Thursday, April 19, 2012

PICHA YA PAMOJA YA LULU NA KANUMBA YANMASWA... ILIPIGWA MWAKA 2006



PICHA pekee ambayo marehemu Steven Kanumba amepozi na aliyekuwa mpenzi wake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ waliyoipiga kwa mara ya kwanza wakiwa pamoja imenaswa.

Picha hiyo inadaiwa kupigwa mwaka 2006 ambapo wawili hao walikuwa wakirekodi filamu iliyofahamika kwa jina la Ripple of Tears.

Katika picha hiyo, Lulu ambaye kwa kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 11 kama kweli mwaka huu (2012) anatimiza miaka 17 kwa mujibu wa baba yake, Mzee Michael.

Kwa maana hiyo, marehemu Kanumba alikuwa na umri wa miaka 22, walipishana miaka 11.
Katika picha hiyo, Lulu anaonekana akilamba koni huku wakiwa wanaondoka kwenye eneo walilonunulia ambalo ni la ‘take away’.

Akiizungumzia picha hiyo, msanii mmoja wa filamu aliyeomba jina lake lisiandikwe alimwambia mwandishi wetu kuwa, anakumbuka kipindi hicho ndipo Kanumba alipoanza kurekodi na Lulu.

“Hii ndiyo picha ambayo Lulu na Kanumba walipiga kwa pamoja kwa mara ya kwanza, ilikuwa mwaka 2006 ambapo tulikuwa tukirekodi filamu ya Ripple of Tears,” alisema msanii huyo.

Hata hivyo, hakuna taarifa zozote zinazoenesha kuwa wawili hao walikuwa wapenzi mwaka huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...