Monday, April 23, 2012

JINSI LULU ALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI LEO NA KILICHOSEMWA.





Mahakama ya hakimu mkazi KISUTU jijini Dar es Salaam leo imeahirisha kesi ya tuhuma za mauaji inayomkabili ELIZABETH MICHAEL maarufu kama LULU dhidi ya mwigizaji maarufu Marehemu STEVEN KANUMBA.

Wakili wa Upande wa Serikali ELIZABETH KAGANDA akizungumza mahakamani hapo ambapo kulikua na watu wengi waliokuja kusikia kinachoendelea, amedai Upepelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba itatajwa tena mei 7 mwaka huu.

Hii ni mara ya Pili kwa ELIZABETH MICHAEL kupandishwa Kizimbani kwa kosa la mauaji Marehemu Steven Kanumba April 7 mwaka huu Sinza Vatican Jijini Dar es Salaam. (Stori kutoka sophiakessy.blogspot.com)

1 comment:

  1. ila jaman upelelezi ufanyike pasipo upendeleo mm naiomba selikari juu ya hili

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...