Thursday, September 29, 2011

WOLPER: maisha yangu fedha mbele




MSANII wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe amekiri kuweka fedha mbele katika maisha yake huku akidai kuwa, hicho ndicho kilichomtoa Moshi kuja jijini Dar es Salaam.
Akizungumza juzikati jijini Dar,  Wolper alisema, linapokuja suala la fedha huwa hataki utani kwani lengo lake ni kutimiza ndoto zake na si vinginevyo.
Mimi ni Mchaga bwana, nimekuja Dar es Salaam  kutafuta fedha na siyo kutafuta mambo mengine,  hivyo niachwe nizisake kwa njia nizijuazo.
Ndiyo maana niko tayari kumpeleka polisi yeyote atakayenizingua katika suala la ‘mshiko’,” alisema Wolper.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...