MWANAMUZIKI mwenye heshima tele ndani ya Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ a.k.a Kiuno Bila Mfupa, amepokea kipigo alipokuwa akifanya shoo katika nchi inayotawaliwa na Rais Mwai Kibaki, Kenya...
Tukio hilo la kufedhehesha kwa mwanadada huyo ambaye amehamishia majeshi yake nchini humo, lilijiri Septemba 3, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Club Sea Front uliopo Mombasa kulikokuwa na Shoo ya Project Fame All Stars Special Tour.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha The Udaku Master, kilichokuwa kimeweka kambi ukumbini humo ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake, shoo hiyo ilikuwa ni maalum kwa washiriki wa Shindano la Project Fame wakiwemo Peter Msechu na Hemedy Suleiman huku Ray C akiwa mtumbuizaji mkuu.
SHOO YAANZA KWA UTULIVU
Chanzo kilidai kuwa, shoo ilianza kwa utulivu huku mashabiki wakiwashangilia Hemedy, Msechu na wasanii wengine kutokana na burudani waliyokuwa wakiiporomosha.
“Kwa kweli mwanzo mambo yalikuwa mazuri, watu walikuwa wakishangilia sana kutoka na burudani kali iliyokuwa ikitolewa. Hakukuwa na dalili za shoo kutibuka,” alisema mnyetishaji huyo.
OJ WA KENYA APANDA, RAY C ATIBUA
Ilidaiwa kuwa, baada ya wasanii kadhaa kupafomu, alipanda msanii mwingine kutoka Kenya aliyefahamika kwa jina la kisanii la OJ ambapo aliimba kwa muda mfupi huku mashabiki wakimshangilia.
Ilinyetishwa kuwa, wakati OJ akiendelea kushusha mistari, Ray C ambaye muda huo alikuwa bwiii, alipanda stejini na kufanya mambo ya ajabu.
“Mashabiki walishangaa kumuona Ray C akiwa tilalila ambapo alivamia jukwaa na kumpokonya ‘maiki’ OJ na kuanza kuongea maneno yasiyoeleweka huku akitukana, kitendo kilichowakera sana watu,” alidai mtoa habari huyo.
MABAUNSA WAMSHUSHA STEJINI
Kutokana na fujo alizokuwa akifanya na matusi aliyokuwa akiyaporomosha, mabaunsa walilazimika kumshusha Ray C stejini kwa nguvu, kitendo kilichowafanya baadhi ya watu kuanza kumfanyizia.
“Midume ilimzunguka, ikaanza kumbonyeza kizenji huku wengine wakimpiga kwa kuwaharibia burudani.
“Liliibuka varangati la ukweli na kama siyo wale mabaunsa, angefanyiwa kitu kibaya zaidi ya kile alichofanyiwa kwani hata nguo alizokuwa amevaa zilikuwa zimeacha nje sehemu kubwa ya mwili wake,” kilisema chanzo hicho.
SHOO YASAMBARATIKA
Ilielezwa kuwa, kutokana na timbwili hilo lililosababishwa na Ray C, shoo ilivunjika huku wadau wengi wakimlaumu mwanadada huyo kwa kufanya mambo ambayo hayakutarajiwa.
Hivi karibuni Ray C aliamua kuhamishia makazi na shughuli zake za kimuziki Nairobi nchini Kenya licha ya kwamba tangu achukue uamuzi huo amekuwa akikumbwa na misala ya hapa na pale.
Juhudi za kumpata Ray C kuzungumzia ishu hiyo ziligonga mwamba kufuatia namba yake kutokuwa hewani kila ilipopigwa. Jitihada zinaendelea na akipatikana ze utamu litawaletea maelezo ya upande wake.
KUTOKA KWA MHARIRI
Ray C bado ni jembe kwenye muziki wa Bongo Fleva na anakubalika sana hivyo anatakiwa kujiangalia upya ili aweze kufanya kile kinachotakiwa na wapenzi wa burudani ya muziki na siyo kufanya mambo yanayomdhalilisha.
Ray C bado ni jembe kwenye muziki wa Bongo Fleva na anakubalika sana hivyo anatakiwa kujiangalia upya ili aweze kufanya kile kinachotakiwa na wapenzi wa burudani ya muziki na siyo kufanya mambo yanayomdhalilisha.
No comments:
Post a Comment