Friday, April 20, 2012

GARI LA MASHINDANO MAREKANI LALIPUKIA, DREVA ANUSURIKA


Gari la Matt Hagan likilipuka kwa moto.

Matt Hagan akitoka kwenye gari hilo.

Matt Hagan.


PICHA za video zimeonyesha gari lililokuwa katika mashindano kwenye kasi ya maili 260 kwa saa, sawa na kilometa 418 kwa saa likilipuka na kumwacha dreva wake akiwa mzima wa buheri.

Dreva huyo, Matt Hagan, alinusurika katika ajali hiyo huko Charlotte, Carolina ya Kaskazini, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo video zilionyesha injini za “gari hilo la ajabu” ikipasuka katika mashindano ya Four-Wide Nationals.

Dreva huyo alionekana kutoshitushwa na tukio hilo kwani aliweza kulidhibiti gari hadi likasimama.
Baadaye hamaki ilifuata ambapo si kwa vile alinusurika katika ajali hiyo, bali kwa kushindwa kumalizia shindano hilo. Video hizo zinamwonyesha Hagan akitoka katika gari hilo ambalo lilikuwa likitoa moshi ambapo anaokota kipande cha gari hilo lililoharibika na kukitupilia mbali.

Ripoti zinasema huu ni mwaka wa tatu mfululizo kwa gari lake kulipuka katika mashindano hayo.
CHANZO: SKYNEWS

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...