Sunday, April 22, 2012

MAAJABU KABURI LA KANUMBA... • Marehemu Steven Charles Kanumba.

 • MAAJABU! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, kaburi la aliyekuwa nguli wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ limeanza kuweka nyufa na kutitia ikiwa ni chache tu tangu alipozikwa...

 • USHUHUDA
 • Mwishoni mwa wiki iliyopita, waandishi walifika katika nyumba hiyo ya milele ya marehemu Kanumba kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar na kushuhudia hali hiyo huku nyomi ya watu mbalimbali ikiendelea kumimika eneo hilo kuweka mashada ya maua.

 • WATU KUTOKA MIKOANI
 • Kama hiyo haitoshi, baadhi ya watu waliofika kutoka mikoani ambao hawaamini kama kweli marehemu Kanumba hatunaye, walipiga picha ili kupeleka ushahidi huko walikotoka.
 • Pamoja na kuona kaburi, pia waliona maajabu kwenye nyumba hiyo ya milele ya marehemu Kanumba iliyooneka kupasuka nyufa na kutitia ukilinganisha na ‘levo’ za makaburi mengine yaliyopo jirani.

 • LINAHITAJI KUKARABATIWA
 • “Kama hali ndiyo hii, kaburi la Kanumba linahitaji kukarabatiwa kwani ni mapema mno kuwa na nyufa na kutitia,” alisema mmoja wa akina dada waliofika mahali hapo kupiga picha na kaburi hilo.
 • Siku ya mazishi ya marehemu Kanumba Aprili 10, mwaka huu, watu wengi walitamani kushuhudia jinsi ambavyo anaingizwa kwenye kaburi hilo ambalo liligharimu zaidi ya Sh. milioni 1.5, lakini hawakuweza kulifikia kutokana na umati mkubwa.

 • TUJIKUMBUSHE
 • Kanumba alifariki dunia Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwake maeneo ya Vatican City Hotel, Sinza jijini Dar baada ya kuanguka chumbani kwake akiwa na mpenzi wake, msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...