Thursday, September 8, 2011

TASWIRA YA YESU YAONEKANA MAWINGUNI HUKO REUNION

Taswira kama ya Yesu ilivyoonekana katika milima Kisiwa cha Reunion.

Mwonekano wa karibu wa kilichoonekana. 

MUUJIZA wa kidini umeonekana kwenye milima mitakatifu ya Kisiwa cha Reunion ambapo mpiga picha wa video wa Ufaransa aitwaye Luc Perrot, aliunasa kwenye kamera yake ukionyesha taswira ya Yesu.

Kisiwa cha Reunion ni eneo la nje la Ufaransa na  kiko Mashariki mwa Madagascar katika Bahari ya Hindi.

Mpiga picha huyo alikuwa eneo la juu la kilele cha mlima Cirque huko Mafate ambapo alinasa taswira ya mikono miwili iliyokuwa imenyooka kila upande kutoka katika mawingu yaliyokuwa angani.

Perrot hakuamini macho yake baada ya kuona hali hiyo, ambapo aligundua pia kwamba taswira hiyo ilikuwa pia imezungukwa na duara yenye nuru ambayo huzunguka vichwa vya watakafitu.

Mwonekano huo ulionaswa Julai 10 mwaka huu, bado haujaelezewa kisayansi chanzo chake.

“Nilikuwa nachukua picha za video katika mlima Cirque na baadaye nikaelekeza kamera yangu maeneo ya mbali angani,” alisema mpiga picha huyo na kuongeza kwamba baadaye akaona kivuli kikielea huku kikiwa kimezungukwa na upinde wa mvua, jambo ambalo lilimshangaza.

“Baadaye niliona mwanga mweupe wa nuru ukiwa umekizunguka kichwa cha taswira hiyo,” alisema katika mahojiano.

Mwezi uliopita, mtu mmoja huko Canada alinasa wingu lililokuwa na taswira ya moja ya miungu wa Kirumi likipita eneo la uani mwake.  Tukio hilo lilijiri kabla ya kunyesha mvua kubwa.  Hata hivyo, jambo hilo limeelezewa kuwa ni “maajabu ya kawaida”.

Je, huo ni mwanga wa watakatifu au upinde wa mvua?

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...