Thursday, September 29, 2011

Sintah na Nature tena........


Kweli adui mpenzi ni laini kwa nyama ya ulimi, wawili wanaopendana kwa dhati hawaachani ila hupumzishana kupisha hasira ziishe, kuhusu mastaa Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’ na Christine John Manongi ‘Sintah’ ni stori ya MV Mapenzi.

Habari zinasema kuwa Nature na Sintah hivi sasa hawana bifu, wamesahau tofauti zao, wapo pamoja hivyo kuibua ‘ndogo ndogo’ kwamba wamerudiana tena baada ya bifu la miaka tisa.

The 5star BLOG inajua kuwa Nature ni mume wa mtu lakini limenasa mazungumzo yake na Sintah ambayo yanatengeneza picha kuwa ama wamerudiana kweli au kuna kitu kinaendelea kati yao.
Chanzo chetu cha kwanza kabisa kiliandika SMS: “Wanaogombana ndiyo wanaopatana, Sintah na Nature sasa mambo yao ni bambamu.”

Katika kuifanyia kazi SMS hiyo, UTAMU ilimpigia simu ‘sosi’ huyo na neno lake likawa: “Nyie fuatilieni mtajua. Nature si aliwahi kuimba kwamba inamuuma sana? (Inaniuma Sana), basi kwa taarifa yenu, hivi sasa haimuumi chochote.”

BLOG hii iliendelea kufanya kazi kwa kuwasiliana na mtu wa karibu na Sintah ambaye baada ya kuombwa aseme anachokijua, kwanza alicheka kisha alijibu: “Mnachelewa sana kujua, Sintah na Nature kwa sasa siyo maadui.”




Hata hivyo, ilipombana ‘sosi’ huyo aeleze uadui wao umeishaje, alisema: “Hayo mambo nadhani Sintah au Nature ndiyo wanapaswa kueleza. Ila najua hivi sasa wanawasiliana vizuri, hawana uadui tena. Kuhusu kwamba ni wapenzi, hilo nakataa.

“Nature ana maisha yake na mke wake. Hana uhusiano wa kimapenzi na Sintah hivi sasa, ila wanawasiliana kama marafiki, zaidi kama wasanii.”

Wakati gazeti hili likiendelea kusaka kiini cha ukweli, ‘sosi’ mmoja alimueleza mwandishi wetu: “Sikuamini kama Nature anaweza kurudiana na Sintah, nimepewa taarifa za uhakika kabisa kuwa wale ni wapenzi, nashangaa kwa sababu najua Nature ni mume wa mtu, Sintah pia alikuwa na wake, jamani hawa mastaa!”

MAZUNGUMZO YANOGA
Uchunguzi wa umebaini kuwa Nature na Sintah hivi sasa wanawasiliana kwa kiwango ambacho kinadhihirisha jinsi wanavyoelewana.

Makachero, walifanya kazi yao kikamilifu na kunasa mazungumzo ya hapa na pale kati ya mastaa hao lakini kile hasa walichokuwa wanaongea kinabaki sirini. 


KIPI KIPO KATIKATI?
Sintah alipozungumza na BLOG hii alisema: “Sijawahi kuwa na uadui na Nature, sihitaji kuzungumza yaliyopita lakini kwa sasa ni kweli tunawasiliana vizuri kwa sababu tunataka kufanya kazi pamoja.

“Kuna filamu tunacheza pamoja, inaitwa Sitaki Demu. Kwa hiyo mimi na Nature ni marafiki kikazi. Kuhusu mapenzi hapana, namheshimu sana Nature, yule ni mume wa mtu, namheshimu sana mke wake. Nami nina mtu wangu, nampenda na kumheshimu sana.”

Nature alisema: “Tunatengeneza filamu, kwa sasa tumesimama, Sintah yupo busy na kazi zake, akishakaa sawa tutakamilisha filamu. Ni kazi tu, hakuna kingine.”



UNAKUMBUKA SITAKI DEMU?
Nature na Sintah walizama kwenye penzi zito mpaka kutangaza kufunga ndoa lakini mwaka 2002 waliachana, huku mwanamuziki huyo akimtuhumu mwenzake kwa kutokuwa mwaminifu.

Baada ya kuachana, kikapita kipindi cha bifu ambapo Nature alidaiwa kurekodi nyimbo mfululizo akieleza madudu ya Sintah. Ngoma hizo ni Sitaki Demu (Original na Remix) pamoja na Inaniuma Sana.

Mwaka 2003, wakati Nature akiwa kwenye ziara ya muziki Mwanza, Sintah alipanda jukwaani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na kucheza wimbo Sitaki Demu.

Nature ambaye alikuwa anaimba, baada ya kumuona Sintah akicheza jukwaani alisusa kuimba, hivyo kutibua shoo hiyo ambayo ilikuwa imeandaliwa na Prime Time Promotion ambayo ni kampuni tanzu ya Clouds Media Group.


Wakati huo, Sintah alikuwa mtangazaji wa Redio ya Watu, Clouds FM, Mwanza na kutokana na tukio hilo la kuhusika kuharibu shoo ya Nature, menejimenti ya redio hiyo, chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Joseph Kusaga, iliamua kumfukuza kazi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...