Sunday, September 18, 2011

NDEGE NDOGO YADONDOKA JIJINI MBEYA ASUBUHI YA LEO



HABARI ZILIZO TUFIKIA MUDA HUU ZINATUPASHA KWAMBA MNAMO MIDA YA SA MBILI NA DAKIKA HAMSINI LEO ASUBUHI ZINASEMA KUWA KUNA NDEGE NDOGO IMEDONDOKA MAENEO YA UYOLE.. HABARI ZAIDI ZINASEMA KUWA NDEGE HIYO ILIKUA NA ABIRIA WA NNE NDANI YAKE LAKINI HAKUNA ALIYE POTEZA MAISHA BALI ABIRIA MMOJA TUU NDIE AMEUMIA.

Imetokea majira ya saa tatu eneo la Nanenane Uyole jijini Mbeya na abiria wanne wanusurika kifo na hakuna aliyefariki.
Abiria walionusurika kifo ni pamoja JVER WAAK Umri wa Miaka 49 ambayealikuwa Rubani, Raia wa Afrika Kusini, Bwana CHRISTIAN BASIL MMASI umri miaka 30, Ambaye ni Afisa Utawala wa mashamba ya Kapunga wilaya ya Mbarali, Balozi MOHAMMED RAMIA kabula leke ni Mmakua mwenye umri wa miaka 64, mkazi wa Masaki jijini Dar es Salaam ambaye ni mfanyakazi EXPORT TRADING na Bwana SUNNY TAYIR mwenye umri wa miaka 50 ambaye ni Mhindi na ni mfanyakazi wa EXPORT TRADING.

Imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Bwana ANACLET MALIMBISA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...