Sunday, April 22, 2012

LULU: MASTAA BONGO WANAFIKI





Elizabeth Michael ‘Lulu’.
ELIZABETH Michael ‘Lulu’ amelonga akiwa lupango Segerea, Dar na kudai kuwa mastaa wa Kibongo ni wanafiki kwa sababu wanamjali mtu anapokuwa kwenye raha lakini akipata matatizo wanaingia mitini.

Lulu anayetisha kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, alisema hayo alipotembelewa kwa lengo la kumjulia hali Jumamosi ambapo alieleza kwa machungu jinsi mastaa walivyomtupa katika kipindi hiki kigumu kwake.

“Siyo siri, mastaa wakubwa wa Bongo ni wanafiki hasa wale wa filamu, hakuna aliyekuja kuniona lakini namshukuru Mungu naendelea vizuri,” alisema Lulu akilishukuru kwa kwenda kumjulia hali.

Aprili 11, mwaka huu, Lulu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar na kusomewa shitaka lake juu ya kifo cha Steven Charles Kanumba ambapo hakutakiwa kujibu chochote hadi atakapopandishwa tena kizimbani Aprili 23.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...