Monday, April 2, 2012

CHIDI BEENZ ATAJA SABABU ZA KUTOBOA PUA


picha kutoka djfetty.blogspot.com
Rapper Mfalme wa Ilala Chidi Benz baada ya kutoboa pua yake, amekubali kuzungumza EXCLUSIVE na millardayo.com nyumbani kwake  kuhusu chanzo cha yeye kufanya hivyo na sababu zake.
Chidi amesema “kila kitu ni mtu jinsi unavyoishi, mimi nilitoboa pua mara ya kwanza nilivyosafiri nikaacha pini kwa hiyo ikaziba kidogo kwa hiyo nilivyorudi nikaenda kutoboa tena, hizi ni hisia zangu na vitu vyangu nilivyoviona kwenye macho yangu pamoja na mimi mwenyewe ninavyoishi vitu vilivyonipitia binafsi mimi binafsi kama Rasheed nikajikuta siku tu nimeamka nikaenda town nikajitoboa nikalipa pesa nikarudi nyumbani baadae ndio nikagundua hivi nimetoboa pua”
.
Chidi amesema “ni alama ambayo nimeiweka kama ni maumivu basi nitayakumbuka yale maumivu na nisiumie tena, kama ni furaha basi nikumbuke ile furaha.. kwa hiyo mimi ndio ninaelewa, nashindwa kuelewa kama kuna watu wanachukulia tofauti kwa sababu unashangaa nini kutoboa pua na nikitoa pini pua inaziba kama kawaida, nini inasababisha uanamke au u**** kwa kutoboa pua, ukiamua unaamua tu kuna watu maaskari bwana na wanajeshi na watu wanasema huyo hivi na yule hivi kwa hiyo kwa kuongea kwako ovyo ntakushtaki kwa sababu itaziba na hutoniambia kitu unajua”
Kuhusu mashabiki wake kumuuliza maswali, Chidi ameiambia millardayo.com amesema “nimekutana na watu wengi sana wameniuliza kuhusu hili swala lakini nikijibu kama ninavyojibu mimi kwa maana yangu wananielewa lakini inategemea mtu ameniulizaje, akiniuliza kiheshima namjibu vizuri ila akija rafu namjibu eeeeh bwana kweli nimetoboa urembo tu najiremba ni kama vile binti kutoboa sikio sasa mimi nimetoboa pua”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...