Tuesday, August 30, 2011

MACHANGU WALIA NJAA



Safari ya blog  hii kuwatembelea machangudoa wa jijini Dar es Salaam ilikamilika kwa kukusanya kilio chao kikubwa ambapo ilibainika wote wanalia hali ya ukame iliyopo sasa, mistari inayofuata inakupa ‘eibisii’.

Hivi karibuni, kikosi kamili cha wapiga picha wetu walitia timu sehemu mbalimbali za jiji ambazo makahaba wanatega wanaume lengo likiwa ni kujua wanachozungumza katika kipindi hiki cha mfungo.





Wengi walisema hali ni ngumu  kiasi cha kukatisha tamaa na mbaya zaidi, wengi wao wanapotoka majumbani usiku kuelekea kwenye ‘lindo’ hubeba nauli ya kuendea tu wakiamini watarudi na Bajaj baada ya kunasa wateja.

Prisca Makungu, kahaba anayepatikana maeneo ya Kinondoni, Dar alisema kuwa zamani alikuwa akikamata shilingi elfu 90 kwa wiki lakini kwa sasa siku saba zinakatika akiwa na shilingi elfu ishirini tu mkononi.





Anna Singano, ni kahaba Corner Bar, Sinza. Anasema kwa sasa anaweza kukata wiki moja bila kuweka kibindoni hata shilingi elfu 10, wakati mwingine anakopa nauli kwa madereva wa Bajaj wa eneo hilo ili aweze kurudi nyumbani kwake, Mabibo.

Isha Suzu, kahaba nje ya Ukumbi wa Sun Cirro, uliopo Shekilango, Ubungo jijini Dar anasema hali ni mbaya. Anafikiria kutafuta kazi za ndani ‘uhausigeli’ ili aweze kujikwamua kimaisha.





Mwajabu Idi, anauza mwili maeneo ya Keys Hotel, Mnazi Mmoja, Dar. Anasema katika kipindi hiki kigumu kwa biashara amelazimika kuchagua siku za kwenda ‘kazini’.

“Hali mbaya jamani. Mimi nimeamua kuchagua siku za kuja, kuanzia Ijumaa mpaka Jumapili nakuja, baada ya hapo nalala tu kwani hata nikija sipati ‘pesa’ za kunitosheleza kama zamani.

Katika hali ya kustaajabisha, kahaba mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Rehema alianika kwamba, katika kipindi hiki cha ukame wa wanaume wakware, wanalazimika kuwapunguzia wateja kiwango cha mshiko.





“Kabla ya hali hii ngumu, mwanaume akitaka kuondoka na mimi lazima anipe shilingi elfu 20 keshi, siku hizi hadi elfu 5 napokea, nitafanyaje sasa?” alihoji Rehema.

Kahaba mwingine, mwanadada mtu mzima aliyekutwa na gazeti hili pembeni ya kituo cha mafuta maeneo ya Sinza Mori alisema katika kipindi hiki cha ukame, wasichana ndiyo wanaondoka kidedea.

“Mimi leo nimeingia hapa (kazini) saa nne usiku, lakini mpaka muda huu (saa saba) sijamwona mwanaume wa kuniongelesha. Hawa machangu wadogo ndiyo wanakula nyomi,” alisema kahaba huyo aliyedai anaitwa Dija mwenye umri wa miaka 41.





KUTOKA KWA MHARIRI;
Wito wa gazeti hili ni kwa serikali kuweka mazingira ambayo yatawasaidia hawa akina dadapoa wanaoishi kwa kutegemea biashara ya kuuza miili wafanye kazi nyingine.

Hii pia itasaidia kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ambapo utafiti unaonesha kuwa, ukahaba nao unachangia.     

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...