule mpemba akamshtua yule mwana sayansi ambaye alikuwa ameanza kusinzia...
"Yaakhe, yakhe.... weye si wajifanya umesoma weye... Hivi ulifundishwa kuogeleaology au hata kujiokoaology??
Yule mwanasayansi akajibu "Hapana, kwani vipi..."
Mpemba akamwambia, "Yakhe, we lala tu, boti ndo hili lazama na leo ndo utazamaology na kufaology.... Samaki leo lazima wakutafuneology hayo machoology na ubongoology wako uliosomaology na kukupa majivunoology... Pole sana yakhe kwa kukosaology asilimia 100 ya kuishiology, kwaheri na ma-ology yako yakheeee!!!!"
No comments:
Post a Comment