Saturday, April 14, 2012

WEMA: SIJAWAHI KUACHANA NA KANUMBA




SIKU chache baada ya kifo cha muigizaji mkubwa katika tasnia ya filamu Bongo, marehemu Steven Charles Kanumba, Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu amefunguka kuwa hakuwahi kuachana na muigizaji huyo.

Akizungumza kwa sauti iliyoambatana na kilio cha kwikwi katika mahojiano maalumu na kituo kimoja cha redio nchini, Wema alisema kuwa ingawa jamii ilikuwa ikifahamu kuwa ameachana naye, ukweli ni kwamba bado walikuwa wapenzi kwa siri.


“Tulikuwa na mapenzi ya siri kati yetu na tulifanya hivyo kwa kuwa kila mtu alikuwa tayari ana mtu wake, ndiyo maana hatukuwa wazi,” alisema Wema katika mahojiano hayo.


Akizungumzia faida aliyoipata akiwa na Kanumba enzi za uhai wake, Wema alisema kuwa ustaa wake katika filamu unatokana na marehemu ambaye alimshauri aingie kwenye tasnia hiyo.
“Kanumba ndiye aliyegundua kipaji changu ambacho leo hii kinanifanya nionekane staa wa filamu ndani na nje ya nchi,” alisema.

1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...