Thursday, September 8, 2011

Shilole, Bonita watwangana



STAA katika tasnia ya filamu za Kibongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ (pichani), juzikati alizichapa kavukavu na mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Bonita..

Kisa cha ugomvi huo uliotokea Jumamosi iliyopita kimedaiwa kuwa ni Bonita ambaye anamiliki saluni inayohudhuriwa na mastaa wengi wa kike wa jijini Dar es Salaam kutuhumiwa na Shilole kutoa maneno ya umbeya.










Akizungumza na mavuvuzela, Shilole alisema kuwa tabia ya Bonita kutoa siri za mastaa wanaotengeneza nywele katika saluni yake inahitaji kukomeshwa na kwa kuanza aliamua kuonesha njia kwa mastaa wengine jinsi ya kumfunga mdomo mwanamke huyo.

Katika ugomvi huo ambao ulivuta umati wa watu, Shilole alimdunda Bonita hali iliyosababisha staa mwingine wa filamu,  Latifa Idabu‘Badra’ kuingilia kati na waamua.

“Amekuwa na tabia mbaya sana, sisi tunakwenda kwenye saluni yake ili  apate riziki, sasa mwenzetu tukiondoka anatuacha uchi, binafsi nimechoka ndiyo maana nimeamua kuchukua hatua hii ya kuja kumshikisha adabu,” alifunguka Shilole.

Kabla blog hili haijamsaka Bonita kutoa maelezo yake, mwanamke huyo alipiga simu kwa mavuvuzela wetu na kuanza kuwalaumu kwa kitendo chao cha kupiga picha.

 “Sikutegemea kama mnaweza kunisaliti, hata nyinyi mnaweza kuja kunipiga picha nikiwa napigwa! Kumbukeni damu ni nzito kuliko maji na ugomvi huu usitufanye tuvunje undugu wetu,” alisema Bonita akilalamika kwa nini  mavuvuzela hao walitinga eneo la tukio na kumfotoa picha.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...