Thursday, September 22, 2011

Wema, Diamond watibuana...


PENZI la Wema Abraham Sepetu na Naseeb Abdul ‘Diamond’ hivi karibuni liliingia dosari baada ya wawili hao kutibuana, Ijumaa Wikienda limetonywa.

Chanzo chetu makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa mastaa hao walifikia hatua hiyo baada ya kutokea mazingira ya kutoelewana kati yao hivyo kutoenda pamoja hata kwenye mashindano ya Vodacom Miss Tanzania 2001.

“Wema na Diamond walizinguana juzikati hadi kufikia hatua ya kutoenda pamoja kwenye shindano la Miss Tanzania, chanzo sijui lakini mwenyewe alisema hawako sawa,” kilisema chanzo hicho.





Katika kujua ukweli wa habari hii, mwandishi wetu alimtafuta Wema na alipopatikana alisema: “Siyo siri, kweli nilitibuana na Diamond, sisi ni binadamu, siyo malaika kwa hiyo kugombana kwetu ni kitu cha kawaida na hili linatokea kwa wapenzi wengi tu.”

Naye Diamond alisema: “Ni kweli tulipishana kauli na Wema kutokana na mapungufu ya kibinadamu lakini kwa sasa tumeweka mambo sawa na tunaendelea na mapenzi yetu kama kawaida.”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...