Saturday, September 17, 2011

Hiki ni kifo..

Huku Ukimwi ukitajwa kuwa ugonjwa hatari unaoambukiza kwa njia ya kufanya ngono, ugonjwa  mwingine wa hatari zaidi umeibuka unaodaiwa kuambukizwa kwa njia ya watu kunyonyana ndimi a.k.a denda.

Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda alisema ugonjwa huo kitaalam unaitwa Herpatitis C na B.

Imeelezwa kuwa, dalili zake zinafanana kwa kiwango kikubwa na zile za Ukimwi ila tofauti ni kwamba mgonjwa mwenye Herpatitis hubadilika rangi na kuwa wa njano kabla ya kufariki dunia.

Dk. Mponda alisema ugonjwa huo ulikuwa nchini muda mrefu na ulikuwa haujulikani kwa wengi lakini sasa umeibuka kwa kasi na kuleta tishio la kusababisha vifo vya watu wengi.

“Huu ugonjwa ni wa siku nyingi sana ingawa ni watu wachache wenye ufahamu nao,” alisema waziri huyo.

 Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na BLOG hii umebaini kuwa, ugonjwa huu una nafasi ya kuwakumba wengi kutokana na baadhi kutoufahamu na kutojua kuwa unapatikana kwa njia ya kunyonyana ndimi.

Imebainika kuwa, wengi wamekuwa wakidhani kufanya hivyo ni njia salama ya kujiridhisha kimapenzi bila kufanya ngono kwa kutotambua kwamba njia hiyo pia ina madhara makubwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya watu walisema hawaufahamu ugonjwa huo hivyo kwa mazingira hayo kuna uwezekano wengi wameshaambukizwa au kuambukiza.

“Mimi ndiyo kwanza nausikia, nimekuwa nikifanya hivyo na wasichana wengi hasa wale ambao siwaamini, licha ya kwamba inaelezwa kuwa kupitia mate pia mtu anaweza kuambukizwa Ukimwi kwa asilimia f’lani, lakini siyo sawa na kufanya ngono na muathirika.

“Kwa maana hiyo wengi tutakuwa na ugonjwa huo, wengine wataendelea kuambukiza endapo elimu haitatolewa,” alisema Saidi Karim mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam.












Naye Jasmin John wa Kariakoo alisema kuwa, ugonjwa huo ni mpya kwake na ameshangazwa na taarifa kwamba unaua watu wengi kuliko Ukimwi.

“Duh! Umenishtua kweli, wanaoridhishana kimapenzi kwa njia ya kunyonyana ndimi ni wengi na kama ni kufa kwa ugonjwa huu, wengi tutakufa hasa wale walio na uelewa mdogo, hili sasa ni balaa lingine,” alisema Jasmin.



Katika siku za hivi karibuni vitendo vya watu kudendeka vimekuwa vikichukua nafasi kubwa katika jamii huku baadhi ya mastaa wakifikia hatua ya kutoona hatari ya kufanya hivyo hata kwenye kadamnasi.




No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...