Monday, April 9, 2012

WADAU WATOA HISIA ZAO KWA JINSI WALIVYOGUSWA NA KIFO CHA STEVEN KANUMBA.



I-VIEW MEDIA
We had argument few days ago with kanumba concerning this photograph which is a movie cover named MOSES... TWICE HE MENTIONED TO ME THAT THIS IS HIS FAVOURATE PHOTOGRAPH EVER..
THIS PHOTO WILL HAVE ITS USE AT HIS FUNERAL IF THE FAMILY ALLOW US TO DO SO

JAKAYA MRISHO KIKWETE
Nimepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Ndugu Steven Charles Kanumba. Kupitia filamu zake, ameburudisha na kuelimisha jamii yetu kwa namna ambayo haiwezi kupimika. Alikuwa msanii mahiri na mwenye kipaji kikubwa ambaye mchango wake mkubwa katika kuanzisha, kukuza na kuimarisha sanaa ya filamu nchini hautasahaulika. Kanumba pia ametoa mchango mkubwa katika kuitangaza nchi yetu ya Tanzania mbele ya mataifa mengine kupitia sanaa ya filamu na uwezo mkubwa wa kisanii. Tutaendelea kumkumbuka kwa mchango wake huo kwa nchi yetu. Namwomba Mwenyezi Mungu awape subira na nguvu wadau wote wa tasnia ya filamu nchini za kuweza kuhimili kipindi hiki kigumu kwa sababu yote ni mapenzi yake. Aidha, naungana na wanafamilia na wasanii wote kuwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema peponi roho ya Marehemu Steven Charles Kanumba. Amen.

REGINALD MENGI (M/kiti wa makampuni ya IPP).
Its always very painful to lose young talents. R.I.P Kanumba

PROF JAY (Bongo Fleva Artist)
Daaah Gone too soon...REST IN PEACE KANUMBA THE GREAT.


PRODUCER MANECKY kutoka AM REC
Kama studio hivi nagonga ngoma flan yenye fillings kali mana naona kama Roy vile ilivyokuwa kama story kumbe kweli The Great ndo Katangulia..Mungu amlaze Mala Pema PePoni

WAKAZI (Bongo Fleva Artist)
Sijawahi kukutana na STEVE KANUMBA na wala sijawahi kuona Movie yake hata Moja, ILA impact yake kwetu ilinilazimu kumuweka in my Punchline in a Song called HIGHER "...Baller Kutoka Ukonga kama Sheby Kazumba/ Plus My Life is a Movie, Steve Kanumba/..."

Only GREAT People have had the Priviledge of makin it on my Name drop List, and for that, You didnt make a mistake callin your self just that.... Rest In Peace Steve Kanumba The Great!! © Wakazi

ROMA (Bongo Fleva Artist)
Dakika...chache baada ya show yangu ya musoma!! Napata taarifa za huu msiba wa THE GREAT K.A.N.U.M.B.A....sikuamini mpaka nilipopiga simu kwa mmoja wa mtu wake wa karibu na kunijibu huku analia kuwa bro hatunaye kweli na ndo' wao wanatoka muhimbili!!....ni msiba mzito na umewagusa wengi nikiwemo!! Pole sana kaole...pole game 1st quality...pole kwa mpinzani wake mkubwa Ray....pole kwa ben swahiba wake sana....dah pole kubwa kwa pacho mwamba!familia yake Na bongo movie wote...pamoja na watanzania wote!! TUTAKUKUMBUKA KWA MENGI KAKA STEVE.....Tumuombee ndugu ye2 apumzike pema peponi!!na asamehewe dhambi zake!! Oooh kaka umetuacha ukiwa angali mdogo...inauma sana!!


MRISHO MPOTO (Bongo Fleva Artist)
NILIDHANI NIMESHAZOEA KUSIKIA HABARI ZA KUSHITUA, LAKINI KWA HII YA KANUMBA? SINA NGUVU TENA, KAMA MOSHI UMEKWENDA HAUTARUDI, KAMA JANI KWENYE MTI LIKIDONDOKA HALIRUDI. KANUMBA TUPE ANGALAU DAKI MOJA TUKUAGE RAFIKI YANGU, NAKUMBUKA UTANI WETU "FITINA MWAKA WAKO HUUMOJA" UMIMEBAKI HISTORIA KWELI? RUDI JAPO TUSEME NENO KWAHERI


MILLEN MAGESE (Fashion Model)
Rest in Peace my friend...you create jobs ,you believed on our own...and you took them as ur own and give them opportunities to believe on themselves and be who they wanna be and take acting as their career....Where do they go now.....Kanumba!!!? Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi...Pigo la taifa jamani..Poleni Kaole poleni Tanzania...!


SOLO THANG (Bongo Fleva Artist)
R.I.P STEVEN KANUMBA,,,Mungu amekupenda zaid,,Pole kwa familia na ndugu wa karibu na wapaenzi wa bongo movie kwa ujumla,,,gone too soon Hommie!


JOYCE KIRIA (Mtangazaji)
sio Watengeneza Film tu, ila Watanzania tumepoteza kijana muhimu sanaa katika nchi yetu. Kifo hakikutenda haki kabisa, Kifo amekuwa mkatili na kila maneno tutasema. Ila mwisho wa siku tunasema Mapenzi ya Mungu yatimizwe. Bwana ametoa, na Bwana ametwaa jina la Bwana libalikiwe




AY (Bongo Fleva  Artist)
R.I.P Steven Kanumba!tulishauriana,tulipeana msukumo kwa mambo ya maendeleo binafsi na ya industry zote mbili.umezimika kama mshumaa uliokuwa unawaangazia wengine,wote tupo njia moja..Mungu akulaze mahali pema peponi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...